Suala ni kuwa na ramani ya dunia ambayo ina ukubwa halisi wa bara la Afrika na nyingine pia.
Ramani inayotumika kwa sasa ilitengenezwa karne ya 16, inaonyesha nchi zilizo karibu na Ikweta kuwa na ukubwa mdogo wakati zile zilizoko kwenye ncha ya kaskazini na kuzini zikionekana kubwa zaidi, Mfano: Greenland inaonekana kuwa na ukubwa sawa na bara la Afrika ingawa Afrika ni kubwa mara 14 kuliko Greenland.