DullyJr
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 13,979
- 11,816
Yanga wana kikosi kizuri sana cha kushindana ligi ya ndani hilo halina ubishi, lipo dhahiri shahiri wala hatupingi ila kuna tatizo mahali kwenye michuano ya kimataifa.
Mfano Simba walienda kambi nchini Misri wakapata mechi nzuri za kiushindani sana, ambazo 60% ya timu hizo ndio unakutana nazo kwenye michuano hii.
Walipotoka kule wakaenda Sudan baada ya ligi kusimama, wakapata mechi na Al Hilal na Asante Kotoko ya Ghana zote hizo ni michezo migumu, wamegusa Afrika Magharibi na Afrika ya Kati.
Wachezaji wameingiza kitu mpaka hapo! Hata ligi iliposimama Simba wakaenda Zanzibar wakapata tena mechi nzuri mpaka na Kipanga ambaye ametoa sare na Club Africain ya Tunisia , vuta picha hapo.
Kifupi ni kuwa kila wakipata upenyo wao wanatoka kwenda kupata mechi za kipimo sahihi kuendana na kasi za kimataifa, wachezaji hawapati presha kwakuwa wamezoea mechi kubwa.
Tofauti na Yanga, timu hii kusafiri nje ya nchi ilikuwa Morocco ambapo wakarejea mapema, mara ya mwisho walienda Nigeria wakafungwa na Rivers hawajawahi kusafiri tena, they need competitive games.
Kocha Mwinyi Zahera amesema kitu kikubwa sana kuwa wachezaji wao wana presha sana, hawapo sawa kwakuwa mechi nzito na za kiushindani kama hizi hawajakutana nazo kama timu, presha ipo juu.
Kama dhamira ni kufanya vyema kimataifa basi tukubali kuwa hizi mechi dhidi ya Mbuni na Friends Rangers pale AVIC TOWN haziwezi kutusaidia, mnapaswa kupata mechi kweli kweli ili kufanya vyema kimataifa.
Chochote ambacho Yanga watakifanya kimataifa kwangu ni bonus tu ila timu kama timu bado haijapata test sahihi ya kufanya makubwa kimataifa, sad truth.
"Simba and Yanga are equal but not the same", wanafanana ila hawapo sawa.
VISIT MOROGORO