Rasmi mashabiki hawataruhusiwa Mechi ya Yanga dhidi ya River Plate.

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
10,053
24,446
IMG_7641.jpg

Hii ni taarifa rasmi ambayo imetolewa na club ya Yanga!

Hili ni pigo jingine kwa Yanga baada ya kuwakosa wachezaji wao tegemezi watatu!

Ikumbukwe kabla ya hili tangazo club ya Yanga tayari ilishakuwa imetangaza viingilio, na wapo wadau ambao tayari walishaanza kuzinunua!

Haya rudisheni hela zao sasa!
 
Haji Manara alikuwa akiona CAF imeruhusu Mashabiki wa Simba wajae Viwanjani alikuwa anadhan ni matokeo ya post zake za Instagram, hakuwa anajua nyuma ya pazia kuna kazi kubwa imefanyika

Sasa awasaidie Yanga waruhusiwe kujaza Uwanja

Kuna siku Babra alisema hadi kuruhusiwa kujaza Watu uwanjani kuna kazi kubwa sana imefanyika
 
Mbona baadhi ya nchi mashabiki wanaruhusiwa kuingia uwanjani? Mfano kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia!! Iweje sisi tukataliwe?

Hili shirikisho la mpira Afrika (CAF) limeanza kufuata tabia za ki ccm!
 
View attachment 1933049
Hii ni taarifa rasmi ambayo imetolewa na club ya Yanga!

Hili ni pigo jingine kwa Yanga baada ya kuwakosa wachezaji wao tegemezi watatu!

Ikumbukwe kabla ya hili tangazo club ya Yanga tayari ilishakuwa imetangaza viingilio, na wapo wadau ambao tayari walishaanza kuzinunua!

Haya rudisheni hela zao sasa!
Hapa nimeona rangirangi tu
 
Kua = Kuwa (kairudia zaidi ya mara nne)
Luninga = Runinga
Utakua = Utakuwa

Haya makosa madogo ya kiuandishi hayapaswi kufanywa na timu kubwa kama Yanga.
 
Kua = Kuwa (kairudia zaidi ya mara nne)
Luninga = Runinga
Utakua = Utakuwa

Haya makosa madogo ya kiuandishi hayapaswi kufanywa na timu kubwa kama Yanga.

Hiyo notice imetoka kwa Manara, hapo unategemea nini...!?
 
Back
Top Bottom