Waandishi Mwanza wazua mgogoro wa aibu fedha za rambirambi za waandishi 5 waliofariki kwenye ajali

MtuHabari

JF-Expert Member
Oct 16, 2020
321
1,019
Majuzi kulitokea ajali mbaya sana iliyo tuhuzunisha sana wana habari na Watanzania wote ambapo watu 14 wakiwamo waandishi 5 walipoteza maisha hapo hapo na kuacha majeruhi kadhaa ambao wengine nasikia bado wanauguza majeraha.

Jambo la ajabu huko Mwanza umezuka mgogoro wa fedha za rambirambi zilizochangwa na watu wema na taasisi mbalimbali ambapo waliamua kuitumia MPC (chama cha Waandishi) kama centre ya kuratibu michango lakini ikataka kujigeuza kama mmiliki wa michango hiyo ilihali hata mchango wenyewe haikutoa.

Shida hiyo iliyo leta mizozo kwa habari nilizoletewa ni Mwenyekiti wa MPC bwana Edward Soko, ambaye kama kawaida yake ndiye chanzo kikuu cha kila aina ya tafrani kwa kusimamia maslahi yake binafsi.

Hii niaibu kubwa kuleta mzozo wa fedha za rambirambi wakati hata bado waandishi hawajasahau msiba huo mzito uliowapata.

Ugawaji wa fedha hizo waandishi waliusimamia vyema kabisa ila yeye kalianzisha kwa kuona hakushirikishwa.
Nakumbuka niliwaasa Waandishi wenzangu wakati ule anafanya lobbying ili achaguliwe kuwa Rais wa UTPC kuwa anaenda kusababisha migogoro nchi nzima kwa waandishi kwa "ujuaji" wake. Nashukuru nilieleweka, ila sasa niwaombe walio karibu naye na wale wapambe wake wamuonye aache hili suala la kutamani rambirambi atavuruga watu wakati huu wa msiba huo mzito.

HIVI NDIO ALIANZISHA KWA KUTOA UJUMBE HUU;

Taarifa kwa wanachama juu ya ugawaji wa fedha za rambirambi*

Ndugu wanachama, jioni ya leo nimeulizwa mara kwa mara juu ya zoezi la ugawaji wa fedha za rambirambi zilizofanyika leo pale ofisi za TBC.

Naomba nijibu suala hili kuwa ni sawa fedha zimegawanywa leo.

Ndugu wanachama km mjuavyo klabu yetu ilihusika kuratibu ukusanyaji wa rambirambi toka kwa wadau, na rambirambi hizo zilitoka kwenye makundi mawili

1.Michango ya waandishi mmoja mmoja au mdau mmoja mmoja

2.Michango ya taasisi
Hii tulipokea toka TEF, MCT, press clubs na AZAM TV

Pia kwa kuwa sisi ndio tulikuwa taasisi kiongozi kwenye msiba huu nilitoa agizoi la akaunti za klabu zitumike katika kukusanya michango, akaunti yetu ya benki ya EXIM ilitumika na pia M PESA yetu ya klabu iliyosomeka kwa jina la Mwanza Press Club zilitumika.

Leo Majira ya saa 5.00 asubuhi nilipokea simu toka kwa mjumbe mmoja kuwa niende Ofisi za TBC ili tukagawe hizo fedha.

Hapo niliwaelekeza wana kamati nikiwa km Mwenyekiti wa hiyo kamati kuwa, zoezi hilo lisifanyike leo na badala yake lifanyike kesho ili maandalizi ya kikao cha kukabidhi fedha yafanyike ikiwemo kuandaa ajenda za kikao hicho km taratibu za ofisi zinavyotaka.

Na baadaye nilifanikiwa kuwapata wahusika waliokuwa wanakusanya fedha na kuwashauri wasitoe pesa .

Lakini kwa bahati mbaya fedha zilitewa toka kwenye akaunti zetu zote mbili yani M PESA na EXIM Bank bila katibu kujua wala Mwenyekiti na zoezi liliemdelea.

Baada ya kuona hivyo niliishauri basi wao wanakamati wanaotaka kugawa fedha basi km watafanya hivyo zile pesa tulizokabidhiwa km Taasisi toka kwa taasisi marafiki wasigawe, lakini niliniambia wameshapanga kuzigawa wao.

Ndugu wanachama taasisi ina mifumo yake ya kiuongozi na usimamiaji wa taasisi.

Kwa ufupi MPC ina uongozi na kama kamati tendaji ndio chombo cha maamuzi ya juu kwa niaba ya wanachama, hivyo nimeitisha kikao cha kamati tendaji kesho saa 6.00 kujua utaratibu uliotumika kutoa fedha benk na kwenye M PESA km ulifuata mifumo yetu ya klabu kwenye kutoa fedha pamoja taratibu za taasisi

Naomba sana wanachama kuweni na subira wakati tunalishughulikia jambo hili, mimi ndiye Mwenyekiti wetu nitasimamia taratibu za kikatiba

Ahsanteni sana
Edwin Soko
Mwenyekiti
 
Mpak sasa imepatikana sh ngap tuanzie hapa Kwanza...mana pesa ni taasis inayojitegemea , haina ndug , rafk wala dini
Habari nilizonazo ni kuwa fedha ni chini kidogo ya milioni 10. Waandishi wengi pamoja na uwezo wao mdogo wa kimapato ndio waliojichangisha changisha.
Serikali ambayo ndio ilikuwa imeratibu safari hiyo ya kikazi kupitia ofisi ya Waziri mkuu ikatoa shs 2m huku ikimgharamia waziri Nape mamilioni kusafiri kwenda msibani. Si bora hizo gharama za safari wangeongezea mchango na serikali ikawakilishwa na RC tuu?
Waandishi sijui lini tutawekwa daraja tunalostahili.
 
Kwani kijani hawajatoa chochote maana mnavyo jipendekezaga kuripoti taarifa Yao wanatakiwa watoe milioni20
 
Majuzi kulitokea ajali mbaya sana iliyo tuhuzunisha sana wana habari na Watanzania wote ambapo watu 14 wakiwamo waandishi 5 walipoteza maisha hapo hapo na kuacha majeruhi kadhaa ambao wengine nasikia bado wanauguza majeraha.

Jambo la ajabu huko Mwanza umezuka mgogoro wa fedha za rambirambi zilizochangwa na watu wema na taasisi mbalimbali ambapo waliamua kuitumia MPC (chama cha Waandishi) kama centre ya kuratibu michango lakini ikataka kujigeuza kama mmiliki wa michango hiyo ilihali hata mchango wenyewe haikutoa.

Shida hiyo iliyo leta mizozo kwa habari nilizoletewa ni Mwenyekiti wa MPC bwana Edward Soko, ambaye kama kawaida yake ndiye chanzo kikuu cha kila aina ya tafrani kwa kusimamia maslahi yake binafsi.

Hii niaibu kubwa kuleta mzozo wa fedha za rambirambi wakati hata bado waandishi hawajasahau msiba huo mzito uliowapata.

Ugawaji wa fedha hizo waandishi waliusimamia vyema kabisa ila yeye kalianzisha kwa kuona hakushirikishwa.
Nakumbuka niliwaasa Waandishi wenzangu wakati ule anafanya lobbying ili achaguliwe kuwa Rais wa UTPC kuwa anaenda kusababisha migogoro nchi nzima kwa waandishi kwa "ujuaji" wake. Nashukuru nilieleweka, ila sasa niwaombe walio karibu naye na wale wapambe wake wamuonye aache hili suala la kutamani rambirambi atavuruga watu wakati huu wa msiba huo mzito.

HIVI NDIO ALIANZISHA KWA KUTOA UJUMBE HUU;

Taarifa kwa wanachama juu ya ugawaji wa fedha za rambirambi*

Ndugu wanachama, jioni ya leo nimeulizwa mara kwa mara juu ya zoezi la ugawaji wa fedha za rambirambi zilizofanyika leo pale ofisi za TBC.

Naomba nijibu suala hili kuwa ni sawa fedha zimegawanywa leo.

Ndugu wanachama km mjuavyo klabu yetu ilihusika kuratibu ukusanyaji wa rambirambi toka kwa wadau, na rambirambi hizo zilitoka kwenye makundi mawili

1.Michango ya waandishi mmoja mmoja au mdau mmoja mmoja

2.Michango ya taasisi
Hii tulipokea toka TEF, MCT, press clubs na AZAM TV

Pia kwa kuwa sisi ndio tulikuwa taasisi kiongozi kwenye msiba huu nilitoa agizoi la akaunti za klabu zitumike katika kukusanya michango, akaunti yetu ya benki ya EXIM ilitumika na pia M PESA yetu ya klabu iliyosomeka kwa jina la Mwanza Press Club zilitumika.

Leo Majira ya saa 5.00 asubuhi nilipokea simu toka kwa mjumbe mmoja kuwa niende Ofisi za TBC ili tukagawe hizo fedha.

Hapo niliwaelekeza wana kamati nikiwa km Mwenyekiti wa hiyo kamati kuwa, zoezi hilo lisifanyike leo na badala yake lifanyike kesho ili maandalizi ya kikao cha kukabidhi fedha yafanyike ikiwemo kuandaa ajenda za kikao hicho km taratibu za ofisi zinavyotaka.

Na baadaye nilifanikiwa kuwapata wahusika waliokuwa wanakusanya fedha na kuwashauri wasitoe pesa .

Lakini kwa bahati mbaya fedha zilitewa toka kwenye akaunti zetu zote mbili yani M PESA na EXIM Bank bila katibu kujua wala Mwenyekiti na zoezi liliemdelea.

Baada ya kuona hivyo niliishauri basi wao wanakamati wanaotaka kugawa fedha basi km watafanya hivyo zile pesa tulizokabidhiwa km Taasisi toka kwa taasisi marafiki wasigawe, lakini niliniambia wameshapanga kuzigawa wao.

Ndugu wanachama taasisi ina mifumo yake ya kiuongozi na usimamiaji wa taasisi.

Kwa ufupi MPC ina uongozi na kama kamati tendaji ndio chombo cha maamuzi ya juu kwa niaba ya wanachama, hivyo nimeitisha kikao cha kamati tendaji kesho saa 6.00 kujua utaratibu uliotumika kutoa fedha benk na kwenye M PESA km ulifuata mifumo yetu ya klabu kwenye kutoa fedha pamoja taratibu za taasisi

Naomba sana wanachama kuweni na subira wakati tunalishughulikia jambo hili, mimi ndiye Mwenyekiti wetu nitasimamia taratibu za kikatiba

Ahsanteni sana
Edwin Soko
Mwenyekiti
Mtoa habari nawewe ufe ili ufaidike na hu mgawo!!!
 
Nimesoma habari yoote sijaona kiasi cha pesa kilichochangwa
 
Nilitaka kusomea journalism nikasita kumbe nilikuwa sahihi,hii ni kada iliyokosa heshima,hamna tofauti na bongo movie,tena bora bongo movie.shame on you .njaa zitawaua,mliharibu sana heshima yenu kwa kugeuka kikundi cha kusifu na kuabudu kipindi kile
 
Back
Top Bottom