Kwa hali ilivyo utekelezaji wake ni mgumu ajabu.Hii inaacha mawali mengi ya kiutendaji kuliko hata ilivyo sasa. Hii haijibu hoja za Wazanzibar, haitoi majibu kwa mustakabali wa Tanganyika wala haitaunusuru Muungano huu ambao watu wanafumba macho ili uendelee kudumu.
Kuna mambo ya kujiuliza na kutafakari hapa....
1.Itakuwaje iwapo Zanzibar Rais akitoka C.U.F - huyu atakuwa makamu wa Kwanza wa rais wa Jamhuri
2. Vipin iwapo mgombea mwenye asili ya Zanzibar akashinda nafasi ya urais wa Jamhuri ya Tanzani- hii itakuwa hivi Rais kutoka Zanzibar, Makamu wa Kwanza kutoka Zanzibar...Huu ni usawa ama?
3. Vipi nafasi ya serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar......kwa sasa anayeshindwa kati ya CUF na CCM automatically anakuwa Makamu wa kwanza wa Rais, ambapo pia chama kilichoshinda kinateua makamu wa pili wa Rais.........Je tutakuwa na Marais sita kwa vyeo na watano kwa idadi?
4. Je huyu Makamu wa pili wa Rais wa Muungano anapigiwa kura ama anateuliwa tu?
5. Nani atarithi/ama atakuwa Raisi kati ya Makamu wa Kwanza na Makamu wa pili iwapo Rais wa Jamhuri atashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu mbalimbali ikiwemo kifo? Kama ni Makamu wa Kwanza anapataje mamlaka kuongoza watu wa upande ambao hawakumchangua?
A: Nafasi za Urais Kivyeo ....
1.Rais wa Tanzania
2.Makamu wa Kwanza wa Rais - Tanzania
3.Makamu wa pili wa Rais - Tanzania
4.Rais wa Zanzibar
5.Makamu wa kwanza wa Rais - Zanzibar
6.Makamu wa pili wa Rais - Zanzibar
B: nafasi za urais kwa idadi(Marais)
1.Rais wa Tanzania
2.Makamu wa Kwanza wa Rais - (Ambaye pia atakuwa Rais wa Zanzibar)...likely
3.Makamu wa pili wa Rais - Tanzania
4.Makamu wa kwanza wa Rais - Zanzibar
5.Makamu wa pili wa Rais - Zanzibar
Natarajia uchambuzi makini kutoka kwa wadau mbalimbali wa siasa za Tz
Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye atakuja na maelezo mazuri juu ya mkanganyiko huu. Ni wendawazimu tu ndiyo watatetea upuuzi huu. Hii rasimu kama itapita italetea mgogoro mkubwa wa kikataba ambao haujawahi kutokea labda tangu dunia hii iumbwe.
Just to add an insult to the wounds, Sitta na gege lake watueleze utaratibu wa kupiga kura ya maoni utakuwaje kati ya wananchi wa Tanganyika na Zanzibar?
Je wote tutapiga kura ya NDIYO au HAPANA kuikataa au kuikubali hiyo rasimu ya katiba inayopendekezwa na CCM.
Kumbuka rasimu hiyo ya katiba ya
muungano ndiyo pia Katiba ya Tanganyika. Ina mambo ya muungano na mambo ya Tanganyika humo humo.
Je, wazanzibari watapiga kura ya NDIYO au HAPANA kwa rasimu yote, wakati kuna mambo ambayo hayawahusu.
Je, na sisi Watanganyika tutakubari mambo yote (kama ardhi, maliasili, serikali za mitaa) kuamuliwa na watu wengine (wazanzibari) wakati mambo hayo hayawahusu kabisa.
Sitta amelikoroga na kwa hili Mtikila naona akiibuka kidedea, kwani kabla hata hiyo rasimu ya katiba kama ikipita kabla haijaanza kutumika, Mtikila ataipinga mahakamani. Na serikali ya CCM ijaandae kugaragazwa! The writing is already on the wall.