Ray c: Sijapata ukimwi, sijaokoka

Ray c: Sijapata ukimwi, sijaokoka

babumapunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
4,644
Reaction score
3,314
Na Musa Mateja

MWANADASHOSTI anayejipanga
kurejea kwenye gemu la Bongo
Fleva kwa kishindo, Rehema
Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya
moyoni akisema kuwa anamshukuru
Mungu kwa kupona madhara ya
madawa ya kulevya bila kupata
matatizo mengine ya kiafya huku
akifafanua suala la kuokoka.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa
katika kipindi chote cha kupigana
na madawa ya kulevya zaidi ya
miaka mitatu iliyopita, alipitia
mengi magumu lakini kikubwa ni
kwamba hivi karibuni alipima na
kujikuta yupo salama na hana
Ukimwi.

Kuhusu suala la kuokoka, Ray C
alisema ukweli ni kwamba
mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini
hivi karibuni alibatizwa na maji
mengi katika Kanisa la Sloam
lililopo Mbezi-Beach na kuungana
na mama yake anayesali kwenye
kanisa hilo
“Namshukuru Mungu nimepona,
sina tatizo la kiafya kama Ukimwi.
Kuhusu kuokoka, mimi sijaokoka.
Nilibatizwa na maji mengi.

Napenda mahubiri ya Sloam.
Nimeungana na mama yangu
anayesali kanisani hapo ndiyo
maana watu wanatafsiri kuwa
nimeokoka.“Watu wakisikia mtu
anasema ameokoka wanatafuta vitu
ili kukujaribu. Kweli mimi sijaokoka
lakini mahubiri yananiweka huru
na nakuwa na amani zaidi,”
alisema Ray C.

Source:Global Publishers
 
Habari nzuri ila hiyo source ndo kimeo..wala sintoamini...hayo
 
kumbe tusiwe tunaona wingi katika kusanyiko tukadhani wote ni wamoja!
 
ila akumbuke hakuna cha bule.akumbuke kauli ya jk kuwa ukisaidiwa lazima ukubali na ww kuliwa kidogo.
patam hapo coz mtoa kauli ndio aliye msaidia
 
Hivi kuokoka Ni nini? Je Ni dhambi kwa binadamu kuokoka?
 
Heri yake amekua mkweli,kwenda kanisani si kuokoka.
 
Yah kila la kheri Ray c nafikiri ni mapito tu ya dunia mateja wezio walitangulia na ni mipango ya mungu tu wewe u mzima.
 
Simple definition:

Kuokoka ni kuacha dhambi, kuacha kumtumikia shetani na kufuata amri za Mungu.
 
Ray C hongera kwa hatua uliyofikia na na nakuombea pamoja na wale marafiki zako ili MUNGU awafungue na huo mtego wa shetani kwa Kizazi hiki.
Kuokoka siyo jambo la ajabu bali ni kusudio lake MUNGU KWA KUMWAMINI YESU TU.
 
Rayc kweli teja kaacha madawa ya kulevya then kaokoka ..natamani karl max angemuona ..maana angethibisha ile kauli yake ya ....is the opium of the society..
Minanaona bado haja acha madawa ila amebadilisha madawa...
 
Njooo kwenye fani yako, wimbo wako wa penzi unanikoga sana moyo wangu
 
Daaah afadhali!!!!!!!!!! Maana huyu dada ulikua akipata alosto ya madawa unakuta hela hana kaishiwa bac anaenda pale jangwani bondeni kwa mapusher wajinga wajinga wanammpa madawa bure mwishoe anajioverdose akijisahau na kusinzia tu wanamla tigo mchana kweupe
 
Wapi huyu alikuwa anagawa kama pipi kwa mateja kariako alivyo kuwa arosto hana hela alikuwa wana fanya mambo ya wakubwa anapewa dozi kweli amepona
 
Huko Sloam umepotea dada.Huyo mchungaji anataka pesa tu,hana lolote analohubiri zaidi ya uongo na ubabaishaji.Kama umenusururika kupata ukimwi ni baati yako usikubali tena kumpa mtu sehemu isiyo ya asili katika mapenzi toa mbele tu.
 
Rayc kweli teja kaacha madawa ya kulevya then kaokoka ..natamani karl max angemuona ..maana angethibisha ile kauli yake ya ....is the opium of the society..
Minanaona bado haja acha madawa ila amebadilisha madawa...
Max anaongelea 'religion'. Don't take advantage of that. Kama ni religion, Ray C (pengine hata na wewe) alikua nayo hata kabla hajaanza kutumia hiyo 'opium'.


tragedy of the commons
 
Ubatizo wa maji mengi kabla ya kuokoka?
Mark 16:16a "whoever believes and is baptized will be saved"
Acts 10:47 "can anyone WITHHOLD water for baptizing these people, who have received the Holy Spirit just as we have?
Moja kati ya yafuatayo yaweza husika:
-kanisa halikuelewa anachokiongea/alidanganya/badilisha
-kanisa hilo sio kama mengine yenye imani hiyo

tragedy of the commons
 
Wapi huyu alikuwa anagawa kama pipi kwa mateja kariako alivyo kuwa arosto hana hela alikuwa wana fanya mambo ya wakubwa anapewa dozi kweli amepona
ukimwi ni ugonjwa uliojaa vitendawili,vipimo pia vimejaa vitendawili...magic johnson nilisikia ana ukimwi nikiwa kinda leo bado yupo ngangari na akipima vipimo vinasoma negative.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom