Ratiba ya Rais Magufuli ziarani Mbeya na hofu ya usalama yafanya wananchi kukaguliwa

Kuna tetesi kuwa wapo walioandaliwa kujiuzulu na kuhamia fisiemu, na ipo taarifa kuwa ataongeza mishahara maradufu!
 
Kama wewe ni mtu mzuri, hofu ya nini kuhusu kukaguliwa? Mbona alipokuja Mwanza kufungua kiwanda cha madawa cha Prince tulikaguliwa na hakukuwa na noma yoyote? A President is not a normal person as your simple minds think!
Mkuu saa nyingine watanzania tuna mihemko , Kama eneo la shopping unafanyiwa screening sembuse kwa Mh Rais.
 
Kuna tetesi kuwa wapo walioandaliwa kujiuzulu na kuhamia fisiemu, na ipo taarifa kuwa ataongeza mishahara maradufu!
Haaaahh
Ni mwendo wa kusifuuuu tu.

Note: Jana Rais akiwa Malawi, ulinzi wake (kile kikosi cha PSU wenye mabaka mabaka), ulikuwa sio wa mchezo mchezo..
 
Tayari tu ratiba imeonesha vitisho! hapo kwenye mabango yenye tija na yasiyo ya kichochezi watumishi wa umma mjiandae kisakolojia kutokumchochea Mtukufu mwenye heri kutizama stahiki zenu! Maana tredi yunions zote zimekua rubber stamp ya serikali huku zikitegemea huruma. Utasikia siku hiyo katika hutuba watakavyokua wanampamba na kumuomba na hapo ndipo anapovimba kichwa na kusema "mwaka 2020 ni wenu watumishi, chapeni kazi kwa nguvu, nchi inasonga mbere, wakati wenu ni sasa mtembee kifua mbere, mafisadi yameisha!!!!!! kijani kwakwakwakwakwaaaaa... niwaombe tu watumishi muwe wavumirivu mwakani sio mbari na mambo yatakua mazuri!!! nawapenda sana (kama alivyowadanganya walimu pale Dodoma)
TuelimishaneMoshi
 
RC ALBERT CHALAMILA ATOA RATIBA RASMI ZIARA YA RAIS MAGUFULI MBEYA.

Leo majira ya saa 8 mchana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amekutana na waandishi wa habari ofisini kwake na kutoa ratiba rasmi ya ziara ya Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli katika Mkoa huu.

RC Chalamila amesema Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli atafika Mkoani Mbeya jioni ya tarehe 25/04/2019 kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo Wilaya ya Mbeya jimbo la Mbeya Vijijini.

Tarehe 26/04/2019 pamoja na mambo mengine atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya CCM maarufu kama Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya.

Tarehe 27/04/2019 ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Rungwe na Kyela ambapo atasalimiana na wananchi katika eneo la Kiwira, Tukuyu na kufungua kiwanda cha maparachichi, mabweni nk katika chuo cha Ualimu Mpuguso Wilayani Rungwe kisha kuelekea Wilayani Kyela ambako kumejengwa Barabara kisha atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya John Mwakangale Wilayani humo.

Tarehe 28/04/2019 atakuwa katika viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya katika tukio la uapisho wa Askofu Nyaisonga wa Kanisa Katoliki.

RC Chalamila ametoa wito kwa watakaohudhuria sherehe hizo kuingia uwanjani kabla ya saa 4 asubuhi na kwamba kila atakayeingia uwanjani humo atakaguliwa kwa ajili ya usalama.

29/04/2019 ataelekea Wilayani Chunya.

30/04/2019 atafanya ziara Jijini Mbeya na atazungumza na wanazuoni wa vyuo na vyuo vikuu katika eneo la Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia (MUST).

Tarehe 01/05/2019 atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wafanyakazi (MEI MOSI) zitakazofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

02/05/2019 atamalizia ziara yake katika Wilaya ya Mbeya (Mbeya Vijijini) kwa kutembelea Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement.

RC Chalamila amewakaribisha wananchi wote kumlaki Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli na amesema mabango yenye tija yasiyo ya uchochezi yanaruhusiwa.
kajuaje kama kutakuwa na mabango?
kwa hio mabango ya kusifia ndege ndio yanaruhusiwa tu
 
Ila hotuba yake ni ile ile moja
1. Ndege
2.tupo kwenye right tlaki
3.ukibeba mzigo chini ya tani moja usikubali kulipa kodi.. kama una tani tatu beba moja moja mara tatu hadi ziishe.
4. SGR
5. Sisi ni matajiri kweli kweli
6. nchi hii imeliwa sana.
7.stigla goji
8. nimetoka malawi na kule nilimwaga ngeli mwanzo mwisho.
 
