Rasmi: Kisinda ruksa kuichezea Yanga

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,554
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitisha usajili wa Twisila Kisinda kuichezea Yanga baada ya klabu hiyo kumuhamisha mchezaji wake wa kigeni Lazarous Kambole.

Awali Kamati hiyo ilizuia usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya dirisha la usajili kwa vile tayari Yanga ilikuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Licha ya changamoto hiyo, pia Kisinda aliombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ambayo tayari imepatikana.

Hivyo kwa kumuhamisha Kambole imepata nafasi ya kumsajili Kisinda kama ilivyokuwa imeshauriwa huko nyuma. Kwa mujibu wa Kanuni ya 62(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12.

Kambole amejiunga na timu ya Wakiso Giants inayocheza Ligi Kuu ya Uganda, na tayari TFF imetoa ITC.

D44CEED7-B1EB-4C1B-820F-BEA2D48B29E4.jpeg
 
Wachambuzi uchwara watakuja na sababu nyingine hapa

Bongo Raha Sana watu wanapenda kudandia mambo.

Angalia issue ya Mgunda na hii ndio utaipata jibu kwamba tuna wachambuzi wa hovyo Sana.

Ushauri wachambuzi wa mpira waache kuchukua bahasha za simba ya yanga.

Mkuu Soma Barua Uelewe
 
😂😂😂😂 tifuatifua mwisho wameamua kusalim amri!!!.

Karia na Tff yake ni wapumbavu na wasio na maono ya mpira!!. Aibu yaoooooo
 
Kisinda ni Kweli alizuiliwa. Kama Yanga Wasinge Fanya Jitihada za Kumtema Huyo Mchezaji wao, Kisinda Asinge Cheza

Kosa La Waandishi Liko wapi?
Kwa taarifa za ndani Yanga walishafanya kila jambo ila katibu mkuu alitoa jibu kabla hata ya kamati kukaa.
 
Kambole Alikuwa Hajapata Timu, Kitu kilicho Fanya Yanga Kuendelea Kusomeka Kuwa na Wachezaji 12 wa Kigeni. Na Mwanzo Yanga Hawakuwa katika Mpango wa Kuachana Na Kambole. Mpango wa Kuachana na Kambole Umekuja Baada Ya TFF kuwashauri kuwa Waachane na Mchezaji Mmoja Ndio Yanga Wakaona Wamtoe Kafala Kambole. TFF isingeweza Kubariki Uhamisho wa Kisinda wakati KAMBOLE HAJAPATA timu.
 
Kosa ni pale wanapohitimisha suala wakati bado mchakato unaendelea

Hawakuhitimisha Wao Walitoa Ushauri kwa Yanga. Yanga ndio walio Kuwa Wanasubiriwa Kufanya Maamuzi Ya Nani Aondoke na Aende wapi?

Hata yanga baada ya Kuitarifu TFF kuwa Wanamuondoa Kambole Waliambiwa mpaka wahakikishe anapata Timu kwasababu walisha Tangaza Kumsajiri
 
Kambole Alikuwa Hajapata Timu, Kitu kilicho Fanya Yanga Kuendelea Kusomeka Kuwa na Wachezaji 12 wa Kigeni. Na Mwanzo Yanga Hawakuwa katika Mpango wa Kuachana Na Kambole. Mpango wa Kuachana na Kambole Umekuja Baada Ya TFF kuwashauri kuwa Waachane na Mchezaji Mmoja Ndio Yanga Wakaona Wamtoe Kafala Kambole. TFF isingeweza Kubariki Uhamisho wa Kisinda wakati KAMBOLE HAJAPATA timu.
Hivi timu haiwezi kumuacha mchezaji na kumsajili mwingine paka mchezaji aliyeachwa apate timu nyingine??? Hii imekaaje wataalamu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom