Makoye Matale
JF-Expert Member
- May 2, 2011
- 6,491
- 2,104
usafiri upo mwingi wa kuwapeleka
Tumewaachia ninyi ili uwarudishe.
usafiri upo mwingi wa kuwapeleka
Hiyo bahati ipo upande mmoja tu siku zote, kwa nini Yanga wasibahatishe walau 3-0?
ukiwa shabiki ni mzigo sana kiasi unasahau kabisa hali halisi...
Mashindano ya mapinduzi ni mashindano yenye dhima ya kuadhimisha mapinduzi ya zanzibar na wala hayapo katika kalenda yoyote ya michezo ya tff...
Timu zinashiriki kwa kualikwa (mtu yoyote mwenye akili timamu anajua kabisa kuwa mwaliko unaweza kukubaliwa au kukataliwa)...
Kuna timu zinaongozwa na ratiba kutoka benchi la ufundi kwa kuangalia mambo kadhaa ya kiufundi kabla ya kushiriki mashindano au mechi zisizo na ulazima...
Yanga kujitoa mashindano binafsi sioni kama ni nongwa maana mashindano hayo hayana tija kwa timu kwa wakati huu...
Tumewaachia ninyi ili uwarudishe.
Sababu unazotoa watu8 sio sababu za klabu ni za kishabiki tu,
Jamani mimi huwa naangalia vitu vingi nyuma ya pazia. Sababu kubwa ya Yanga ni kutokuwa na uhakika wa kuwatumia wachezaji kadhaa ambao inawategemea. Ngasa, Msuva na Canavaro wanaumwa na wangeikosa michuano hiyo. Okwi na Kiiza bado wapo Uganda na wamezima simu zao. Ukiangalia kikosi walau wanachokitegemea kilichocheza na Simba na kufungwa 3-1, wakaona hao waliobaki kambini ndio hawawezi kabisa. Walianza na sababu ya kusema hawajapatiwa mwaliko rasmi, akatokea ofisa wa ZFA na kuthibitisha kwa kuonyesha dispatch waliyosaini Yanga kupokea mwaliko. Yanga wakaja na mpya kwamba wanataka wawekewe wazi kuwa watakula nini na watalala vipi. Kabla hawajajibiwa kuwa watakuwa wanakula nini, ndio wakaja na hiyo mpya nyingine ya kusema hawana benchi la ufundi. Brandts bado yupo ndani ya notisi ya siku 30, Minziro bado yupo, Mkwasa ameshakubali kujiunga nao, hivi kombe la mapinduzi linahitaji Boby Williamson? Ukweli ni kwamba wachezaji wao wa kutegemewa hawapo, waliobaki kambini wana hofu ukizingatia wametoka kufungwa na Simba. Yanga inabidi ianze kuwaamini wachezaji wote waliosajiliwa, kuna kipindi (mwaka jana) kikosi cha kwanza cha Simba kilienda kuweka kambi Uarabuni na huko kwenye kombe la Mapinduzi wakaenda akina Singano na Mkude na wakafika Semi Final, leo hao vijana ndio wanaoitisha Yanga!
Sababu kubwa ya uamuzi huo 'Bado hawajapata benchi la uhakika la ufundi'.
Cha kujiuliza ni nini kisa cha kumtimua Brandts!? Je yawezekana baada ya kuangalia timu pinzani uoga umeingia?kwamba kipigo kingine kutoka kwa mnyama iwapo watakutana kitaleta mtafaruku jangwani? Nini hasa?
Manji asipoondolewa yanga itakufa..
Rage hajambo? Upepo wa kumtimua umeishia wapi?
Anayetakiwa kudhibiti nidhamu ya wachezaji sio uongozi wa timu..Ni Kocha na benchi lake la ufundi na kwa hili Brandts na benchi lake la ufundi wamefail ndio maana kila mtu anamshangaa Brandts kwa kulialia kuhusu nidhamu ya wachezaji ilhali yeye ndio anapaswa kuidhibiti..Ila yanga mmetuaibisha kweli penye miti mingi hapana wajenzi, mpaka kocha analalamika wachezaji wanajiona mastaa halafu nothng wanafanya!! Ustaa unakuja baada ya kuwajibika!! Tubadilike, SIMBA HAWA HAWA WATAENDELEA KUTUPA KICHAPO CHA MBWA MWIZI MPAKA TUKOME!!!
Ila yanga mmetuaibisha kweli penye miti mingi hapana wajenzi, mpaka kocha analalamika wachezaji wanajiona mastaa halafu nothng wanafanya!! Ustaa unakuja baada ya kuwajibika!! Tubadilike, SIMBA HAWA HAWA WATAENDELEA KUTUPA KICHAPO CHA MBWA MWIZI MPAKA TUKOME!!!
uzuri wa nyani sisi tunapenda ndizi za njano sana.Siyo ninyi mliotimua makocha wazawa hivi karibuni kwa matokeo mabaya, hivi mna pointi ngapi kwenye ligi? Nyani kumbe haoni kundule eeh? Kumbe, huona la mwenzie!