Ray aamua... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ray aamua...

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Dr. Chapa Kiuno, Feb 29, 2012.

 1. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi Wetu

  STAA anayemiliki mkwanja mrefu katika tasnia ya filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray', amemvaa ngwiji mwenzake Steven Charles Kanumba na kumchana kwa kitendo cha kumlipua baba yake mzazi, mzee Charles Kusekwa, katika vyombo vya habari, Risasi Jumamosi lina mkanda mzima.

  Akizungumza na gazeti hili, Ray ambaye inadaiwa ana bifu baridi na Kanumba, alisema kitendo alichokifanya mshkaji wake si cha kiungwana kwa kuwa aliyekuwa anamzungumzia ni baba yake mzazi.

  HABARI KAMILI
  Ray alisema, hata kama baba yake angekuwa amefanya kosa kubwa kiasi gani, kumuanika kwenye vyombo vya habari ni kumkosea adabu.

  "Kiukweli pale Kanumba alikosea sana, huwezi kumsema mzazi wako. Baba ni Mungu wa duniani. Anatakiwa kuheshimiwa kwa namna yoyote," alisema na kuongeza:

  "Kwanza mzazi huwa hakosei...tunatumia uungwana kusema, anasahau! Hata kama alimkosea, tutasema alijisahau...halafu unapomsema mzazi wako kwenye vyombo vya habari unatarajia nini? Adharaulike au? Hakufanya sawa hata kidogo."

  NI LAANA

  Akiendelea kutambaa na mistari, Ray alisema kitendo alichokifanya Kanumba ni sawa na kutafuta laana.

  "Hata kama hatamlaani, lakini moja kwa moja ni laana. Huwezi kumkosesha amani mzazi wako kiasi kile. Nina uhakika Kanumba hakuomba ushauri kabla ya kwenda kwenye runinga.

  "Alikurupuka. Kama angezungumza na sisi wasanii wenzake, naamini hakuna ambaye angemkubalia. Tungemshauri vizuri tu. Hili ni kosa kubwa. Ni sawa na kumvua nguo mzazi wako," alisema.

  Akaongeza: "Mbaya zaidi, baba yake amejibu tuhuma zake kwenye gazeti, na yeye tena akamjibu. Inaonesha ni kwa namna gani anapenda mashindano na mzazi wake. Si kitu kizuri hata kidogo. Hapo Kanumba alichemka, lazima aelewe huo ukweli.

  "Unajua kuna mambo mengine hayapaswi kujulikana na watu. Yeye kama msanii mkubwa, mwenye heshima, leo hii anaanika maisha yake ya utotoni? Eti baba alimtesa? Ili iweje? Amepata nini kwa kusema hayo kama siyo kumdhalilisha tu mzazi wake? Haikuwa sawa.

  "Haya mambo wangeyajadili kifamilia ingekuwa na maana zaidi kuliko kuyaanika hadharani."


  AMTAKA AOMBE RADHI
  Ray alisema, Kanumba akitaka aendelee kupaa katika anga la filamu, anatakiwa kumuomba lazi baba yake.
  "Kitu pekee kilichobaki ni kumuomba baba yake msamaha. Amemkosea sana, amuombe amsamehe ili asibaki na kinyongo. Hiyo ndiyo njia pekee ya kumsafisha," alisema na kuongeza:
  "Nina imani atamsamehe na watafungua ukurasa mpya. Huu ni ushauri wangu. Ana uhuru wa kuufuata au kuuacha. Mzazi siku zote ana huruma na mwanaye, bila shaka atamsamehe."


  NI MWENDELEZO WA BIFU?

  Alipoulizwa kuwa sababu ya kusema yote kwa Kanumba ni kwa kuwa ana bifu naye, Ray aliruka kimanga, akaeleza kuwa, amefanya hivyo kama msanii mwenzake na ni kwa nia njema.

  "Sizungumzii mambo ya bifu hapa, naongelea usahihi wa alichokifanya. Naamini hata jamii haiwezi kuona eti kumshauri mtu ni bifu. Ni mawazo yangu, kama nilivyosema awali," alisema.

  RAY AAMUA... - Global Publishers
   
 2. ney kush

  ney kush JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 1,195
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  Eeeeeh!!
   
 3. aspen

  aspen JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ray umeonesha una busara kanumba bado umri mdogo atakuwa tu hivi vijisenti vya mpa ngebe .
   
 4. Z

  Zero_brain Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ray na huyo mwenzake wote vilaza tu.
   
 5. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Hivi mwanaume kumtungisha mimba mwanamke akazaa ndio kunampa sifa ya 'uMungu wa dunia, mHeshimiwa kwa namna yoyote, na hasiyeKosea kamwe'!? Kweli jigy-jigy tu inakupa hiyo heshima yoote?!

  To me it takes more than just to impregnate a woman to be a father! uBaba hauishii kwenye kumjaza mwanamke mimba, bali unaanzia hapo kwenye kumjaza mwanamke mimba, sasa kama hukutimiza majukumu yako yaliyotakiwa kufuatia kumtia mwanamke mimba..mtoto akiwa maarufu na mkwanja usirudi eti kujitia wewe ni baba! Nyambaff...

  Mimi nalea mtoto wa dada yangu...binti smart (kichwa) kweli kweli kushinda hata mwanangu wa kumzaa, lakini huyu binti alitelekezwa na baba yake tangu akiwa na miaka mi3, na dada akiwa hana uwezo wowote wa kumlea na kumsomesha huyu mtoto. Sasa mtoto now yuko chuo kikuu doing very great baba yake anakuja eti anataka mwanae....nyambaff! Wakati tunambembeleza kumsupport mwanane anatoa matusi alifikiri mtoto atakuwa looser?!

  Kama unataka sifa ya baba kuwa mungu wa dunia na kuheshimiwa play your part kama baba!
   
 6. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  well said

   
 8. D

  Dotowangu JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hawa wote vijisent na kupenda kuonekana kwa watu kunawasumbua..hivi rafiki yako wa kweli huwezi kumshauri mkiwa wawili mpaka wawepo waandishi wa habari?
   
 9. H

  Handsome Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Riwa ubarikiwe mbinguni na duniani,
   
 10. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Riwa hapo umesema kweli. Baba au mama aliyenilea kwa upendo nitamthamini zaidi kuliko biological parents ambao hawana habari na mimi
   
 11. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ati Mung wa duniani!!!??? hi kweli kali. Mungu anamjua anamsikia???
  baba kama hajatimiza responsibility za ni sawa tu mama anayezaa mtoto na kumtupa chooni
  kama hakumtaka akiwa mdogo angekufa kwa kukosa matunzo angeongea nini???
  apotelee mbali
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli inauma sana aisee. Ngoja nami niutafute umaarufu ili baba yangu ajitokeze!
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  hayajawakuta, yakiwakuta wala hamtasema kitu.
   
 14. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mzungu alisemaa "Any man can be a father but it needs someone special to be dad", kabla hatujamlaumu Kanumba hebu tujiulize huyu anayeclaim kuwa baba is he a father (biologicaly) or a dad (responsibly)
  Kama limtu linakataa mtoto halafu akifanikiwa kimaisha linamsumbua na kumtisha na laana, laana my foot. Laana yako haitapokelewa mbinguni wala duniani.
  Nina scenario kama yako mkuu Riwa, nalea huyu mtoto asiye na hatia na yuko bright mno, namsubiri huyo bingwa wa kugawa mbegu aje.
   
 15. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Upo sahihi Kongosho, kama baba hakujua umuhimu wa kuwa baba basi hana maana.

  Ray alitaka tu kujionyesha yupo sahihi mbele ya jamii wakati jamii ipo fair katika judgement.
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  kweli wanaume tuna tabia ya kudai mtoto baada ya kuona mtoto ana mafanikio ni mbaya sana!
   
 17. +255

  +255 JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Na HUYU naye alikuwa na makosa?!
   
 18. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  mmmh..
   
 19. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  the way the cookie crumbles...

  Ngoja nipite kwanza.
   
 20. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #20
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya MALUMBANO YAMEKWISHA TIME HAVE TOLD US baba anapashwa kuheshimiwa hata afanye kosa lipi! mungu kaweka ktk amri zake kumi WAHESHIMU BABA NA MAMA YAKO UPATE MIAKA MINGI NA HERI DUNIANI! Asiye mheshimu Baba yake hatopata miaka mingi duniani!(atakufa mapema!) MUNGU ndiyo kasema hivyo si mimi!
   
Loading...