Raisi Obama na Maswali ya waandishi

Gosheni

Senior Member
Oct 28, 2008
199
138
Ikiwa mara ya kwanza tangu awe raisi wa taifa kubwa kiumbo, kubwa kiuchumi kuliko zote dunia, kubwa kijeshi, raisi Obama jana alihutbia press conference. katika press conference hiyo Obama alizungumzia kuhusu umuhimu wa nchi ya marekani kuangalia njia mbadala wa matumizi ya nishati nyingine tofauti na hii iliyopo sasa, kwa kufanya hivyo itapunguza gharama za maisha, na pia kutengeneza ajira mpya namba nimesahau, vilevile kusaidia kuhusiana na maswala ya mazingira, ukizingatia mambo ya ozone layer.

Cha ajabu, waandishi walizoea baada ya hotuba kinachofuata ni maswali, badala yake mjamaa, alikwenda akasaini vitabu vitatu, waheshimiwa mtatueleza vinahusiana na nini.

Swali jee! kunauwezekano Obama ameanza mambo ya viongozi wa Afrika hivyo kukimbia maswali, kwani iwapo angeruhusu maswali, kunauwezekano wangembana, hivyo kuonyesha uzaifu wa mpango huo. sababu mradi huu yeye siyo wa kwanza kuzungumzia, kwani tangu miaka ya 70's raisi Richard Nixon alikuwa mtu wa kwanza kuzungumzia hilo hivyo kufuata maraisi wote wa marekani, na hakuna hata mmoja ambaye ameisha wahi kutekeleza.

Naomba kuwakilisha
 
obama ni wetu tu ngozi nyeusi bwana hata kama atakimbia maswali anawasaidizi wenye akili waliokwenda shule wakaelewa tunakula ili tuishi na sio tunaishi ili tule kama mijiviongozi ya tanzania mifisadi.
 
Maswali yalijibiwa na yule msemaji wa white house. Ile ya Obama nilivyoelewa ni ilikua kuweka sheria mpya za lobbyst na kufreez salary za white house employees making over $100,000. Au labda tunaongelea tukio tofauti?
 
Mimi sioni tofauti kumbwa kati ya obama na jk. Kikwete tulimtegemea sana kwa ahadi zake lakini leo tumeanza kujuta, same case kwa wamarekani wanamtegemea kwa makuu mno bwana obama lakini mwisho wa yote itakuwa aibu, na hilo ndio litakuwa anguko kubwa la mtu mweusi duniani
 
Mimi sioni tofauti kumbwa kati ya obama na jk. Kikwete tulimtegemea sana kwa ahadi zake lakini leo tumeanza kujuta, same case kwa wamarekani wanamtegemea kwa makuu mno bwana obama lakini mwisho wa yote itakuwa aibu, na hilo ndio litakuwa anguko kubwa la mtu mweusi duniani
KITUKO UNALETA VITUKO!! Unasema huoni tofauti kati ya Obama na JK ??
Naomba nitumie nafasi hii kukushangaa mkuu.
 
Back
Top Bottom