Ray aamua...

naomba nimjibu Ray niki quote kwako. sina hakika kama kuna watu walioishi na mama wa kambo wakaona machungu yake. naongea through experience. sio mama wa kambo wote of course. wako wenye mioyo ya dhahabu na wenye mioyo ya kishetani. mara nyingi baba humthamini mke mdogo pamoja na watoto wa mke mdogo hata asiowazaa yeye, mke mkubwa na watoto wake wote wanakua hawana maana mbele yake. hapo ndipo watoto wa mke mkubwa mnapokosa haki mbadala kutoka kwa baba yenu mzazi, shinikizo kubwa likitoka kwa bi mdogo ambaye hajawazaa. Kanumba hana laana ya baba kwa sababu baba alichojua ni kutoa mkojo, akazaliwa na biashara ikaishia hapo. alipopata jina, sasa ndio baba anajitokeza na kujifanya ni mwanae. chukulia Kanumba angekua chokoraa pale UWT/Morogoro Road, baba angemtambua? sana sana angetukanwa mama kua kamshindwa mtoto. acheni kuropoka kwa mambo ya familia za watu ambayo hamjui undani wake. RIP big daddy...

Hivi mwanaume kumtungisha mimba mwanamke akazaa ndio kunampa sifa ya 'uMungu wa dunia, mHeshimiwa kwa namna yoyote, na hasiyeKosea kamwe'!? Kweli jigy-jigy tu inakupa hiyo heshima yoote?!

To me it takes more than just to impregnate a woman to be a father! uBaba hauishii kwenye kumjaza mwanamke mimba, bali unaanzia hapo kwenye kumjaza mwanamke mimba, sasa kama hukutimiza majukumu yako yaliyotakiwa kufuatia kumtia mwanamke mimba..mtoto akiwa maarufu na mkwanja usirudi eti kujitia wewe ni baba! Nyambaff...

Mimi nalea mtoto wa dada yangu...binti smart (kichwa) kweli kweli kushinda hata mwanangu wa kumzaa, lakini huyu binti alitelekezwa na baba yake tangu akiwa na miaka mi3, na dada akiwa hana uwezo wowote wa kumlea na kumsomesha huyu mtoto. Sasa mtoto now yuko chuo kikuu doing very great baba yake anakuja eti anataka mwanae....nyambaff! Wakati tunambembeleza kumsupport mwanane anatoa matusi alifikiri mtoto atakuwa looser?!

Kama unataka sifa ya baba kuwa mungu wa dunia na kuheshimiwa play your part kama baba!
 
huyu Ray alikua anafuta mahali pa kuyeyusha donge lake naKanumba. Mungu ni mmoja tu. huyo baba suruali u-mungu kautoa wapi?

Na Mwandishi Wetu
HABARI KAMILI
Ray alisema, hata kama baba yake angekuwa amefanya kosa kubwa kiasi gani, kumuanika kwenye vyombo vya habari ni kumkosea adabu.
"Kiukweli pale Kanumba alikosea sana, huwezi kumsema mzazi wako. Baba ni Mungu wa duniani. Anatakiwa kuheshimiwa kwa namna yoyote," alisema na kuongeza:


 
“Kiukweli pale Kanumba alikosea sana, huwezi kumsema mzazi wako. Baba ni Mungu wa duniani. Anatakiwa kuheshimiwa kwa namna yoyote,” alisema na kuongeza:

sasa hii ni kujitafutia laana.............mwelezeni ray hakuna miungu wengi yuko mmoja tu naye ni Yesu Kristu na hakuna Mungu mwingine............mzazi ni kiumbe............tu hawezi kuwa Muumba hata siku moja.......
 
Jamani RAY yupo right ingawa amekosea kwenye kusema Baba ni mungu wa duniani.

Ila kikubwa hata kama baba au mama walikutelekeza hapo mwanzo lakini bado ni wazazi wako tu. Ndio maana walisema kwenye bible waheshimu faza na maza ili upate maisha marefu mjengoni. Hawakuelezea status watakayonayo wazazi wako at that time ili uwape hiyo heshima.

Take care.
 
Back
Top Bottom