RC Arusha apokea ujumbe wa Mabunge Duniani (IPU)

RC Arusha apokea ujumbe wa Mabunge Duniani (IPU)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
π—₯𝗖 𝗔π—₯𝗨𝗦𝗛𝗔 π—”π—£π—’π—žπ—˜π—” π—¨π—π—¨π— π—•π—˜ π—ͺ𝗔 π— π—”π—•π—¨π—‘π—šπ—˜ π——π—¨π—‘π—œπ—”π—‘π—œ (π—œπ—£π—¨)

β–ͺ️Kufanya Mkutano wa Mabunge Mkoani Arusha

β–ͺ️Wajumbe zaidi ya 1500 kutoka nchi wanachama wa IPU kuhudhuria

β–ͺ️Rais Dkt. Samia apendekezwa kuwa Mgeni rasmi

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA. Amos Gabriel Makalla mapema leo Alhamisi Disemba 04, 2025 ameupokea na kuzungumza na Ujumbe wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano mkubwa wa Mabunge unaotarajiwa kufanyika Mkoani Arusha na kuhusisha Maspika, Wabunge na Viongozi zaidi ya 1500 kutoka kote duniani.

Ujumbe wa IPU umeongozwa na Balozi Ande Filip, akiongozana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa Geneva,Uswisi Dkt. Hoyce Temu ambapo katika maelezo yake Balozi Ande amesema katika Mkutano huo, Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.

"Tanzania ni Mwenyeji na sababu kubwa ni ushiriki na historia yake katika IPU na kikubwa zaidi ni namna wao wanavyoiona Tanzania na sisi tumewahakikishia tupo tayari kuwapa ushirikiano kufanikisha mkutano huo mkubwa wa Kihistoria." Amesema Mhe. Makalla.

Mhe. Makalla amesema Mkutano huo ni fursa kwa Wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla na ukija wakati mzuri katika kudhihirisha amani, usalama na utulivu uliopo nchini na kuaminika kwa Tanzania Kimataifa, akiwataka wananchi kujiandaa kutumia fursa za ujio wa mkutano huo kiuchumi.

Kwa Upande wake Balozi Ande kwaniaba ya Maafisa wengine wa IPU, amesema Mkutano huo wa Kimataifa utafanyika kwa siku sita Jijini Arusha na kulingana na ratiba, washiriki wake kutoka kote duniani watakuwa na zaidi ya siku sita Mkoani Arusha ili kuwapa fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria na Vivutio vya Utalii vilivyopo Arusha na maeneo mengine ya jirani.
 

Attachments

  • IMG-20251204-WA0084.jpg
    IMG-20251204-WA0084.jpg
    73 KB · Views: 13
  • IMG-20251204-WA0088.jpg
    IMG-20251204-WA0088.jpg
    101.4 KB · Views: 10
  • IMG-20251204-WA0087.jpg
    IMG-20251204-WA0087.jpg
    72.5 KB · Views: 12
  • IMG-20251204-WA0086.jpg
    IMG-20251204-WA0086.jpg
    85 KB · Views: 12
  • IMG-20251204-WA0089.jpg
    IMG-20251204-WA0089.jpg
    90.3 KB · Views: 14
  • IMG-20251204-WA0085.jpg
    IMG-20251204-WA0085.jpg
    86.4 KB · Views: 14
Naona kama yale ya Royal Tour yanataka kujirudia - Ni full kutumia rasilimali, just for appearance...

Putting Lipstick on a Pig...
 
Mbona taarifa haijasema nili linaanza?
 
Back
Top Bottom