Rasimu ya Katiba ndiyo imeshatolewa na kazi sasa iko miongoni mwetu kwani Mabaraza ya katiba yatapata mawazo yetu sisi wananchi. Naomba tujadili lau machache yanayohusu maisha yetu ya kila siku kama watanzania. Mi naanza na suala la Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na hasa ile sehemu ya kwanza katika sura ya tisa . Kimsingi sehemu hii inatoa aina za wabunge watakaounda bunge hilo kama ifuatavyo;
SURA YA TISA
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
KUUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
105.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.
(2) Wajumbe wa Bunge watakuwa wa aina zifuatazo:
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;
(b) Wabunge watano watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa Washirika wa Muungano.
(3) Kwa madhumuni ya Ibara ya ndogo (2)(a), kila mkoa kwa upande wa Tanzania Bara na wilaya kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ni jimbo la uchaguzi.
(4) Katika kila Jimbo la Uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme.
(5) Wabunge wote katika kila Jimbo la Uchaguzi watapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hiina sheria inayoweka utaratibu kuhusu mambo ya uchaguzi.
My take ni sehemu ya 4. Je kuna haja bado ya kutoa nafasi za namna hiyo. Ili kuhakikisha kuwa raslimali za Taifa zinatumika ipasavyo nadhani kusingejitokeza suala la jinsia. Wajitokeze wagombea kutafiuta nafasi moja tu ya ubunge la sivyo najiuliza utendaji wao utakuwaje na hasa ikitokea wakawa ni kutoka vyama viwili tofauti.
Na tujadiliane kwa pamoja. Isome vyema katiba kisha njoo na hoja yako
The Listener - Ex Detective