Raza: Kama fisadi ni fisadi, huo si ubaguzi wa rangi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
Raza: Kama fisadi ni fisadi, huo si ubaguzi wa rangi

Mwandishi Wetu Juni 3, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

ALIYEWAHI kuwa mshauri wa masuala ya michezo wa Rais wa Zanzibar Dk. Salmin Amour, Mohamed Raza, amezidi kusikitishwa na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, na hasa suala la kuporomoka kwa maadili, akihoji “iko wapi CCM ya mwaka 1977 iliyotokana na TANU na ASP?”

Raza ambaye wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, alimzawadia vifaa vya michezo Mbunge wa Same Mashariki kwa ajili ya shughuli za michezo jimboni kwake baada ya mbunge huyo kutunukiwa Tuzo na Marekani, wiki hii alizungumza na Raia mwema na kueleza masikitiko yake hayo.

“Wizi unatisha serikalini tena ukihusisha baadhi ya viongozi…zamani CCM ilikuwa haitaki mchezo wa namna hiyo na yeyote anayehusika hatua zilichukuliwa hata kama kiongozi anatuhumiwa tu, aliwekwa kwanza nje ya uongozi wa chama na serikali ili kupisha uchunguzi,”

“Lakini leo hii hili halifanyiki ndani ya CCM wapo viongozi watuhumiwa lakini wameachwa hawajasimamishwa, sisemi kwamba wana makosa moja kwa moja lakini kama mtu unatuhumiwa na kama unakipenda chama chako na huna shaka yoyote na huna uroho wa madaraka kwa nini usikae pembeni kupisha uchunguzi?

“Iko wapi CCM ya mwaka 1977 iliyozaliwa baada ya kuunganishwa kwa vyama vyenye uadilifu na uzelando wa TANU na ASP?” alihoji Raza.

Katika jitihada za kumwondoa katika lawama hizo Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Raza aliwatupia lawama wasaidizi wa kiongozi huyo mkuu wa nchi, akiamini kuwa hawezi kufanya mambo yote mazuri kwa nchi peke yake bila mwongozo mzuri na bora kutoka kwa wasaidizi wake.

“Kwanza, Rais ameonyesha utayari mkubwa wa kupiga vita ufisadi na ubadhirifu wa aina yoyote na ndiyo maana leo tunaweza kuzungumza hivi lakini utayari huu wa Rais unaonekana kupingwa kwa chini chini na baadhi ya wasaidizi wake. Kuna hali ya kulindana kuanzia katika chama hadi serikalini na taasisi nyingine.

“Kama chama kingekuwa kinamuunga mkono Rais bila shaka yoyote ni lazima watuhumiwa wengine wenye nyadhifa na ambao bado wako katika chama kama viongozi wangesimamishwa kwanza kupisha uchunguzi na kama watabainika safi warejeshwe huu ndiyo utaratibu bora wa chama bora au serikali bora,” alisema Raza.

“Leo hii utasikia au kuona baadhi ya viongozi wanashindwa kutembea mitaani mchana kwa kuhofia kuzomewa kuwa ni mafisadi…wengine wakitajwa wanajidai kuwa huo ni ubaguzi wa rangi…mimi nasema hakuna ubaguzi wa rangi katika suala la ubadhirifu.”

“Mtu utahukumiwa kwa matendo yako kama ni mwizi utaitwa mwizi na kama ni fisadi utaitwa fisadi hakuna cha ubaguzi wa rangi hapa…tusipotoshe watu. Matendo yenu ndiyo yanayotumiwa na wananchi kuwahukumu,” alisema Raza.

Pia Raza alionya kuwa chakula kilicholetwa na Serikali ya Japan, kwa ajili ya kuuzwa kwa wafanyabiashara kwa bei nafuu ili nao wawauzie wananchi kisiachwe kiwafikie mafisadi kwa kuwa watawalangua wananchi na hasa ikizingatiwa kuwa matendo yao yanathibitisha kuwa hawana huruma kwa wananchi masikini.

