RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Watu walitoa maoni yao kuhusu hizo
ofisi ulizotaja lakini chaajabu sijui
wamesahau ama ni nini.

Nakumbuka kwenye bajeti ya utawala
bora hata Wabunge walitaka Katiba
inayo itamke bayana kuhusu ofisi
hizi ila najua kwenye Bunge la Katibu
huenda moto ukawaka sana.
 
Mkuu utaratibu huu uko nchi nyingi tu nao ni kwa wapiga kura kujiandikisha kumkataa mwakilishi wao na kisha kupiga kura. Kura zikitosha jamaa anarejeshwa alikotoka anawacha wananchi wachague mwingine
P
Patahitaji utaratibu mzuri na usimamizi makini, kinyume chake itakuwa vurugu. Vyama vya Siasa (au hata watu wenye maslahi yao) vinaweza pia kutumia mwanya huu kufanya jimbo "lisitawalike". Ebu nidokeze mojawapo ya nchi hizo ili nifuatilie kuona wanavyousimamia.
 
This is great! nimeisoma rasimu yote. softcopy ipo Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa ajili yako.
Rasimu inaleta mwanga mzuri wa Tanzania tunayoitaka hasa pale ambapo inaonesha nia ya uwajibikaji zaidi wa serikali kwa wananchi na pia lengo la kupata kweli viongozi wa kisiasa kwa ajili ya kusimamia serikali na kuongoza wananchi badala ya maslahi binafsi ilivyokuwa huko nyuma.
Ile vurugu ya kutafuta uongozi sasa nadhani itakwisha na wananchi watapata hasa chaguo lao kwa manufaa yao. Sura za mwanzo zinalenga kulirejesha Azimio la Arusha kwa kurudisha misingi ya uongozi bora, la msingi ni usimamizi na utekelezaji wa sheria hii mama. Imejitahidi kuondoa maslahi binafsi ya viongozi kwa kutenganisha biashara na utumishi, imeondoa pia mgongano wa kimaslahi baina ya utendaji na siasa kwa kutoruhusu watendaji wa umma kushiriki siasa labda kama wataridhia kukoma kwa ajira za umma ikiwa ni pamoja na vyombo vya dola, n.k. Wito wangu ni kuwa viongozi wa majimbo (mikoa na wilaya) lazima wawe na uchungu wa wananchi wanaowachagua; hiki ni kilio cha watu cha muda mrefu, tulisema wakuu wa mikoa na wilaya wapo kwa maslahi ya dola, sasa isije tena ikawa hawa wa majimbo wakawa kwa maslahi ya dola au binafsi, ingawa sidhani kama lengo la katiba ni kubakiza rasilimali za mahali zifanye kazi mahali pale tuu. Mtizamo wangu wa jumla ni katiba nzuri, ommissions chache za spellings zinarekebishika. :nod:
 
Ndugu zangu wapendwa wa Shirikisho yaani wenzetu wa Zanzibar, kwaniaba ya waTZB wote, naomba sn amani na upendano tuweke mbele kwa maslahi ya TZ shirikisho, kwani kama tutaweka ushabiki na utengano wakusema nyie wa bara sisi wa Zenji tutauana, bila sababu, ninauhakika kwa TZB hatuna hili lkn makubwa yatakuwepo kama tusipomuweka Mungu mbele na upendano wetu na mshikamano wetu tusipouweka mbele,.
Viva Whole TZ, Viva TZB Viva Zanzubar yenye madalaka yake chini ya muungano, naamini kila mshiriki atajifunza kwa mwenzake.
Mungu zibariki serikali zetu tatu zijazo.
Amen.
 
Rasimu ya katiba inasema moja ya sifa za kugombea ubunge ni lazima uwe na elimu ya kidato cha 2. Urais ni shahada.Wale wenye elimu ya msingi sahau ubunge.
 
maswala ya standards za bidhaa za viwandani etc pia yangekua ya kimuungano zaidi. Tanzania Bureau of standards and other standardization agencies
 
Hii rasimu ya Katiba mpya inaonyesha mabadiliko makubwa ya Kiserikali na ya madaraka katika sekta mbalimbali ... kwa kifupi Tanzania itakuwa mpya.... hii inaamana kwamba waliokuwa madarakani kuanzia mawaziri, manaibu wao, wakuu wa mikoa, wa wilaya....kwa sasa hawana uhakika na nini kitatokea na kitawatokea baada ya katiba kuanza kutumika rasmi sasa ni wakati wa wao kujiandaa lakini HALAHALA CHONDE CHONDE wasikwapue chao mapema....
 
Hebu angalia kichwa chako cha habari na contents kisha fanya marekebisho na utaje na Ibara au kifungu kinachopendekeza hivyo ili rahisi kurejea kwenye rasimu husika. thanks
 
rushwa ni janga la kitaifa, ni lazima utendaji wa taasisi ya kupamba na rushwa uwe kwenye katiba, kama vile wa CAG, tena sasa waifanya kabsa kuwa tume ya kupambana na rushwa...badala ya taasisi
 
Ss hawa wabunge wa viti maaalum ina maana ndo mwisho??
Mm nilikuwa na mpango wa kugombea ayaaaaaa dili limeharibikaa
 
Hili lilkuwa linanisumbua iweje Rasimu ya Katiba izinduliwe lakini isiwekwe hata kwenye website yao. Ilipaswa kuanzia jana mara tu baada ya uzinduzi iwekwe. Nimeangaika kuippata kwenye tovuti yao haifunguki, inaonekana imelemewa na watu wengi wanaojaribu kufungua. Mkuu tusaidie kwa kuiweka hapa kama attachment ili tuipate pia.
 
Umeona Polisi? Hiyo ndiyo taasisi ya kupambana na rushwa (kwa kawaida).

Rasimu ya katiba sio katiba yenyewe.
 
Naomba kuelimishwa kama katika mfumo huu wa serikali tatu ni kwamba hii katiba itakuwa ya mpito kuelekea kwenye uundaji wa dola ya Zanzibar na Tanganyika na baadaye Tanganyika na Zanzibar itabidi watengeneze katiba zao kwa reflection ya katiba hii wakizingatia mambo yasiyo ya muungano. Baadaye itaundwa serikali ya muungano ambayo ita administer yale mambo saba ya muungano na kujenga umoja katika muungano na raisi wa muungano hatokuwa na nguvu bali ni symbol ya muungano na umoja katika muungano wetu. OR, serikali za Tanganyika na Zanzibar zitaongozwa na mawaziri wakuu watendaji na raisi wa serikali ya muungano yeye atakuwa symbol tu kutuunganisha baina ya pande mbili?!
 
Lakini Nyerere na Karume sio mihimili ya taifa hili.

walikuwa ni personalities na washakufa na hatuwezi kuendelea kuongozwa na wafu

tuna katiba na mihimili ya taifa

na kama zanzibar wanataka kuondoka wapewe nafasi ya kufanya referendum waamue hatma yao

kuna ubaya gani hapo?

Hoja si kuongozwa na wafu au la...kila taifa lina historia yake, na hatuwezi kujitenga na hao watu wawili tukitaka kurudi nyuma katika historia for reference purpose, ni sajabu kuwa na jambo jipya bila ya la zamani, hivyo basi tunahitaji mawazo yaliyoweka msingi wa taifa hili katika kujenga taifa jipya, that is if we want Taifa jipya, We can let Zanzibar go, but faida ya Zanzibar kwenda ni ipi?? iKIBAKI NI IPI?? Ok Zanzibar wanabendera yao, hiyo ina badili nini?? USA the most powerful country in the world bado inaongozwa na misingi ya uhuru waliyoweka kina Abraham Lincon, na Bado wanawaheshimu na kukubali misingi yao bora, sisi taifa changa ambalo bado tunaishi kwa misaada tunajua NINI katika anga za kisiasa na kidemokrasia?? I think we are better of together than being solo, we needa stronger union than this, Warioba and his group daima watakua na laana ya kulibomoa Taifa hili kwa kisingizio cha Katiba mpya.
 
Calm down everybody! Naona mmekuwa emotional kidogo.

Points kama "hakuna nchi iliyowahi kuitwa Tanzania Bara, kwa hivyo hilo jina lifutwe" zinatoka wapi? Hakuna vile vile nchi iliwahi kuitwa Tanzania!

Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ni majina yanayojumuisha jiografia vizuri sana. Tanganyika ni jina lililokuwepo zamani. Limekufa kama yalivyokufa majina Rhodesia, Zaire na Nyasaland.
 

Similar Discussions

36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom