Raisi Mstaafu Arudia Kazi yake ya Ualimu

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,146
13,216
12439104_1098291083526236_6643654311973425208_n.jpg
 

Attachments

  • 12439104_1098291083526236_6643654311973425208_n.jpg
    12439104_1098291083526236_6643654311973425208_n.jpg
    19.2 KB · Views: 33
Hiz nchi watu wanaoshi vizur sana ..

Huyu mphd wa Morogoro anaogopa nini kurudi kufundisha kama mwenzie, sababu kama kazi yake kabla ilikuwa kufundisha ni vema na haki kuitendea haki taaluma yake.
 
Alaa !! vipi huyu nae? hachukui pipa nae asafiri kama wastaafu wenzie?????!!!
JK azidi kupasua anga Ulaya
BY JOSEPH MWENDAPOLE
27th March 2016
sv.png

Rais mstaafu Jakaya Kikwete
Wakati Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiendelea kusafiri kwenda mataifa mbalimbali kwa shughuli za kikazi na kufikisha nchi 10 alizokwisha tembelea, Rais John Magufuli leo ametimiza siku ya 143 tangu aapishwe kuingia Ikulu bila kukwea ndege kwenda ughaibuni.


Hiyo inaweza kuwa rekodi ya aina yake kwa kuwa haijawahi kutokea tangu Uhuru kwa Rais mstaafu kusafiri safari nyingi za nje ya nchi kushinda Rais aliyeko madarakani.

Hadi sasa, Rais John Magufuli ametumia siku zote za kuwa kwake madarakani kusimamia kampeni yake ya kuongeza mapato ya serikali na kukomesha vitendo vya ufisadi kupitia kile anachokiita ‘kutumbua majipu’.

Mbali na mataifa mbalimbali aliyokwishatembelea, rekodi zinaonyesha kuwa Machi 21 mwaka huu, Kikwete alikwenda nchini Tunisia kwenye mkutano wa nane wa nchi majirani na Libya ambapo yeye ni mwakilishi maalum wa Afrika wa usuluhishi wa mgogoro wa taifa hilo.

Kabla ya kwenda Tunisia, Kikwete alikuwa katika mji wa Salalah nchini Oman alikoshiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya na alishindwa kuhudhuria kuapishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Shein kutokana na kuwa nje ya nchi.

Katika mkutano wake na viongozi wa Libya, Kikwete alisisitiza kuwa suluhisho la kudumu la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.
Juzi Rais huyo mstaafu aliwasili Dubai akitokea Tunisia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kwa shughuli hizo hizo za upatanishi wa mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Libya.


 
Maisha kama haya Miviongozi mingi ya Africa inayatamani lakini haijiamini. Ahmed Nejad alikuwa Rais "chizi" anaejiamini sana.
 
Huyu mphd wa Morogoro anaogopa nini kurudi kufundisha kama mwenzie, sababu kama kazi yake kabla ilikuwa kufundisha ni vema na haki kuitendea haki taaluma yake.
GPA
Haisomi mkuu.si unajua uDr. wenyewe kaupatia Vaal University
 
Walimu wenyewe wanatamani kuacha ualimu waingie kwenye siasa!! sembuse kurudia ualimu.
 
Huyu mphd wa Morogoro anaogopa nini kurudi kufundisha kama mwenzie, sababu kama kazi yake kabla ilikuwa kufundisha ni vema na haki kuitendea haki taaluma yake.
Dr. Rutengwe alikuwa ofisa wizara ya kilimo, hajawahi fundisha huyo
 
Back
Top Bottom