Wananchi wanatakiwa kuingia uwanjani saa 4 halafu rais anaingia saa 10, chakula watapewa? halafu huyu ni kipenzi cha wanyonge sasa hofu ya nini mpaka kukaguana au mbeya siyo kwa wanyonge?
Ugumu wanauleta wenyewe na complications zao but masikini ya Mungu wananchi hata hawana neno,Utukufu uko kwetu wananchi ndio maana hta wenye silaha bado wanatuogopa
 
Hivi kwa nini asiwe free kama uhuru yaani ukimwona uhuru anapiga stori na washkaji jukwaani kama sio raisi vile
 
Kuna tetesi kuwa wapo walioandaliwa kujiuzulu na kuhamia fisiemu, na ipo taarifa kuwa ataongeza mishahara maradufu!
kwahiyo tuseme anawachora kina mhagama na mkuchika ili baadae waonekane wasaliti kama kwenye kikotoo?
 
RC ALBERT CHALAMILA ATOA RATIBA RASMI ZIARA YA RAIS MAGUFULI MBEYA.

Leo majira ya saa 8 mchana, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amekutana na waandishi wa habari ofisini kwake na kutoa ratiba rasmi ya ziara ya Mheshimiwa Rais Dr. John Pombe Magufuli katika Mkoa huu.

RC Chalamila amesema Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli atafika Mkoani Mbeya jioni ya tarehe 25/04/2019 kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo Wilaya ya Mbeya jimbo la Mbeya Vijijini.

Tarehe 26/04/2019 pamoja na mambo mengine atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya CCM maarufu kama Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya.

Tarehe 27/04/2019 ataendelea na ziara yake katika Wilaya ya Rungwe na Kyela ambapo atasalimiana na wananchi katika eneo la Kiwira, Tukuyu na kufungua kiwanda cha maparachichi, mabweni nk katika chuo cha Ualimu Mpuguso Wilayani Rungwe kisha kuelekea Wilayani Kyela ambako kumejengwa Barabara kisha atafanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya John Mwakangale Wilayani humo.

Tarehe 28/04/2019 atakuwa katika viwanja vya Sokoine Jijini Mbeya katika tukio la uapisho wa Askofu Nyaisonga wa Kanisa Katoliki.

RC Chalamila ametoa wito kwa watakaohudhuria sherehe hizo kuingia uwanjani kabla ya saa 4 asubuhi na kwamba kila atakayeingia uwanjani humo atakaguliwa kwa ajili ya usalama.

29/04/2019 ataelekea Wilayani Chunya.

30/04/2019 atafanya ziara Jijini Mbeya na atazungumza na wanazuoni wa vyuo na vyuo vikuu katika eneo la Chuo Kikuu cha sayansi na Teknolojia (MUST).

Tarehe 01/05/2019 atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wafanyakazi (MEI MOSI) zitakazofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

02/05/2019 atamalizia ziara yake katika Wilaya ya Mbeya (Mbeya Vijijini) kwa kutembelea Kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement.

RC Chalamila amewakaribisha wananchi wote kumlaki Mheshimiwa Rais Dr. Magufuli na amesema mabango yenye tija yasiyo ya uchochezi yanaruhusiwa.
Vip Raisi wa Mbeya atakwepo kwenye mapokezi
 
Wananchi wanatakiwa kuingia uwanjani saa 4 halafu rais anaingia saa 10, chakula watapewa? halafu huyu ni kipenzi cha wanyonge sasa hofu ya nini mpaka kukaguana au mbeya siyo kwa wanyonge?
Huo sasa ni uchochezi,kwani amekwambia ukaguziwao ni kwa sababu rais anakuja au ndio utaratibu wa viwanja vya ndege.
 
Sio nchi za wenzetu, nenda Club de Alberto moshi hapo ukaguzi ni muhimu, vipi ukiingia na kisu au silaha yoyote kumdhuru mtu
Tunaishi zama tofauti; kukaguliwa ni mambo ambayo inabidi watu wayazoee tu.. kwenye nchi za wenzetu hata watu wakiingia kwenye klabu ya disko tu wanakaguliwa...
 
Sio nchi za wenzetu, nenda Club de Alberto moshi hapo ukaguzi ni muhimu, vipi ukiingia na kisu au silaha yoyote kumdhuru mtu
Unajua watu wengine wameshazoea kupingapinga tu kila kitu,anaweza akajipinga hata yeye mwenyewe.Suala la ukaguzi wanalichukulia kama suala la kutokuwa na imani,kumbe ni usama tu unafanywa pale.
 
Hivi wewe unajitambua.

Huyo mwenyekiti wenu wa kudumu wa chama tu analindwa na mibaunsa itakuwa Rais, tena mwenye uthubutu. Msijekutupotezea Rais wetu kama mlivyompoteza PM Sokoine
kumbe kipindi cha sokoine kulikua na chedema
 
Back
Top Bottom