Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Kwa kuwa Rasimu iliyozinduliwa jana inazungumizia Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania tu na siyo nchi washirika,
kwa kuwa Rasimu imependekeza serikali 3 ya Muungano, Zanzibar na Tanganyika, na
kwa kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar ina mifumo kamili ikiwepo ofisi, viongozi,sheria mbali mbali zinazoongoza nchi hiyo ikwepo mgawanyo madaraka miongoni mwao, na upande wa Tanganyika hamna kitu, na
Kwa kuwa serikali ya Tanganyika haina sheria yo yote na Tume ya Uchaguzi hasa ktk ngazi za wilaya na kata na mitaa nk,
Hivyo basi, Mimi najiuliza, je Rasimu hii ikipita na kuwa katiba, ndo sisi watanganyika, tutaanzisha upya mchakato wa kutafuta katiba mpya ya Tanganyika yetu kabla ya 2015?
Ikumbukwe kuwa, wazanzibar wana katiba yao tayari inayotoa mwongozo kuhusu uchaguzi na tume ya uchaguzi nk. Tanganyika haina mwongozo wowote. Na Tanganyika inahitaji aina viongozi wanaohitajika na kazi zao, idadi wa wabunge na kazi zao, Tume ya uchaguzi, kama Tunahitaji wakuu wa wilaya/mikoa au la. Tunahitaji mamlaka ya serikali za mitaa iweje nk.
Tunahitaji kujua majukumu na mipaka ya Rais na mawaziri wa Tanganyika. Yote yanatakiwa yawepo ktk katiba mpya ya Tanganyika. Sasa najiuliza, je, rasimu hii ikipita kuwa katiba kamili 2014, ndo sisi watanganyika tutaanzisha upya mchakato upya wa katiba tena? Je, itawahi uchaguzi wa 2015?
Ni swali linalonichanganya.
Au ndo siri ya maombi ya miaka 2 zaidi ya kikwete imejificha hapa?
NB;
Nimetumia Tanganyika Vs Tanzania bara kwa kuwa mujibu wa Mapendekezo ya Tume nchi washrika zinaruhusiwa kuwa na mahusiano ya moja kwa moja na nchi za nje. Kwa hiyo, kuwa na jina Tanzania na Tanzania Bara ktk medani za kimtaifa itawachanganya jumuia za kimataifa.
Nawasilisha