RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

kwani umri wake nao ndio utasimama au utazidi kusonga mbele?mbona akina sumaye hawapo kwenye medani za siasa kwa sasa and still wanaota kuhusu urais?tujadili mambo ya muhimu tusianze kujadili watu kwa chuki binafsi!!!
 
Rasimu ya Katiba ndiyo imeshatolewa na kazi sasa iko miongoni mwetu kwani Mabaraza ya katiba yatapata mawazo yetu sisi wananchi. Naomba tujadili lau machache yanayohusu maisha yetu ya kila siku kama watanzania. Mi naanza na suala la Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na hasa ile sehemu ya kwanza katika sura ya tisa . Kimsingi sehemu hii inatoa aina za wabunge watakaounda bunge hilo kama ifuatavyo;

SURA YA TISA
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO
SEHEMU YA KWANZA
KUUNDWA KWA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO

105.-(1) Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano.

(2) Wajumbe wa Bunge watakuwa wa aina zifuatazo:
(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;

(b) Wabunge watano watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuchaguliwa kuwa wabunge kuwakilisha watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa Washirika wa Muungano.

(3) Kwa madhumuni ya Ibara ya ndogo (2)(a), kila mkoa kwa upande wa Tanzania Bara na wilaya kwa upande wa Zanzibar, itakuwa ni jimbo la uchaguzi.

(4) Katika kila Jimbo la Uchaguzi kutakuwa na nafasi mbili za ubunge, moja kwa ajili ya mwanamke na moja kwa ajili ya mwanamme.

(5) Wabunge wote katika kila Jimbo la Uchaguzi watapatikana kwa kupigiwa kura na wananchi kwa mujibu wa masharti ya Katiba hiina sheria inayoweka utaratibu kuhusu mambo ya uchaguzi.


My take ni sehemu ya 4. Je kuna haja bado ya kutoa nafasi za namna hiyo. Ili kuhakikisha kuwa raslimali za Taifa zinatumika ipasavyo nadhani kusingejitokeza suala la jinsia. Wajitokeze wagombea kutafiuta nafasi moja tu ya ubunge la sivyo najiuliza utendaji wao utakuwaje na hasa ikitokea wakawa ni kutoka vyama viwili tofauti.

Na tujadiliane kwa pamoja. Isome vyema katiba kisha njoo na hoja yako

The Listener - Ex Detective
 
Nimeipenda rasimu ya katiba mpya, ila nilipoingalia kwa jicho jingine nikagundua kuna gharama kubwa sana kuifanya iwe halisi

Ila always cheap is expensive.

Tusiogope
 
Ninangojea niipate rasimu na kuisoma niilewe vizuri. Lakini kabla ya hapo, nimefurahishwa na tume kupendekeza katika nchi hizi mbili zilizoungana, kila nchi iwe na serikali yake. Tanganyika (sio Tanzania Bara) na Zanzibar. Kutokana na hilo, je kila nchi itakuwa na Raisi wake? Je kiongozi wa kusimamia masuala yale saba yaliyowekwa kuwa ndio masuala pekee ya Muungano, naye ataitwa Rais? Je katiba ya kushughulikia yale masuala saba ya Muungano ndio hiyo inayojadiliwa sasa? Je kama kila nchi itakuwa na katiba yake, mamlaka ya katiba ya muungano yanaishia kwenye yale masuala saba ya muungano na sio vinginevyo? Ninapata kigugumizi sana kwa hili.
 
Unaweza kuna na jambo la maana la kujadili lakini tumia Kiswahili kwa sababu neno "diversify" hapo juu halina maana uliyokusudia. You seem to have serious issues with the Queen's lingua franca. Look at your third phrase, just too out of conventional thinking.

i had no time to edit, but i am sure in regadless of minor errors my contribution is noted..
 
Ninangojea niipate rasimu na kuisoma niilewe vizuri. Lakini kabla ya hapo, nimefurahishwa na tume kupendekeza katika nchi hizi mbili zilizoungana, kila nchi iwe na serikali yake. Tanganyika (sio Tanzania Bara) na Zanzibar. Kutokana na hilo, je kila nchi itakuwa na Raisi wake? Je kiongozi wa kusimamia masuala yale saba yaliyowekwa kuwa ndio masuala pekee ya Muungano, naye ataitwa Rais? Je katiba ya kushughulikia yale masuala saba ya Muungano ndio hiyo inayojadiliwa sasa? Je kama kila nchi itakuwa na katiba yake, mamlaka ya katiba ya muungano yanaishia kwenye yale masuala saba ya muungano na sio vinginevyo? Ninapata kigugumizi sana kwa hili.

Kuna tatizo lililopo kw awabunge wa Zanzibar kuwepo katika Bunge la Muungano kujadili mambo ambayo sio Union matters kwahilo nadhani imesolve hiyo mischief
 
Heh! Mwanzo na mwisho wa Zito?
Kwa nini? Kwani Zito hatafika miaka 40? Unamaanisha nini?
He is too young and has a bright future ahead of him, ajue tu kuzichanga karata zake vizuri(aachane na mautoto utoto yake.)
 
HABARI WANA JF!

Jana tume ya mabadiliko ya katiba iliwasilisha kwa wananchi rasimu sifuri ya katiba ya Jamhuri ya shirikisho la Tanzania kwa kimombo The federal republic of Tanzania.

Kwa mujibu wa rasimu hii, binafsi naona mambo muhimu ambayo hayajatajwa au kwekwa kwa discusion.

1. Rais kutoshtakiwa-Ni makosa kumwacha rais huru kwa kumwekea kinga kisheria. Hii inapelekea wengi wawe wajeuri, wasiotii kuwa dola inatoka na inaanzia kwa wananchi. Ni wazi wataendelea kujificha chini ya kivuli cha kinga ya kutoshitakiwa. Ni heri iwe rais anaweza kushitakiwa ili hata wale wanoona Ikulu mi mahala pa kwenda kuficha maovu yao waone kuwa bado hawatakuwa wamekimbia mkono wa sheria. kama watu wote ni sawa kama ilivyoainishwa katika Rasimu sifuri ya katiba ya Jamhuri ya shirikisho la Tanzania, rais naye ashtakiwe kwa makosa aloyafanya kabla na hata baada ya kipindi chake cha urais mara inathibitika kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya ofisi au namna yoyote ya ukiukaji wa sheria za nchi na ndio maana anaapa kuilinda na kuitetea katiba husika.

2.Suala la wakuu wa wilaya na mikoa-natamani au naonelea kusiwe na nafasi hizi maana zimekuwa za kisiasa tu na hazitusaidii katika kusogeza gurudumu la maendeleo.badala yake kuwe na mameya na wakurugenzi tu. Mameya waendelee kuchaguliwa miongoni mwa madiwani katika halmashauri husika.

3.katiba kutamka tu kuwa Viongozi wasishiriki Rushwa, ufisadi, na kuwa na maslahi binafsi kabla ya yale ya taifa, haitoshi.haya hata sasa hivi yapo kwenye nyaraka mbali mbali za utendaji wa serikali yetu lakini hayafanyiwi kazi.
Kaitba iweke hukumu ikibidi ya kifo kwa wale watakaoshiriki maovu haya.

4.
 
Jana wakati jaji warioba anawasilisha hotuba yake kwa wananchi kuhusu rasimu ya katiba mpya, alipofika kwnye kipengele cha umri unaofaa kugombea urais na kutaja kuwa tume inapendekeza umri ubakie kama ulivyo hivi sasa wa miaka 40, zitto kabwe, mbunge wa kigoma kaskazini, naibu katibu mkuu wa chadema nusura alie..alinuna, akakunja uso na mbaya zaidi kamera ya tv ilimmulika na kuonekana na taifa zima lililokuwa likifuatilia tukio hilo..

my take: katiba mpya ni mwanzo wa mwisho wa zitto kisiasa? Mana alisema hatgombea tena ubunge hope alikuwa na malengo flani
Hapo in bold unataka kukoleza story yako tu. Mbona sisi hatukuona hivo? He was relaxed na alisema alipoulizwa kama atagombea ubunge jimboni kwake, au kama kuna uwezekano wa kugombea Tanzania Bara alijibu tu "hapana, sitagombea" (On his twitter acc). Huko kununa wewe uliona wapi?
 
