RC Arusha alipa WAHUNI ili kuvuruga uchaguzi wa Vijana Arusha

Meitinyiku L. Robinson

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
412
90
Katika hali ya kushangaza Mkoa wa Arusha umeonekana kugubwikwa na sintofahamu baada ya Chaguzi zinazoendelea ndani ya Chama kuonekana ama kuingiliwa au kutishiwa na vyombo vya dola.

Haya yamebainika leo baada ya Mkuu wa Mkoa anayemwakilisha Raisi katika Mkoa kuonekana kuingilia chaguzi hizi hasa uchaguzi wa kesho wa Vijana Mkoani Arusha baada ya kukutana na genge la wahuni wa katika Mkoa huu na kuwalipa fedha za wapiga kura ili kesho wafanye fujo na hatimaye kuvuruga uchaguzi huo.

Hili limesemwa na mmoja wa kijana aliyelipwa fedha hizo akisisitiza kuwa RC kawaahidi vile vile fungu jingine pale watakapokamilisha zoezi hilo akidai kuwa hayo ni maagizo kutoka ngazi za juu.

Baada ya kupatikana kwa habari hizi Vijana Mkoani hapa wameonekana wakiwa katika makundi wakiapa kuwa kama RC katumwa Mkoani kwa kazi ya kuwachagulia viongozi basi hayo yatajulikana kesho hata kama ni kwa damu. Mtoa habari kasisitiza kuwa kuna mtu ambaye system inamuhitaji ambaye ni lazma ashinde na asiposhinda basi fujo zifanyike.

Haya si ya kushangaza manake hata majuzi katika chaguzi za Wilaya hasa Wilaya ya Arumeru DC mmoja alisikika akisema kuwa asiposhinda yule anayehitajika basi kuna watu atawaweka rumande.

RC; katafadhalishwa yafuatayo,

Mosi, ofisi ya Mkoa ni mahala pa kumwakilisha Raisi na kutatua kero za Wananchi na si pango la wahuni na vikao vya magendo visivyo na msingi wowote kwa wananchi

Pili, awasiliane ba hao aliowapa kazi hiyo na asitishe mara moja la sivyo tutajikoki ipasavyo na Arusha hapatakuwa sehemu salama kwa kesho

Tatu, katumwa kuiwakilisha Serikali na si Chama

Nne, Awaachie vijana jukumu la kuamua manake hao ndio wajuao ni yupi atakaye wafaa

Tano, hela za wapuga kura zitumike kwa namna ambavyo imeidhinishwa na si vinginevyo

Sita, Akumbuke spidi aliyokuja nayo na aliyonayo sasa

Saba, Kama anadhani kukamata baadhi ya Vijana ni suluhu usiku ashauriane na mkewe juu ya usahihi wa jambo hili

MWISHO; Kiongozi alishapangwa yeye yu nani hata abatilishe????
 
Mwisho: kiongozi alishapangwa, yeye yu nani mpaka abatilishe??? Anguko kuu linakaribia! Hata hivyo kesho watu watapigwa na kitu kizito au chenye ncha nkali...mwiko kusema risasi
 
Saba, Kama anadhani kukamata baadhi ya Vijana ni suluhu usiku ashauriane na mkewe juu ya usahihi wa jambo hili

MWISHO; Kiongozi alishapangwa yeye yu nani hata abatilishe????

ha ha ha ha ha ...Mrs atasema nini kama maagizo yametoka juu?
 
hahahahahaaa..........mnageukana when it comes to uongozi kwenye lichama lenu!
 
ha ha ha ha ha ...Mrs atasema nini kama maagizo yametoka juu?

Nna Hakika akimshirikisha mke atashauriwa ipasavyo, Kama kamhanda angemshirikisha mkewe kisingetokea kilichotokea Nyololo. RIP MWANGOSI!
 
Katika hali ya kushangaza Mkoa wa Arusha umeonekana kugubwikwa na sintofahamu baada ya Chaguzi zinazoendelea ndani ya Chama kuonekana ama kuingiliwa au kutishiwa na vyombo vya dola.

Haya si ya kushangaza manake hata majuzi katika chaguzi za Wilaya hasa Wilaya ya Arumeru DC mmoja alisikika akisema kuwa asiposhinda yule anayehitajika basi kuna watu atawaweka rumande.

Tatu, katumwa kuiwakilisha Serikali na si Chama

Saba, Kama anadhani kukamata baadhi ya Vijana ni suluhu usiku ashauriane na mkewe juu ya usahihi wa jambo hili

Naunga mkono hoja.

Alafu wewe hukusikia kauli ya waziri mkuu, kuhusu kazi ya wakuu wa wilaya na mikoa?
 
Ni ukweli uliowazi hizi habari zitatufurahisha wana cdm. Lakini habari imekaa kiudaku zaidi kuliko uhalisia kwasababu zifuatazo.
Vijana wa ccm hapa Arusha hawapendi kujulikana maana ni aibu kubwa kujitambulisha kama mwana ccm hapa Arusha.
Nipo Arusha na nimepita maeneo ya jengo lao, stadium na mitaa ya Bondeni na sijayaona hayo makundi.
Sijawahi kusikia kuwa kuna "hela za wapiga kura" kwenye chama chochote maana ni rushwa.
Naiona habari hii kama utangulizi wa kuhalalisha fujo walizopanga kufanya kwenye uchaguzi wao na hawakawii kusema ni cdm!
 
...huyu sishangai kabisa. Ni rafiki mkubwa wa dhaifi na ndo maana alimwokota kule BK akiwa anapakua barua posta, akamtupa bagamoyo kama DC, bila shaka akamfunda na kumpigishwa twisheni kwa tule tubibi tusangoma twooote na then akapelekwa AR kwa kazi maalum kama hizi, za kusaidia wapambe wote wa RZ1 !! Lakini kule machalii sio wa kuchezea, si unakumbuka walimpopoa na nyanya mbovu pale sokoni...
 
Nchi yetu imeharibika kabisa hatuko salama kabisa namuonea huruma Jakaya Kikwete Legacy anayoacha ni piga ua uhuni mtupu RC,RPC,DC wote sasa wameingia kwenye kufanya fujo duuh kweli Tanzania ni maajabu ya dunia
 
Ni ukweli uliowazi hizi habari zitatufurahisha wana cdm. Lakini habari imekaa kiudaku zaidi kuliko uhalisia kwasababu zifuatazo.
Vijana wa ccm hapa Arusha hawapendi kujulikana maana ni aibu kubwa kujitambulisha kama mwana ccm hapa Arusha.
Nipo Arusha na nimepita maeneo ya jengo lao, stadium na mitaa ya Bondeni na sijayaona hayo makundi.
Sijawahi kusikia kuwa kuna "hela za wapiga kura" kwenye chama chochote maana ni rushwa.
Naiona habari hii kama utangulizi wa kuhalalisha fujo walizopanga kufanya kwenye uchaguzi wao na hawakawii kusema ni cdm!

Rushwa ndani ya ccm ni utaratibu wa kawaida sana, jana hujaona morogoro vijana wanadai chai na vigwangala kwanza ndipo wapige kura? ukiona mtu wa ccm analialia ujue kazidiwa fungu la kugawia wapiga kura.
 
Kama ni kweli aondolewe mara moha ukuu wa mkoa maana hajui kazi yake na tena atakuwa mvurugaji wa amani badala ya kujenga amani Mkoani kwake
 
"huyu mkuu wa mkoa wa arusha hatapaweza hapa" by lowasa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom