mamayoyo1
JF-Expert Member
- Jul 25, 2018
- 1,011
- 1,019
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amekuwa mbogo kwa watendaji wanaochelewesha ugawaji na usambazaji vitambulisho vya wajasiriamali katika maeneo yao mkoani humo.
Dk Mahenge alisema hayo baada ya kutembelea halmashauri mbalimbali, kukagua namna vitambulisho hivyo vilivyotolewa kwa wajasiriamali na Rais John Magufuli Disemba 10, mwaka jana vinavyosambazwa kwa wajasiriamali wadogo.
Hali ya usambazaji au ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali katika halmashauri hizo mkoani humo, haujashika kasi kubwa, hivyo aliwataka watendaji hao kuongeza kasi ili kufikia lengo la kukamilisha vitambulisho hivyo.
Mkuu wa Mkoa alifanya ziara katika halmashauri za Chamwino, Kongwa, Kondoa na ziara bado inaendelea katika maeneo mengine ili kuhakikisha usambazaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo unakamilika mapema.
Akiwa katika ziara wilayani Kondoa, Dk Mahenge aliwataka watendaji kuharakisha usambazaji wa vitambulisho hivyo kwa wananchi na viongozi wanatakiwa kuhamasisha wananchi kuvichukua.
Alitawaka watendaji kuongeza kasi kugawa vitambulisho lakini kusimamia na kuhakikisha kwamba wajasiriamali wasio na vitambulisho hivyo hawaruhusiwi kufanya biashara au shughuli zozote. akiwa wilaya ya Chamwino, Dk Mahenge alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Athuman Masasi kuharahakisha usambazaji wa vitambulisho hivyo vya wajasiriamali, badala ya kufanya kazi bila kuwa na vitambulisho.
Mkuuu wa Mkoa wa Dodoma alikabidhiwa na Rais Magufuli vitambulisho vya wajasiriamali 25,000, ambavyo alivigawa katika halmashauri zake kwa uwiano wa wingi wa idadi ya watu katika wilaya hiyo.
Katika mgawanyo huo, Jiji lilipata vitambulisho 5,000, Chamwino 4,000, Kongwa 3,750, Mpwapwa 3,500, Bahi na Chemba zote zilipata vitambulisho 2,750 kila moja, Kondoa Mji 2,500 na Kondoa Vijijini 750.