Familia ya Ndesamburo yakabidhi milioni 3 ya rambirambi kwa wanafunzi wa Lucky Vincent

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
rambirambi+pic.jpg

Arusha. Familia ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshi Mjini marehemu, Phillemon Ndesamburo imekabidhi Sh3 milioni leo, ahadi ya rambirambi iliyotolewa na marehemu Ndesamburo kabla ya kufariki dunia.

Ndesamburo kabla ya kuaga dunia Mei 31 mwaka jana aliahidi kutoa rambirambi kwa ajili ya wahanga wa tukio la ajali ya basi lililoua wanafunzi pamoja na watumishi wa shule ya Lucky Vincent.

Lakini kabla ya kutimiza ahadi yake aliaga dunia baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake mjini Moshi.

Tukio la kukabidhi rambirambi hiyo liliendana na zoezi la kutembelea mnara wa kumbukumbu wa wanafunzi 32, walimu wawili pamoja na dereva mmoja waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea mwaka jana eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi rambirambi mtoto wa marehemu, Rita Thadey amesema familia imekabidhi kiasi hicho cha fedha kama ahadi iliyoachwa na marehemu baba yao kabla mauti hayajamkuta.

“Sisi kama familia tumejisikia faraja sana kutimiza ahadi iliyoachwa na marehemu baba yetu ni hilo tu,”amesema Rita

Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema kwamba marehemu Ndesamburo siku chache kabla ya kuaga dunia alimpigia simu na kumwita nyumbani kwake ili akumkabidhi rambirambi na alipomfuata nyumbani hali yake ilibadilika ghafla kabla ya kuaga dunia.

Lazaro amesema Ndesamburo amefariki akiwa mikononi mwake lakini anajisikia faraja mara baada ya familia ya marehemu kuhakikisha wanatimiza ndoto na ahadi yake.

“Ahadi hii ilikuwa niipokee mimi kwa kuwa marehemu aliniita nyumbani kwake anikabidhi rambirambi lakini nilipowasili hali yake ya afya ilibadilika ghafla na akafariki mikononi mwangu,” amesema Lazaro.

Chanzo: Mwananchi
 

Amanikullaya

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
1,108
2,000
R.I.P Mungu Amrehemu ampe pumziko,na watoto Mungu awabariki kw kumuenzi mzee wao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom