real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,303
- Katika ajali iliyotokea Mei, 2017 eneo la Rhotia Marera huko Karatu, wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja walipoteza maisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Mvutano umeibuka ndani ya Umoja wa Watanzania wanaoishi nje, unaoitwa Tanzania Global Diaspora Council kuhusiana na fedha za rambirambi za vifo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Lucky Vicent.
Katika ajali iliyotokea Mei, 2017 eneo la Rhotia Marera huko Karatu, wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja walipoteza maisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Barua na maandiko mbalimbali ya Watanzania hao ambayo gazeti hili inayo, inadai kuwa fedha zilizochangwa zilikuwa ni Sh2.4 milioni lakini wakajulishwa zilizochangwa ni Sh1.7 milioni.
Barua hiyo inadai kuwa baada ya gazeti hili kumtumia ujumbe wa WhatsApp kiongozi anayetuhumiwa ili atoe ufafanuzi, hakutoa ufafanuzi badala yake akafanya mipango ya haraka haraka kukabidhi fedha hizo.
Bila kuwashirikisha viongozi wenzake, inadaiwa kiongozi huyo alimteua mwandishi mmoja wa habari wa Tanzania amtumie Sh1.75 milioni pekee, ili amsaidie kukabidhi kwa uongozi wa Serikali Arusha.
Hata hivyo, kupitia kundi rasmi la Wanadiaspora, wanachama walichachamaa wakidai nyaraka walizonazo zinaonyesha kiasi halisi kilichochangwa ni Sh2.4 milioni na siyo Sh1.7 milioni.
“Baada ya kubanwa sana amekubali, kulipa hiyo tofauti. Tunachofanya sasa tunawasiliana na uongozi wa Serikali Arusha kujua kama wamezipokea. Kesho (leo) tutapata majibu,” kilidai chanzo kimoja.
Katika moja andiko lake katika kundi hilo baada ya kubanwa, kiongozi huyo aliandika: “Hiyo tofauti iliyopo ya Sh719,846 nitaitoa mwenyewe kwa kuwa nilikubali kubeba dhamana hiyo.”
Chanzo: Mwananchi