Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,176
- 17,635
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema hadi sasa hajaandika barua ya kuomba ruhusa ya kwenda kugombea ubunge hivyo yeye bado hana dhamira ya kuweka nia ya kugombea ubunge popote kama baadhi ya taarifa zinavyodai.
Akiongea Jijini Dar es salaam, RC Chalamila amesema "Kuhusu swali la je, Bwana Chalamila atarajiwe au asitarajiwe kwenye kugombea ubunge?, mtakumbuka Rais wa Tanzania alitoa maelekezo kwa Viongozi ambao wanatamani kwenda kugombea nafasi za ubunge, udiwani au nafasi zinginezo, na alitoa maelezo kwamba tuandike barua mapema ili tuweze kujulikana"
"Labda niwaeleze tu Waandishi wa Habari kwamba, Mimi kama RC sikuandika barua, na kwasababu sijaandika barua maana yake ni kwamba mpaka sasa bado sijaweka nia lakini hata kule ambako ninasikia manenomaneno kwamba Bwana Chalamila anakuja anakuja, nako zilikuwa ni hisia kwamba Bwana anakuja lakini kiukweli kazi hizi ambazo Mh. Rais ametupatia ni kazi kubwa na zina heshima yake na kwakuwa zote ni kazi za kutumikia Watu, ubunge na ukuu wa mkoa zote ni za kutumikia Watu, ebu kwa kipindi hiki nibaki na heshima hii ya Mh. Rais ya kutumikia Watu upande huu wa Serikali"
"Wapo baadhi ya Watu wanaeneza maneno kule tunakotokea, Mh. Rais anakataza Watu, kiukweli Mh. Rais alishatoa utaratibu na hawezi kumzuia Kiongozi yoyote wa kisiasa kutokwenda kuchukua fomu ya kuwania nafasi yoyote, alichotaka ni taarifa ili unapotoka mchakato wa vetting wa kumpata Kiongozi mwingine uweze kufanyika kwa uhuuru na sio kwa kwa ghafla, kwahiyo Mimi nilimzingatia kiasi cha kutosha, hizo zilikuwa ni hisia na kwasababu sijaandika barua ni kwamba Mimi bado sijawa na dhamira ya kutia nia"