Ratiba ya maziko ya mama yetumpendwa..mama pdidy kesho saa nane

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,150
Ndugu zanguni
atuna budi kuishi kama wasio na matumaini na kuamini mungu ndie alimleta na ndie alieamua kumchukua ni vigumu kuamini na sikuwahi kuhisi hili ila furaha ilioje ni kwamba mama yangu mpenda amekufa katika bwana saa tano usiku, saa mbili akaomba wachungaji akiwa na nguvu za kuongea..walipokuja akaomba mchungaji awabariki manesi wanaomtibu then akaongoza sala ya toba alipomaliza nikiwa nyuma yake akasema yesu unipokee akaomba nimpumzishe alale..nikiwa nimeendelea kumshika sikujua kumbe ameshakufa nikiwa namweka sawa niende nyumban nikagundua utukufu wa mungu umeshatimizwa

ahsanten kwa maombi yenu kibinadamu ni ngumu lakini mungu ndie mweza yote

msiba uko kimara bucha ukifika upande wa kulia ..tunaaaga kesho saa nane mchana tunaenda kuzika makaburi ya mbweni...for more info 0713 45 87 22

bwana akubariki wewe ulietumia muda wako kutuombea familia ni vigumu kushukuru lakini mungu akujalie pale palipopungua
 
R.I.P Mama, na Mungu akujaze nguvu na uvumilivu zaidi katika kipindi hichi kigumu cha msiba.
 
Pole Sana. Tupo [pamoja katika kumuombea mama yetu mpendwa.

RIP mama.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Pole sana Kamanda, Kazi ya Mungu haina makosa. Mama ametangulia nasi tutamfuata. Jina la bwana lihimidiwe.
 
Mungu amlaze mahali pema mama yetu mpendwa.

Na Mungu huyohuyo aendelee kukupa moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu sana kwako.

Pole sana mkuu Pdidy kwa msiba huu mkubwa uliokupata.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa..... JIna lake lihimidiwe.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom