Vyamavingi
JF-Expert Member
- Oct 3, 2014
- 5,803
- 5,518
Mpendwa Rais, narejea kauli yako ya wiki iliyopita wakati ukifungua hosteli za wanafunzi pale UDsm, ulipoitaka TCU kuacha kuwapangia wanafunzi vyuo vya kusoma. Hadi sasa sijaelewa kama ulikuwa na maana hiyo au ulimaanisha vinginevyo.
Nijuavyo, TCU haiwapangiii wanafunzi vyuo vya kujiunga zaidi ya kuratibu ili kila mwanafunzi ajiunge na chuo anachotaka lkn kwa kuwa baadhi ya kozi ktk baadhi ya vyuo hujaa mapema TCU wanamsaidia mwombaji kwenda chuo kingine
. Hii haina tofauti na kujaza fomu za kujiunga na Sekondari kwa wanaomaliza darasa la saba. Enzi zetu tulijaza machaguo 3, unapokosa nafasi kwa chaguo la kwanza unapelekwa chaguo la pili hadi la tatu. Sasa iwapo mwanafunzi atajaza chaguo moja tu na akakosa itakuwaje wakati amefaulu kwa alama za kujiunga na kidato cha 1? Hivyo ndivyo wanavyofanya TCU kupitia mfumo wa Central Admission System (CAS) , wanarahisisha sana udahili na kupunguza gharama kwa mwombaji kwa kiasi kikubwa.
Zamani wakati tukiwa na vyuo vichache vya serikali tu wakati waombaji wakiomba moja kwa moja baadhi yao walikuwa wanachaguliwa kujiunga na vyuo viwili hadi vitatu na kusababisha waombaji wengine wakose nafasi. Nina ndugu yangu alichaguliwa kujiunga na IDM Mzumbe na UDsm kwa wakati mmoja. Alikwenda kusoma IDM kwa mwezi mzima lkn baadaye mwaka huohuo akaacha na kwenda UDsm kusoma kozi aliyochaguliwa huko ya Uhandisi badala ya Uhasibu aliyochaguliwa IDM. Sasa kwa namna ile si alizuia nafasi ya mtu mwingine pale IDM?
Mheshimiwa Rais, TCU ina umuhimu mkubwa, na ukweli ni kuwa wanafunzi wa sasa wanapata upendeleo mkubwa kuoutia TCU tofauti na sisi tuliosoma nyakati zile. Kupitia TCU mwombaji aliyekosa nafasi mara ya kwanza, anapata nafasi ya kujua ni chuo gani bado kina nafasi na kwa kozi gani. Hapo mwombaji anapewa fursa ya kuamua kuomba Chuo hicho kwa kozi zilizo wazi au kuamua kusubiri mwaka unaofuata.
Kwa kifupi wanachofanya TCU sio kumlazimisha mwombaji kwenda chuo asichotaka bali kumshauri.
Ikumbukwe pia hakuna chuo kinachoweza kudahili wanafunzi wote wenye sifa, wanafunzi wengi wangependa kujiunga na vyuo vilivyopo Dar na vile vya serikali kwa kuwa ada zake ziko chini kuliko vyuo binafsi. Pia kupitia CAS- TCU mwombaji anakuwa na uhakika wa udahili kwani anapata nafasi ya kufahamishwa kuwa ombi lake limefikishwa, litashughulikiwa na atapewa nafasi ya kuchagua chuo na kozi mbadala ikiwa hatapata udahili ktk awamu ya kwanza.
Wakatabahu,
Vv