“Kuna mchele unatolewa na Japan ambao utauzwa kwa wafanyabiashara ni kweli kila mfanyabiashara anataka faida lakini malengo ya mchele huo yasiharibiwe wananchi wauziwe kwa bei nafuu, mchele huu usiingie mikononi mwa mafisadi,” alisema Raza ambaye pia ni mfanyabiashara.
 
na kuhusu huo mchele ya kweli anayosema manake mafisadi madili yote wao wanayatolea macho hili kujipatia faida nyingi.
 
Raza: Kama fisadi ni fisadi, huo si ubaguzi wa rangi

Mwandishi Wetu Juni 3, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Raza ambaye wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, alimzawadia vifaa vya michezo Mbunge wa Same Mashariki kwa ajili ya shughuli za michezo jimboni kwake baada ya mbunge huyo kutunukiwa Tuzo na Marekani, wiki hii alizungumza na Raia mwema na kueleza masikitiko yake hayo.

.

- Sawa sawa, tupo pamoja sana hapa.

Respect.

FMEs!
 
Raza: Kama fisadi ni fisadi, huo si ubaguzi wa rangi

Mwandishi Wetu Juni 3, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Katika jitihada za kumwondoa katika lawama hizo Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Raza aliwatupia lawama wasaidizi wa kiongozi huyo mkuu wa nchi, akiamini kuwa hawezi kufanya mambo yote mazuri kwa nchi peke yake bila mwongozo mzuri na bora kutoka kwa wasaidizi wake.

"Kwanza, Rais ameonyesha utayari mkubwa wa kupiga vita ufisadi na ubadhirifu wa aina yoyote na ndiyo maana leo tunaweza kuzungumza hivi lakini utayari huu wa Rais unaonekana kupingwa kwa chini chini na baadhi ya wasaidizi wake. Kuna hali ya kulindana kuanzia katika chama hadi serikalini na taasisi nyingine.

"Kama chama kingekuwa kinamuunga mkono Rais bila shaka yoyote ni lazima watuhumiwa wengine wenye nyadhifa na ambao bado wako katika chama kama viongozi wangesimamishwa kwanza kupisha uchunguzi na kama watabainika safi warejeshwe huu ndiyo utaratibu bora wa chama bora au serikali bora," alisema Raza.

"Leo hii utasikia au kuona baadhi ya viongozi wanashindwa kutembea mitaani mchana kwa kuhofia kuzomewa kuwa ni mafisadi…wengine wakitajwa wanajidai kuwa huo ni ubaguzi wa rangi…mimi nasema hakuna ubaguzi wa rangi katika suala la ubadhirifu."

"Mtu utahukumiwa kwa matendo yako kama ni mwizi utaitwa mwizi na kama ni fisadi utaitwa fisadi hakuna cha ubaguzi wa rangi hapa…tusipotoshe watu. Matendo yenu ndiyo yanayotumiwa na wananchi kuwahukumu," alisema Raza.

- Finally, amejitokeza mwanaume na kumpa support Mengi, tena hadharani mchana kweupe wakati wengine wanajificha ficha, Mungu hawezi kumtupa mja wake pamoja na mapungufu yake lakini Mengi anajaribu kutusaidia sisi wananchi na hawa manyang'au na kwa hili Raza anahitaji heshima tena nzito sana, yaani kumpa support Mengi when it is needed yaani now!

- wakuu kesho Jumapili huko makanisani tumkumbuke kumuombea mzee wetu huyu Mengi maana kuna waliomkamia sana na inatisha sana, I mean CC iliyopita kidogo mafisadi wale mtu huko ndani ya kikao kwa hasira dhidi ya Mengi, Mungu apishile mbali na walegee wote, hasa Sophia Simba na ulegee!

Maneno mazuri sana mkuu
 
Mhh...pamoja na RAZA? Yale yale ya kuwa pamoja na kina Lowassa, Rostam na wengineo.....

omarilyas

- Hamna three ways about it Either uko na Mengi/Wananchi/Raza au Makamba/Rostam/Lowassa, hakuna middle ground wala neutrality!

- Uko wapi mkuu?

Respect.

FMEs!
 
- Finally, amejitokeza mwanaume na kumpa support Mengi, tena hadharani mchana kweupe wakati wengine wanajificha ficha, Mungu hawezi kumtupa mja wake pamoja na mapungufu yake lakini Mengi anajaribu kutusaidia sisi wananchi na hawa manyang'au na kwa hili Raza anahitaji heshima tena nzito sana, yaani kumpa support Mengi when it is needed yaani now!

