Rangi za aura

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,102
2,717
Mwili unatoa rangi. Rangi zinabubujika kutoka kwenye mwili kulingana na tabia au afya ya mtu. Hapo ndipo dini inafanana na physics.

NYEKUNDU. Katika hali yake nzuri nyekundu inaonyesha nguvu ya kujituma. Majenerali wazuri na viongozi wa watu wana rangi nyekundu nyingi katika aura yao. Ipo aina ya rangi nyekundu iliyo dhahiri na ina kingo za manjano . Hii inaonyesha mtu ambaye ni "Mpiganaji" (Crusader)- ambaye anajitahidi kila wakati kusaidia wengine. Usichanganye hii na mchochezi wa kawaida(ordinary meddler); "nyekundu" yake itakuwa "kahawia"! Miale myekundu dhahiri inayotoka kwenye kiuongo Cha mwili(organ) inaonyesha kuwa kiungo hicho kiko katika afya nzuri sana. Baadhi ya viongozi wa ulimwengu wana rangi nyekundu nyingi katika uundaji wao. Kwa bahati mbaya, mara nyingi sana , huchafuliwa na vivuli vya uchafu.

Nyekundu mbaya(a bad red), yenye matope au giza sana, inaonyesha hasira mbaya au mtu mwenye ghadhabu . Mtu huyo si wa kutegemewa, mgomvi, msaliti, mtafuta-binafsi kwa gharama ya wengine. Nyekundu zisizo dhahiri(nyepesi)mara kwa mara huonyesha msisimko wa neva. Mtu mwenye rangi nyekundu "mbaya" anaweza kuwa na nguvu za kimwili. Kwa bahati mbaya pia atakuwa na nguvu katika kufanya vibaya.

Wauaji daima rangi nyekundu iliyodhalilika(degraded red) katika auras zao. Nyekundu nyepesi(LIGHTER, si "wazi") inaonesha wasiwasi na kutokuwa na utulivu kwa mtu. Mtu kama huyo yuko anashughulika sana - anasisimka sana - na hawezi hats kukaa kutulia kwa zaidi ya sekunde chache kwa wakati mmoja. Hakika mtu wa namna hii anajifikiria sana. Nyekundu karibu na viungo (organs)zinaonyesha hali yao. Nyekundu iliyofifia, yenye rangi ya hudhurungi hata, inayosonga polepole kwenye kiuongo inaonyesha saratani. Mtu anaweza kujua kama saratani ipo AU IKIWA NI ITAKUJA BAADAYE! Aura inaonyesha ni magonjwa gani yataathiri mwili baadaye, iwapo hatua za matibabu hazitachukuliwa. Hii itakuwa mojawapo ya matumizi makubwa zaidi ya "Tiba ya Aura" katika miaka ya baadaye.

Nyekundu yenye madoadoa, inayong'aa kutoka kwenye taya inaonyesha maumivu ya jino; msukumo wa hudhurungi kwa wakati kutoka kwa nimbus (nimbus ni halo inayozunguka kichwa)unaonyesha hofu katika wazo la kutembelea daktari wa meno. Scarlet kawaida "huvaliwa" na wale ambao wanajiamini kupita kiasi; inaonyesha kwamba mtu anajipenda sana. Ni rangi ya kiburi cha uwongo - kiburi bila msingi. (false pride) Lakini - Scarlet pia inaonyesha wazi zaidi karibu na makalio ya wanawake hao ambao huuza "upendo" kwa sarafu za dola! Hakika wao ni "Wanawake Wekundu!"

(Scarlet Women)Wanawake kama hao huwa hawapendi kabisa tendo la ngono kwa kweli; kwao ni njia tu ya kujitafutia riziki. Kwa hivyo, mtu mwenye majivuno kupita kiasi na kahaba hushiriki rangi sawa katika aura. Inafaa kufikiria kwamba misemo hii ya zamani, kama vile "mwanamke mwekundu," "hali ya bluu,"(blue mood) "hasira nyekundu," (red rage)"mweusi kwa hasira" ( black with temper)na "kijani kwa wivu(green with envy)" kwa kweli huonyesha kwa usahihi hali ya mtu anayepatwa na ugonjwa kama huo. Watu ambao walianzisha misemo kama hiyo ni wazi kwa uangalifu au bila kujua waliona aura.

Bado tunaendelea na kikundi "nyekundu" - pink ( kwa kweli zaidi no Kama matumbawe(coral), ) inaonyesha kutokomaa. Vijana (teenagers)huonyesha waridi (pink)kuliko nyekundu yoyote. Katika hali ya mtu mzima, pink ni kiashiria cha utoto na ukosefu wa usalama. Nyekundu-kahawia, kitu kama ini bichi, inaonyesha mtu mbaya sana(nasty person). Mtu anayepaswa kuepukwa, kwa maana ataleta shida. Inapoonekana juu ya kiungo inaonyesha kwamba kiungo hicho ni kigonjwa sana na mtu ambaye ana rangi kama hiyo juu ya kiungo muhimu atakufa hivi karibuni.

Watu wote walio na RED inayoonyesha mwisho wa mfupa wa kifua (mwisho wa sternum) wana shida ya neva. Wanapaswa kujifunza kudhibiti shughuli zao na kuishi kwa utulivu zaidi ikiwa wanataka kuishi kwa muda mrefu na kwa furaha.

ORANGE. RANGI YA MACHUNGWA. Chungwa kwa kweli ni tawi la rangi nyekundu, lakini tunaipa heshima ya kuipa uainishaji wake kwa sababu baadhi ya dini za Mashariki ya Mbali zilikuwa zikiona rangi ya orange kama rangi ya jua na kuisujudu. Ndiyo maana kuna rangi nyingi za machungwa katika Mashariki ya Mbali. Kwa upande mwingine, ili tu kuonyesha pande mbili za sarafu, bado dini nyingine ziliamini kwamba rangi ya bluu ndiyo rangi ya jua. Haijalishi una maoni gani, rangi ya chungwa kimsingi ni rangi nzuri, na watu walio na kivuli cha machungwa(shade of orange) kinachofaa katika aura yao ni wale wanaozingatia sana watu wengine, ni wafadhili wa kibinadamu, (philanthropist)watu wanaojitahidi kusaidia wengine ambao hawajabahatika. Rangi ya manjano-machungwa inapaswa kutamanika kwa sababu inaonyesha kujidhibiti(self control), na ina fadhila(virtue) nyingi.
 
Back
Top Bottom