Theoretically mko sawa kabisa, hata mimi nilijua hivyo hapo awali. Think outside the cage, utaona ukweli kuwa wasio na digrii wamefanyakazi kubwa nchi hii, nimekupa mifano hapo juu.

Pia usomi wa elimu ya kutazamia hakika hatutafika popote, njiani kumetegwa mabomu; hiki pekee ndo kinafanya tunaibiwa zaidi baada ya kusoma kuliko hapo mwanzo. Narudia digrii isiwe katika kigezo cha kuwa waziri.

Zaidi ni ubaguzi kwa wasio na digrii (80% ya waTZ), hali ambayo tumeshuhudia wachapakazi wakihaha kutafuta digrii ili waweze kukidhi masharti ambayo hayana tija. Mwisho wake digrii zinauzwa na wenye njaa zaidi ya hao wachapakazi wanastahili ila vigezo vimewakwamisha. NCHI NI YA WOTE, nani kahalalisha wasomi pekee tena wasio na muuongozo wa elimu ndo wenye akili za kutuongoza??? hakuna kitu kama hicho. Elimu isije kutumika na wamiliki wake(Developed Countries) kama weapon of war katka dunia ya leo. TUNATAKA WACHAPAKAZI NA WAKWELI full stop.
 
Sijui ni rasimu au ni white paper au ni mwongozo au frame ya katiba mpya hili sasa ndio suala ambalo tuwambie Watanzania na kwamba kule tuendako hatujafika na hatuna sababu ya kupongezana kwani kuanzia jana ndio tumeanza hatua ya kwanza ya safari yetu ndefu ya kuelekea kupata katiba ya Watanzania. Sitaki kuwa msemaji katika maandishi yangu leo ila naomba niwaletee busara za 'Mtume' Nelson Mandela Rais wa Kwanza Taifa Huru la Afrika Kusini.

1. "Our greatest fear is not that we are inadequate, but we are powerful beyond measure, it is our light, not our darkness that frightens us" (kwa busara hii fuatilia mchakato wa katiba)

2. "There is nothing enlightened about shrinking so that other people won't feel insecure around you. We were born to make manifest the glory of God within us. It is not just in some; it in everyone. And, as we let our own light shine, we consciously give other people permission to do the same. As we are liberated from our fear, our presence automatically liberates others. I have walked that long road to freedom. I have tried not to falter; I have made missteps along the way. But i have discovered the secret that, after climbing a great hill, one only finds that there are many more hills to climb" (Je umechangia nini hadi sasa na unajiaanda kufanya kwa ajili ya zao la katiba mpya ya Watanzania)

3. "There is no easy walk to freedom anywhere, and many of us will have to pass through the valley of the shadow of death again and again before we reach the mountaintop of our desires" (umejiandaa kutoa nini ili kufikia m,abadiliko haya)

4. 'There is nothing like returning to a place that remains unchanged to find the ways in which you yourself have altered' (hatuwezi kurudi tulikokukataa lakini sheria yetu ya katiba mpya inatupa fursa ya kusonga mbele hata kama hatukukubaliana au inaturudisha ground zero)

Tume kwa kiasi kikubwa imefanya kile ambacho tulikitaka na kukisemea sasa kazi kubwa inaanzia pale ambapo nukta ya Mhe Sinde iliishia na hapo sasa ndio utaratibu uliolalamikiwa wa kufinyanga mabaraza utakapoanza kufanya kazi. Ili kazi ya Tume ya Katiba iwe takatifu na yenye utukufu ndani yake mchakato wa mabaraza ulipaswa kusimamiwa ili nao ulete zao linalofanana na zao lao la fremu hii ambayo kila mtu anaipongeza.

Kimsingi vita bado mbichi kwani sasa ndio utaona msuguano mkali kutoka kwa wahafidhina na makundi ambayo yanahoja zao ambazo hazijazingatiwa. Kama vile CAG anawajibika kwa nani na uteuzi wake ukoje, wizara 15 ni zipi zitajwe kwenye katiba, Nafasi ya Waziri mkuu ipo? kwa kuwa sasa tunaenda kwenye federal government, Katiba ya bara ipo? Kimsingi katiba ya Jamhuri Muungano ndio nguzo na katiba ya bara na Zanzibar ziweje na asilimia 97 ya mambo yaliyomo kwenye katiba ya Muungano lazima yaingizwe katika katiba za serikali za bara na Zanzibar bila marekebisho na nyogeza yao kwa kadiri watakavyoona

MISEMO YA NELSON MANDELA INAWEZA KUTUSAIDIA KUJUA KAMA TUMEFIKA AU BADO NA KWA KAZI IPI TUMEFIKA AU BADO. MADIBA KWANGU NI MODEL NA NI MTUME

VIVA WAPAMBANAJI, WAKO WANAOBEZA MLICHOFANYA NA WATAENDELEA KUBEZA ENDELEENI KUTUPA NURU KWANI NURU YENU NA WELEDI WENU NI UKOMBOZI KWETU.
 
Ninangojea niipate rasimu na kuisoma niilewe vizuri. Lakini kabla ya hapo, nimefurahishwa na tume kupendekeza katika nchi hizi mbili zilizoungana, kila nchi iwe na serikali yake. Tanganyika (sio Tanzania Bara) na Zanzibar. Kutokana na hilo, je kila nchi itakuwa na Raisi wake? Je kiongozi wa kusimamia masuala yale saba yaliyowekwa kuwa ndio masuala pekee ya Muungano, naye ataitwa Rais? Je katiba ya kushughulikia yale masuala saba ya Muungano ndio hiyo inayojadiliwa sasa? Je kama kila nchi itakuwa na katiba yake, mamlaka ya katiba ya muungano yanaishia kwenye yale masuala saba ya muungano na sio vinginevyo? Ninapata kigugumizi sana kwa hili.

Mkuu usingoje fuata link hapa: http://www.katiba.go.tz/attachments/article/182/Rasimu _Final_ (1).pdf
 
Dogo zito alijiamini sana kuwa lazima agombee haya sasa hata jimboni alishaaga ila nasikia anaenda kugombea kigoma mjini jimbo la awali limemshinda.
 
Ninangojea niipate rasimu na kuisoma niilewe vizuri. Lakini kabla ya hapo, nimefurahishwa na tume kupendekeza katika nchi hizi mbili zilizoungana, kila nchi iwe na serikali yake. Tanganyika (sio Tanzania Bara) na Zanzibar. Kutokana na hilo, je kila nchi itakuwa na Raisi wake? Je kiongozi wa kusimamia masuala yale saba yaliyowekwa kuwa ndio masuala pekee ya Muungano, naye ataitwa Rais? Je katiba ya kushughulikia yale masuala saba ya Muungano ndio hiyo inayojadiliwa sasa? Je kama kila nchi itakuwa na katiba yake, mamlaka ya katiba ya muungano yanaishia kwenye yale masuala saba ya muungano na sio vinginevyo? Ninapata kigugumizi sana kwa hili.
Viongozi wakuu wa nchi za Tanganyika na Zanzibar wataitwa MAGAVANA.Rais atakuwa mmoja tu naye ni ni RAIS SHIRIKISHO i.e JMT
 
Wewe ni mnafiki tu!! Jitahidi kuu upgrade unafiki wako ili angalau usipoeleweka uchekeshe,sasa kama huu haueleweki,wala hauchekeshi,tungeuweka hata kwenye jokes lakini bado hau fit!! Tupa kule
 
mkuu katika dunia ya sasa hatuhitaji wanaharakati watuongoze coz watatuongoza kwa hisia na matukio.hata kama wasomi ni wachache zaidi ya wasiowasomi hiyo sio sababu ya msingi.na cheo sio uwaziri pekee,bado kuna ngazi nyingine hao wengine wawepo huko.
 

Similar Discussions

36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom