Ramadhan Mbwaduke ndio mchambuzi wangu bora kwa upande wa Tv

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,968
6,137
Huyu jamaa ukimsikiliza kwa makini utagundua ana madini mengi sana.

Anachambua mpira kwa data, uhalisia na ukweli. Huwa namfatilia sana kila jumapili pale AzamTv kupitia kipindi cha Sports AM chini ya Mahamoud Bin Zubery.

Haya yaliyotokea jana kwa Simba, Azam na Yanga alishayaongea toka ratiba imepangwa.

Aliichambua game ya kwanza ya Yanga dhidi ya Al Hilal kidha akachambua game ya marudiano itakavyokuwa namna Al Hilal performance yao wakiwa nyumbani, rekodi ya mechi zao nk.

Jamaa hana mihemko, utamchukia bure lakini ndio ukweli atakuchambulia kuhusu timu yako.

Hongera sana Mbwaduke, naona kwasasa umechukua nafasi ya Ali Mayai kwenye uchambuzi wa mechi za NBC PL piga kazi kaka!
 
Nilikuwa nataka kuanziasha Uzi kumhusu..nikaona ngoja niangalie kama upo Uzi kabla..nimeukuta huu..
Jamaa yuko vizuri kwani anachambua kwa kutimia Data..Hana mihemko kama ya wachambuzi wengine uchwara.
 
Jamaa kwa takwimu tu yuko vizuri. Mpaka hua nawaza pengine zimeandikwa mbele yake ndio anazisoma. Siku moja alikua akitaja umri wa kikosi chote cha Horoya mmoja mmoja mpaka walioko benchi nikawa nami nahakikisha ni mule mule.

Anakupa strength na weakness ya timu sahihi kabisa. Pengine angekua hata kwe benchi la ufundi la timu kama ya Taifa awe mshauri tu. Naangaliaga Sport AM kwa ajili yake.

Nje ya mada,
Atoke kwenye Magazeti ya Uhuru na Mzalendo yanayosomwa pale Lumumba tu akatafute changamoto zingine kwengine.
 
Shida aliyonayo Mbwaduke ni mwoga katika kukosoa madhaifu ya timu au mchezaji mmojammoja na ilo ndio eneo muhimu ki uchambuzi Kwa mchezaji au timu kujirekebisha.
Katika Eneo ilo Edo Kumwembe yupo vizuri.
 
Mbwaduke hata yeye huwa unajua kabisa kuwa hapendi kuwa wazi kwenye madhaifu nadhani inachangiwa na kariba yake Kuna watu hawapendi kuongelea madhaifu sana ya watu wengine
Ila kwa uchambuzi na utulivu jamaa yuko vizuri na huwa ana utulivu kwenye kuelezea kitu
 
Yanga mkubwa huyo jamaa na uchambuzi wake upo biased sana yaani hata ukimsikiliza tu kwa mara ya kwanza unajua huyu ni uto
 
Jamaa yupo vizuri Sana hasa kitakwimu. Yupo tofauti Sana na wachambuzi wa michongo wanaochambua baada ya matotekeo . Namakubali Sana Ramadhani Mbwanuke binafsi ni mfuatiaji wa kipindi Cha sport am
 
Back
Top Bottom