GE2025 Rasmi Paul Makonda ni mrithi wa Mrisho Gambo Arusha mjini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Maswa Yetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2023
Posts
1,399
Reaction score
2,617
Paul Makonda ameshinda kwa kupata kura zaidi ya elfu 9 ambayo ni sawa na 97% na kuwaacha mbali wenzake kwenye kura za maoni ya ccm kwenye jimbo la Arusha mjini.

Wasiompenda msukuma mwana kolomije Paul Makonda sasa watakuwa nae sana hapo mjni
===============
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, ameibuka mshindi kwa kishindo katika kura za maoni za kuwania nafasi ya ubunge kupitia CCM, baada ya kupata kura 9,056, sawa na asilimia 97.65 ya kura zote halali zilizopigwa.

Taarifa rasmi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi wa ndani wa CCM katika jimbo husika zimeeleza kuwa mchakato huo ulifanyika kwa amani, uwazi na kufuata taratibu zote za chama. Makonda ameonesha nguvu kubwa ya kisiasa na kukubalika kwa kiasi kikubwa na wanachama wa CCM.

Katika kura hizo, kulikuwa na wapiga kura zaidi ya 9,200 waliojitokeza, na ni wachache tu waliopigia wagombea wengine au kuwa na kura zisizo halali. Paul Makonda alitofautiana kwa mbali sana na wagombea wengine, jambo lililoashiria uungwaji mkono mkubwa ndani ya chama hicho.

Mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Wagombea watakaoshinda katika kura hizi, kwa kawaida hupendekezwa kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi husika.
 
Si rahisi bhana hata matokeo ya shule aligushi seuse haya ya kiswain ya ccm mxewwww kwendraaa
 
Paul Makonda ameshinda kwa kupata kura zaidi ya elfu 9 ambayo ni sawa na 97% na kuwaacha mbali wenzake kwenye kura za maoni ya ccm kwenye jimbo la Arusha mjini.

Wasiompenda msukuma mwana kolomije Paul Makonda sasa watakuwa nae sana hapo mjni
Shuga Mami yuko Kazini kama kawaida!!!!!
 
Paul Makonda ameshinda kwa kupata kura zaidi ya elfu 9 ambayo ni sawa na 97% na kuwaacha mbali wenzake kwenye kura za maoni ya ccm kwenye jimbo la Arusha mjini.

Wasiompenda msukuma mwana kolomije Paul Makonda sasa watakuwa nae sana hapo mjni
Safi xnaaa naona mabadilko yatafika mpk ngarenaro
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kada maarufu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, ameibuka mshindi kwa kishindo katika kura za maoni za kuwania nafasi ya ubunge kupitia CCM, baada ya kupata kura 9,056, sawa na asilimia 97.65 ya kura zote halali zilizopigwa.

Taarifa rasmi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi wa ndani wa CCM katika jimbo husika zimeeleza kuwa mchakato huo ulifanyika kwa amani, uwazi na kufuata taratibu zote za chama. Makonda ameonesha nguvu kubwa ya kisiasa na kukubalika kwa kiasi kikubwa na wanachama wa CCM.

Katika kura hizo, kulikuwa na wapiga kura zaidi ya 9,200 waliojitokeza, na ni wachache tu waliopigia wagombea wengine au kuwa na kura zisizo halali. Paul Makonda alitofautiana kwa mbali sana na wagombea wengine, jambo lililoashiria uungwaji mkono mkubwa ndani ya chama hicho.

Mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao. Wagombea watakaoshinda katika kura hizi, kwa kawaida hupendekezwa kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi husika.
464499123.jpg
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameshinda kura za maoni za Ubunge wa Arusha Mjini kwa kupata kura 9,056 sawa na asilimia 97.63 ya kura zilizopigwa.

Akitangaza matokeo hayo leo August 04,2025 Msimamizi wa uchaguzi amesema jumla ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo ni 10,186 na waliopiga kura ni 9,276 (91%) ambapo kura zilizoharibika ni 11 na kura halali zilizopigwa ni 9, 265.

Paul Makonda amepata 9,056 (97.63%), Mustafa 83, Gonga 46 , Ali Babu 28, Aminata 26, Mgweno 16 na Kishumbua 10.
 
Paul Makonda ameshinda kwa kupata kura zaidi ya elfu 9 ambayo ni sawa na 97% na kuwaacha mbali wenzake kwenye kura za maoni ya ccm kwenye jimbo la Arusha mjini.

Wasiompenda msukuma mwana kolomije Paul Makonda sasa watakuwa nae sana hapo mjni
Hivi kwanini asingegombea huko usukumani kolomije? Kwamba ana uchungu sana na maendeleo ya wananchi wa Arusha mjini au Kigamboni kwa kipindi kile, kuliko Mwanza!?
 
Arusha/wadudu wanachotwa akili kiboya sana. Makonda na festivals za nyama choma na Land rover zisizo na tija yeyote ile mnampa ubunge. Smh
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom