Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 521
- 827
Lissu amesema kuwa amekutana na shahidi wake, Ramdhan Kingai, mahakamani baada ya kuitikia wito wa Mahakama, ambapo alizungumza naye kuhusu maeneo ambayo anaweza kuyatolea ushahidi.
Lissu amesema kuwa Kingai amemweleza kwamba hawezi kuwa shahidi wake na kwamba hayuko tayari kufika kizimbani kutoa ushahidi kwa niaba ya mshtakiwa. Kwa mujibu wa Lissu, Kingai amemwambia kuwa yuko upande ambao utafurahia Lissu kukutwa na hatia.
Lissu pia ameeleza kuwa Kingai amemwambia kwamba mashahidi wengine wawili, ambao ni Mkuu wa Majeshi na Mkuu wa Jeshi la Polisi, nao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi kwa kuwa watakuwa upande wa mashitaka.
Kufuatia maelezo hayo Lissu ameiomba Mahakama kufunga ushahidi akidai kuwa hana mashahidi wengine.
Upande wa Jamhuri pamoja na mshtakiwa wanatarajiwa kufanya mawasilisho ya hoja za mwisho katika shauri la uhaini siku ya Jumatano September 23, 2026 kabla ya kupangwa kwa terehe ya uamuzi.
Lissu amesema kuwa atajitahidi kuandaa hoja za Majumuisho ya Mwisho (Final Submission) hadi kufikia siku ya Jumatano licha ya kuwa muda ni mfupi. Jamhuri pia nao wamesema kuwa watajitahidi kuwa wamekamilisha hadi kufikia siku hiyo.
Hata hivyo Jamhuri wameeleza Kupitia wa Wakili Katuga kuwa wamepokea kwa masikitiko taarifa ya mashahidi wa Lissu kufika mahakamani kutoa ushahidi.