Respect.

FMEs!

Naunga mkono haya ya Raza.
Raza akiongea ni kama mawazo ya vigogo kule Zenj.Upepo wa mueleko wa mafisadi naona wanaupata kisawasawa.
Sasa kinaeleweka na inaelekea paka lazima atafungwa kengele kabla ya 2010.
 
Hayo ni mawazo potofu. Jiitahidi umuelewe Raza.
 
Hayo ni mawazo potofu. Jiitahidi umuelewe Raza.

Ni kweli si ajabu uelewa wangu mdogo mkuu.Lakini kwa kadri nionavyo mimi, wale waliolia (ikiwa ni pamoja na mawaziri wetu) kuwa kuwataja vinara wa wizi wa fedha za umma (ambao wengi ni waasia) ni ubaguzi wa rangi.

Sasa pamoja na ufinyu wa argument hiyo, kuwa, kuwa taja mafisadi hao ni ubaguzi,Raza kwa upande wa Tz Visiwani amepasua jipu na kwajibu-kisiasa wale wanao jipendekeza kwa mafisadi.
Nani asiyemjua mwanamichezo Raza "mshauri" wa Kommadoo Salmin.
Sasa ndugu yangu Pakacha uelewa wangu unaishia hapo hebu wewe tumwagie wa kwako!!
 
Salimin siyo Rais na Raza siyo Mshauri wa Rais hivi sasa. Raza hata si kiongozi wa shina (Balozi) kule CCM. Raza ni mropokaji tu kama mimi. Lakini sawa, ndio demokrasia hiyo, tunaruhusiwa kuropoka- tukipenda- almuradi hatuvunji sheria.
 
Sasa mkuu Pakacha inaelekea uelewa wako ndio una walakin.
Raza hana mamlaka yoyote ndani ya SMZ na hata CCM hilo ni wazi.
Sasa wewe, Pakacha, vua shati lako na ukayaongee hadharani yale aliyoongea Raza pale Kibanda Maiti, na shuhudia valangati utakalolipata.
Raza "mshauri" , kwa muda mrefu sana ameetumika kama "vent valve" ya kuongea mambo nyeti ya kisiasa na wanasiasa wa Zenj kwa yale wasiyopenda wao wenyewe kuongea hadharani
 
Inaonekana wewe hujiamini. Kama kuropoka si unaropoka tu, hapa. Basi unaweza kuropoka popote pale almuradi usivunje sheria za nchi. Jiamini yakhe.Sio Raza tu hata wewe unaweza kuropoka kule Zenj- lakini usivunje sheria.
 
Ra kadhamini mkutano wa cuf katoa 250m na ccm z'bar wamekasirika sana, kwa hiyo raza kafikisha ujumbe
 
Ra kadhamini mkutano wa cuf katoa 250m na ccm z'bar wamekasirika sana, kwa hiyo raza kafikisha ujumbe
Ujumbe wa nini. Kama Raza anachangia CUF si na mimi naweza kuchangia Jahazi Asili. what is the problem?
 
Inaonekana wewe hujiamini. Kama kuropoka si unaropoka tu, hapa. Basi unaweza kuropoka popote pale almuradi usivunje sheria za nchi. Jiamini yakhe.Sio Raza tu hata wewe unaweza kuropoka kule Zenj- lakini usivunje sheria.

Yakhe si kujiamini au la .Hii dunia ya real politik.
Na usipoelewa hilo basi utajifunza the hard way.
 
Why all over sudden Raza kaanza kupiga kelele??

CCM wamemwekea kauzibe anakopata misamaha ya kodi nini??
 
Alichokisema Raza nina uhakika kuwa makada wa CCM kama Makamba,Mkuchika, Lowassa na Sofia Simba hawawezi kukiongea hadharani kwa vile wamekula ndoano ya mafisadi.
It does not need a rocket scientist to figure that out.
Sasa Mengi emegusia hilo na tunaona kash kash anayopata.
Ngugu yangu Pakacha hebu lisemee hilo wazi wazi kule Zenj tutakao kuunga mkono tuko wengi sana.
 
Back
Top Bottom