Rasmi NCCR Mageuzi yajitoa Uchaguzi Serikali za Mitaa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Chama cha NCCR-Mageuzi kimetangaza kujitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24. Msimamo huo umetolewa leo na Mwenyekiti James Mbatia jijini Dodoma.

====

Chama cha NCCR-Mageuzi kimetangaza kujitoa kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
1573462470499.png

Msimamo huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia jijini Dodoma akiongea na Wanahabari.

Ikumbukwe tayari CHADEMA, ACT Wazalendo na CHAUMA wameshatangaza kujitoa kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema Mamlaka ya Uchaguzi inawatambua wagombea wa vyama vya upinzani vilivyotangaza kujitoa kwenye Uchaguzi huo.
 
Wajiondoe wote kwani wakijiondoa hatuishi. Tulikuwa na maendeleo wakati wa chama kimoja na upinzani umetuletea vurugu na umaskini tu


State agent
Tanzania haijawahi kuwa na maendeleo tokea nyerere atoke ikulu, viwanda vyote reli Ndege mliuza ndipo sasa mtukufu magufuli kachukua pesa za walipa kodi kajifanya ni zake toka mfukoni anajidai kufufua viwanda, Reli kununua Ndege kwa cash kula 10% humo humo kwenye manunuzi na kwenye miradi yote mikubwa.
 
Back
Top Bottom