RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

dhambi ya ubaguzi iakutafuna wewe na wenzio mpaka siku yenu ya mwisho

Mkuu siyo mimi, sheria ndo iko hivyo. Kama ni dhambi ya ubaguzi basi dhambi hiyo iko kwa waliotunga sheria hiyo na wala siyo mimi. Mimi nimesema facts za kisheria na wala sikuzitunga mimi. Unanionea tu.
 
kwa mtu mwenye hadhi ya mjumbe wa baraza kuu la chadema taifa, hili swali linakudhalilisha. hiyo tanganyika iko rwanda??? iko somalia??? kumbuka tanzania inatokana na tanganyika na zanz
 
Tanganyika inaweza kuwa na katiba ya mpito na bunge la mpito ambalo litatumia sehemu kubwa ya katiba ya Muungano kwa kuchomoa mambo ya Muungano na kubakiwa na misingi mingine na tunu zake kama ilivyotokea baada ya kupata uhuru. Hapo anaweza kuchaguliwa waziri mkuu wa muda ili kufanya uchaguzi wa 2015 na baada ya mwaka mmoja 2016 au 2017 uchaguzi kamili wa tanganyika yenye katiba ukafuata.
 
Mkuu siyo mimi, sheria ndo iko hivyo. Kama ni dhambi ya ubaguzi basi dhambi hiyo iko kwa waliotunga sheria hiyo na wala siyo mimi. Mimi nimesema facts za kisheria na wala sikuzitunga mimi. Unanionea tu.

soma tena comment yako niliyonukuu uone madhaifu yake, wewe ni kiongozi unapaswa uondoe uchama ktk hili..hii ni katiba ya nchi na hii nchi ni zaidi ya uzanzibar na utanganyika.
 
Hivyo basi, Mimi najiuliza, je Rasimu hii ikipita na kuwa katiba, ndo sisi watanganyika, tutaanzisha upya mchakato wa kutafuta katiba mpya ya Tanganyika yetu kabla ya 2015?

Itabidi uchaguzi upelekwe mbele kidogo japo hadi 2018 ili kukamirisha haya kwanza, na nafahamu Kikwete ni mjanja sana atakuwa hii ngoma alisha calculate.

Via Mobile.
 
Kutakuwa na Tume ya uchaguzi, itakayoundwa na wajumbe 7 ( hatujaambiwa wa Zanzibar wangapi na wabara wangapi) maana hapa tunaongelea Rasimu ya Muungano; Wote hawa 9 akiwemo mwenyekiti na makamu wake watateuliwa na Rais. Naomba ufafanuzi juu na Uhuru wa hii tume inayoteuliwa na Mh. Rais. Maana hiki kimekuwa kilio cha miaka nenda rudi.
 
Rasimu ya katiba mpya inataka tuwe na majimbo 25 tanzania bara yaani mkoa mmoja jimbo moja. Sasa kama hii itapita maana yake mapepari ndio watakaokuwa wabunge maana kufanya kampeni mkoa mzima si suala jepesi. Binafsi naona demokrasia itabanwa na tutazalisha viongozi mafisadi. Pia jangamoto za bungeni zitapungua
 
kwa mtu mwenye hadhi ya mjumbe wa baraza kuu la chadema taifa, hili swali linakudhalilisha. hiyo tanganyika iko rwanda??? iko somalia??? kumbuka tanzania inatokana na tanganyika na zanz

Huwa naogopa sana ku-comment mahala ambapo sijaelewa, ila hapa nimeelewa kwamba hukuelewa
 
Kuna mambo ambayo rasimu imetoa majibu ya maswali yako, mengine hayana majibu.
Kimsingi, hakuna cheo cha WAZIRI MKUU. Kimekufa, na kilikuwa hakina maana yoyote kwa sababu makamu wa raisi alikuwepo.
Kuhusu wizara; Wizara 15 ni nyingi kwa sababu mambo ya muungano ni machache. Mambo ya muungano ni kama ifuatavyo.

  1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – WIZARA YA KATIBA
  2. Ulinzi na Usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – WIZARA YA ULINZI, WIZARA YA MUUNGANO
  3. Uraia na Uhamiaji – WIZARA YA MAMBO YA NDANI
  4. Sarafu na Benki Kuu - ????????
  5. Mambo ya Nje – WIZARA YA MAMBO YA NJE
  6. Usajili wa Vyama vya Siasa – Hakuhitaji wizaraa hapa, inahitajika taasisi inayojitegemea.
  7. Ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya Kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano. – haihitajiki wizara.
Kwa hiyo, kwa mtazamo wangu; serekali ya jamuhuri ya muungano inatakiwa iwe na wizara sita au saba hivi basi.
Kuhusu mapato; Zanzibar tayari ina Zanzibar Revenue Board (ZRB) na Tanganyika nayo iwe na TRB yao ili kushughulikia ushuru wa bidhaa yasiyotokana na mambo ya muungano.

Kwa kweli hakuna maelezo kuhusu CAG. Lakini nadhani kwa vile mambo ya muungano ni machache tu, mambo nyeti na yanayomgusa mwananchi wa kawaida kama, afya, miundombinu, rasilimali (???), elimu, kilimo, nk yako mikononi mwa serikali za washiriki wa muungano, kila mshirika atakuwa na CAG wake.
 
Nakuunga mkono kwa 100% kuuliza swali hili kwani ni sawa na kutafuta kura za maoni kwa wananchi ili siku likijitokeza tuwe na majibu sahihi.
 
Ndugu Samson

Kuna vyama vya kichanga? Na vya kidongo ni vipi? Na vya kichuguu viko wapi?
kwa mfano kutakuwa na wagombea wa urais watatu kwa maana ya tanzania zanzibar,tanzania bara na rais wa shirikisho,kwa vyama venye uhaba wa watu wenye uwezo wa kuongoza vitapata wakati mgumu sana najaribu kufikiri kutoka chadema nani atagombea zanzibar,nani atagombea bara,na nani atagombea urais wa shirikisho.hali hii pia yaweza kukikuta chama cha nccr mageuzi na vyama vingine pia vichanga.
 
Miongoni mwa siku ambazo zitaingia kwenye kumbukumbu muhimu katika historia ya nchi hii ni tarehe ya jana 03-06-2013. Siku hii ambayo rasimu ya Katibu imetolewa kwa mara ya kwanza ikiwa ni hatua muhimu katika mchakato wa uundwaji wa Katiba Mpya ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Katika Rasimu hiyo imeainishwa kuwa kutakuwa na serikali tatu, yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Serikali ya Tanzania Bara. Jambo hili la kuwa na serikali tatu ni jambo kubwa linalostahiki kujadiliwa katika upekee wa aina yake.

Lakini jambo hili linaibua mkanganyiko wa kimantiki, kwa maana uwepo wa rasimu ya Katiba inayoitambua Tanzania Bara unalazimisha kuwepo kwa Taifa linalotambulika kikatiba kama Taifa la Tanzania Bara. Lakini ni nchi ipi hasa tunayoitaka kuitambua kama Tanzania Bara ni ile ile Tanganyika ya Awali..?

Jambo hili linakuza na kupamba msukumo chanya uliokuwepo awali wa kufufua TANGANYIKA na kwa namna nyingine kuhamasisha mchakato hasi wa kuunda Tanzania Bara (nchi mpya yenye jina lisilo na asili wala historia). Siioni wala siitambui TANZANIA BARA bali naikumbuka na kuitaja TANGANYIKA, ama lina nini jina TANGANYIKA hata iletwe TANZANIA BARA..?

Rasimu hii lazima izae watanganyika wenye kueleweka na kutambulika si kinadharia bali kikatiba kama watanganyika, wenye nchi kamili yenye mamlaka kamili. RASIMU HII NI MCHAKATO WA KUUNDA TANGANYIKA.,mchakato ambao ni lazima usimamiwe na uratibiwe na WATANGANYIKA WENYEWE. Nikiwa namaanisha si tena jukumu wala sehemu ya wajibu wa TUME YA KATIBA katika kusimamia kwa namna yeyote mchakato huo.

Lakini nauona ugumu wa kuifufua TANGANYIKA kwa kuivua Kutoka Katika koti la TANZANIA iliyoimeza na kuificha kabisa. Kwa mtazamo jambo hili ni kubwa na pana zaidi kuliko uundaji wa Katiba Mpya. U-TANGANYIKA ni Dhana mfu vichwani na katika mioyo ya watu.,sijui watu hawa ambao wengi wamezaliwa na wako chini ya miaka hamsini ya TANZANIA ambao hawajawahi kuishuhudia wala kuiishi Tanganyika wataipokeaje TANGANYIKA ya leo..?? Nchi huru yenye mipaka ambayo ilikuwepo..? ama Nchi mpya inayoundwa upya kabisa ambayo haikuwepo katika hata nadharia za watanganyika wenyewe..???
HAKIKA HUU NI UTATA..???
 
hivi sasa, ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na tbc1. Mgeni rasmi ni rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania jakaya mrisho kikwete... Katiba mpya kwa tanzania yenye neema

tufuatilie

mengi nayaona ni ushindi kwa mh mch mtikila, mgombea binafsi, pamoja na tanganyika huru
 
Its a wastage of resources kuwa na serikali tatu.

If we are seriously into our Union, tuwe na serikali moja.

I see this as a diversion into the facts that need be addressed.

Mambo yote ambayo ni controversial na tyalionekana na wazee wetu hapo mwanzo, (Karume na Nyerere) yamo humu ndani).

I see a clear and crystal intwntion to diversify us from facts such as poverty and natural resources.

Tutaachwa tukijadili haya mambo watu wakifanya yao.

I suggest katika rasimu mpya neno Tanzania Bara be removed and replaced by Tanganyika, Hakuna kitu kama TANZANIA BARA bali kunaTanganyika.



Kama wanaamua kutumia neno Tanzania Bara, basi na Zanzibar itamkwe Tanzania visiwani. otherwise, tunataka kuona Tanganyika
 
Rasimu ya katiba mpya inataka tuwe na majimbo 25 tanzania bara yaani mkoa mmoja jimbo moja. Sasa kama hii itapita maana yake mapepari ndio watakaokuwa wabunge maana kufanya kampeni mkoa mzima si suala jepesi. Binafsi naona demokrasia itabanwa na tutazalisha viongozi mafisadi. Pia jangamoto za bungeni zitapungua
...kaka....chambilecho "maandiko matakatifu", wengi wataitwa wachache watachaguliwa...!muda ukiwadia wote wanaoamini "wanachagulika" watajitoa mbele, wajieleze kwa umma wa sehemu husika...na atakaekuwa kaaminiwa na kukubaliwa na wengi zaidi katika umma huo ndio atakuwa muwakilishi wa eneo hilo bungeni...si masihara hata kidogo! ni hivyo! ...sasa iliyobaki ni kwa wapiga kura wenyewe!!!...labda kwa kusaidiana ningeomba nipewe jibu na wenzangu ktk JF ya GT...rasim pia ina namna ambayo wapiga kura wanaweza mshughulikia (kidemokrasia) mwakilishi wao ambae "wamemgumia" kuwa ni "snake in the monkey shadow"? au itakuwa "adios amigo" mpaka uchaguzi unaofuata (endapo "eloe" atakua amemjalia maisha "zuga" huyo?)
 
hivi kwanini mmekaa kibaguzi baguzi nyie??? shame on you!!!!!!!!
Huna akili hata moja hata ya kumegea tonge la ugali,yaani unataka nchi yetu tuwauzie wazanzibari wenye wimbo wao,bendera yao,katiba yao, serikali yao,wimbo wa taifa wao halafu sisi tusiseme kwa sababu kuna watu wanapata book saba kwa posti za kutibua mijadala ya kitaifa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom