Rangi nyeusi si rangi ya asili ya binadamu

Rangi nyeusi si rangi ya asili ya binadamu

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,764
Reaction score
20,903
Rangi hii imetokea tu maishani sababu ya mazingira yanayochochea kuzalishwa Melanin kwa wingi.

Rangi asili ya binadamu ni nyeupe. Kisayansi binadamu tunashare ancestor na sokwe mtu. Ukiangalia vizuri sokwe mtu chini ya manyoya yake ni mweupe.

Pia jamii za watu wa kale zaidi duniani kama wale wabushmen wa kalahari ni weupe.

Hii rangi nyeusi siyo rangi asili ya binadamu.
 
Kama ni melanini ndio imezalishwa basi watoto wangekuwa wanazaliwa weupe kama wazungu kisha jua linazalisha melanini na kuwa black, cha kushangaza wazungu wakija Afrika hata wakikaa miaka mia wanakuwa na rangi yao ya uzungu ile ile. Kinachobadilika ni kufubaa au kung'aa kwa ngozi.
 
BIBLIA:
Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.

6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
 
Kama ni melanini ndio imezalishwa basi watoto wangekuwa wanazaliwa weupe kama wazungu kisha jua linazalisha melanini na kuwa black,cha kushangaza wazungu wakija afrika hata wakikaa miaka mia wanakuwa na rangi yao ya uzungu ile ile....Kinachobadilika ni kufubaa au kung'aa kwa ngozi.
Mazingira huwa yanabadilisha genes za watu. Kitendo hiki huchukua miaka mingi sana. Kwa hiyo waafrika tunazaa watoto weusi sababu tayari genes zetu zimebadilika.
 
Unataka kusema ma albino ndo most perfect human beings due to excessive lack of melanin?as long as melanin Is concern
Sema hawa wanakosa melanini kila sehemu hadi kwenye nywele. Kisayansi ancestors wetu walikuwa weupe ndani ila walifunikwa na manyoya meusi kama walivyo sokwe leo. Hata wazungu utakuta wana vinyweleo vyeusi. Ualbino ni tatizo.
 
Mimi kwetu weupe pee kuliko hata hao wazungu, ila still kuna nchi Ulaya mashariki walinirushia ndizi nikisubiri train
 
Back
Top Bottom