Ratiba ya Rais Magufuli ziarani Mbeya na hofu ya usalama yafanya wananchi kukaguliwa

''Atakwenda Kyela kulikojengwa barabara'' Sijaelewa hii ratiba ina maana gani
 
Kubwa la majizi ziarani Mbeya.

RC ALBERT CHALAMILA ATOA RATIBA RASMI ZIARA YA RAIS MAGUFULI MBEYA.

Leo majira ya saa 8 mchana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amekutana na waandishi wa habari ofisini kwake na kutoa ratiba rasmi ya ziara ya Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli katika Mkoa huu.

RC Chalamila amesema Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli atafika Mkoani Mbeya jioni ya tarehe 25/04/2019 kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo Wilaya ya Mbeya jimbo la Mbeya Vijijini.

Tarehe 26/04/2019 pamoja na mambo mengine atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya CCM maarufu kama Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya.

Tarehe 27/04/2019 ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Rungwe na Kyela ambapo atasalimiana na wananchi katika eneo la Kiwira, Tukuyu na kufungua kiwanda cha maparachichi, mabweni nk katika chuo cha Ualimu Mpuguso Wilayani Rungwe kisha kuelekea Wilayani Kyela ambako kumejengwa Barabara kisha atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya John Mwakangale Wilayani humo.

Tarehe 28/04/2019 atakuwa katika viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya katika tukio la uapisho wa Askofu Nyaisonga wa Kanisa Katoliki.

RC Chalamila ametoa wito kwa watakaohudhuria sherehe hizo kuingia uwanjani kabla ya saa 4 asubuhi na kwamba kila atakayeingia uwanjani humo atakaguliwa kwa ajili ya usalama.

29/04/2019 ataelekea Wilayani Chunya.

30/04/2019 atafanya ziara Jijini Mbeya na atazungumza na wanazuoni wa vyuo na vyuo vikuu katika eneo la Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia (MUST).

Tarehe 01/05/2019 atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wafanyakazi (MEI MOSI) zitakazofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

02/05/2019 atamalizia ziara yake katika Wilaya ya Mbeya (Mbeya Vijijini) kwa kutembelea Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement.

RC Chalamila amewakaribisha wananchi wote kumlaki Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli na amesema mabango yenye tija yasiyo ya uchochezi yanaruhusiwa.
 
Wananchi wanatakiwa kuingia uwanjani saa 4 halafu rais anaingia saa 10, chakula watapewa? halafu huyu ni kipenzi cha wanyonge sasa hofu ya nini mpaka kukaguana au mbeya siyo kwa wanyonge?
Ww kweli mjanja wa kijiji. Kama Gwajima tu analindwa vp Rais
 
Hakuna ukaguzi unaoweza kuzuia chochote tarehe ikifika. Refer Anwar Sadat assassination in 1981, members of the security apparatus fled to cheat death.
 
Bila shaka ukaguzi huo utakuwa wa mabango, watataka ya kumfurahisha Mkulu tu.
 
Hivi wewe unajitambua.

Huyo mwenyekiti wenu wa kudumu wa chama tu analindwa na mibaunsa itakuwa Rais, tena mwenye uthubutu. Msijekutupotezea Rais wetu kama mlivyompoteza PM Sokoine
Nilitoa ushauri angalau Praise Team iwe na watu angalau wenye elimu kuanzia kidato cha nne! Mnavyojazana darasa la saba D inakuwa ni tabu.
Hata hujui mfumo wa vyama vingi ulianza lini. Naalabuk
 
hivi tarehe 26/04 si ndo sikukuu ya muungano?? au mwaka huu hakuna maadhimisho?? coz naona ratiba ya 26/04 magu atakuwa mbeya au sikukuu ndo inafanyikia huko?? naomba ifafanuzi plz
 
Wapinzani wa Mbeya punguzeni ushamba, kukaguliwa kwenye mikutano ya Magufuli hakujaanza leo wala jana, labda nyinyi mtaona ni kitu cha ajabu sababu ndio mara ya kwanza JPM anazuru Mbeya kama Rais ila mikoa mingine aliyozuru kukaguliwa ni jambo la kawaida sana.

Tena hakikisheni nguo mnazoingilia uwanjani hazina metallic objects ili kukwepa usumbufu, shika mkanda wako mkononi na electronic devices ulizonazo.
 
Kama walikua hawakagui watu ni makosa makubwa sana...

Kawaida atakapopita rais au kuja rais lazima ukaguzi upite...

Cc: mahondaw
 
Wananchi wanatakiwa kuingia uwanjani saa 4 halafu rais anaingia saa 10, chakula watapewa? halafu huyu ni kipenzi cha wanyonge sasa hofu ya nini mpaka kukaguana au mbeya siyo kwa wanyonge?
Mkuu rudia kusoma vizuri siku ya kwanza atatua uwanjani na kuelekea ikulu ndogo hatahutubia mahali popote.
Siku inayofuatia ndiyo atahutubia na itabidi wananchi wafike kabla ya saa 4 asubuhi.
 
Wananchi wanatakiwa kuingia uwanjani saa 4 halafu rais anaingia saa 10, chakula watapewa? halafu huyu ni kipenzi cha wanyonge sasa hofu ya nini mpaka kukaguana au mbeya siyo kwa wanyonge?
Soma historia ya Alof Palme utaelewa hata ukiwa kipenzi risk ipo
 
RC ALBERT CHALAMILA ATOA RATIBA RASMI ZIARA YA RAIS MAGUFULI MBEYA.

Leo majira ya saa 8 mchana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amekutana na waandishi wa habari ofisini kwake na kutoa ratiba rasmi ya ziara ya Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli katika Mkoa huu.

RC Chalamila amesema Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli atafika Mkoani Mbeya jioni ya tarehe 25/04/2019 kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo Wilaya ya Mbeya jimbo la Mbeya Vijijini.

Tarehe 26/04/2019 pamoja na mambo mengine atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya CCM maarufu kama Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya.

Tarehe 27/04/2019 ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Rungwe na Kyela ambapo atasalimiana na wananchi katika eneo la Kiwira, Tukuyu na kufungua kiwanda cha maparachichi, mabweni nk katika chuo cha Ualimu Mpuguso Wilayani Rungwe kisha kuelekea Wilayani Kyela ambako kumejengwa Barabara kisha atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya John Mwakangale Wilayani humo.

Tarehe 28/04/2019 atakuwa katika viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya katika tukio la uapisho wa Askofu Nyaisonga wa Kanisa Katoliki.

RC Chalamila ametoa wito kwa watakaohudhuria sherehe hizo kuingia uwanjani kabla ya saa 4 asubuhi na kwamba kila atakayeingia uwanjani humo atakaguliwa kwa ajili ya usalama.

29/04/2019 ataelekea Wilayani Chunya.

30/04/2019 atafanya ziara Jijini Mbeya na atazungumza na wanazuoni wa vyuo na vyuo vikuu katika eneo la Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia (MUST).

Tarehe 01/05/2019 atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wafanyakazi (MEI MOSI) zitakazofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

02/05/2019 atamalizia ziara yake katika Wilaya ya Mbeya (Mbeya Vijijini) kwa kutembelea Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement.

RC Chalamila amewakaribisha wananchi wote kumlaki Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli na amesema mabango yenye tija yasiyo ya uchochezi yanaruhusiwa.
MHASHAM BABA ASKOFU NYAISONGA (HEADMASTER ) PANDAHILL. wa zamani

NI KWAMBA ANASIMIKWA RASMI KUWA KUWA ASKOFU WA JIMBO LA MBEYA NA SIO "uapisho "

Neno hilo limetumika vibaya .
NAAM Nimependa NADHANI WATAONANA PIA NA RAFIKI YAKE MARK MWANDOSYA...
 
Ni kweli ukaguzi Upo Ni wa Kawaida. Ni Utaratibu tu. Nimeshiriki Songea. Lazima upite kwenye screening. WALE vijana wapo smart sana. Mabango ya hovyo na hoja ZA kitoto huchanwa. Ukileta zako zepe unachezea ZA chembe Utaenda umia mbele mbele ua safari. KIFUPI bango nyingi ni Uchochezi tu hayana tija.
 
uoga tu, sasa kuchana mabango ili iweje
 
Back
Top Bottom