Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimesikia kauli za baadhi ya wanasiasa hapa nchini wakisema eti Rais Magufuli ni dikteta. Hoja wanazotoa wanasema eti ni kutokana na Jeshi la Polisi kuzima maandamano, makongamano ya vyama vya upinzani na kuzuia mikutano yote ya kisiasa kutokana na taarifa za kiintelijensia kuonesha kuwa hali si shwari. Wapiga zumari hao kwa ujumla wanasema kuwa eti Rais Magufuli anaminya demokrasia ya wanasiasa.
Ukiondoa hao wapinzani ambao inafahamika wazi kuwa hali yao kwa sasa si nzuri kutokana na kudhibitiwa kule Bungeni ambapo Naibu Spika amekuwa mwiba kwao kwa kusimamia ipasavyo kanuni, wapo wanaharakati ambao kwa kweli wanashangaza sana. Mmoja wa wanaharakati hao ni huyu anayejulikana kwa jina la Jenerali Ulimwengu.
Nasema kuwa kamtukana kwa sababu sababu za mkwamo wa Katiba Mpya zinajulikana. Kwamba wapinzani walisusia mijadala ya Bunge Maalum la Katiba na ndiyo iliyozaa UKAWA. Hata hivyo, tuweke kumbukumbu sawa kuwa licha ya UKAWA kujiondoa kwenye Bunge hilo, mjadala uliendelea na hatua iliyofikiwa ni kuandaliwa kwa Katiba Pendekezwa ambayo ilipaswa kupigiwa kura na wananchi ili iwe Katiba Mpya. Hata hivyo, kwa vile muda ulikuwa mfupi, mchakato huo ukaahirishwa ili kupisha Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.
Labda nimuulize Jenerali Ulimwengu, hivi sasa wabunge wa upinzani wamesusia mijadala ya Bunge la Bajeti kwa madai eti hawamtaki Naibu Spika. Je ina maana mchakato huo umekwama? Mbona wabunhe waliopo wanaendelea na majadiliano na bajeti inapitishwa?
Kwa hali hiyo, inashangaza kuona mpuuzi mmoja, mtu ambaye hapendi kuona nchi hii ikiwa na utulivu anamshambulia Kikwete kwa makosa ambayo hayaeleweki. Mpuuzi kama huyu ambaye anajua kabisa nini kilifanyika ila kwa kujitoa kwake ufahamu anaamua kuuhadaa umma kuwa fedha zilitumika bure bila ya katiba mpya kupatikana. Huu ni upuuzi, ujinga na wendawazimu wa hali ya juu. Kosa la Kikwete lipo wapi? Hasira za Ulimwengu kwa Kikwete zinatokana na nini? Ni mashtaka gani ambayo yanamkabili Kikwete mpaka astahili kushtakiwa? Kama ni chuki binafsi, kwa nini asimchukie Benjamin Mkapa ambapo wakati wa utawala wake Februari 2001 alitangazwa kuwa si Raia wa Tanzania?
Rais wangu Magufuli, inavyoonekana kuwa nchi hii kuna watu wanachezea sana na lengo lao ni amani tuliyonayo ivurugike, tuzichape ili wao wafurahi. Haiwezekani hata kidogo. Rais wangu Magufuli, umesingiziwa sana kuwa wewe ni dikteta. Ni wakati sasa wa kuonesha kuwa wewe si dikteta ila haupo tayari kuwaacha watukanaji wa viongozi, wachochea uvunjifu wa amani na wachonganishi kama akina Jenerali Ulimwengu, Zitto Kabwe na wengineo wa aina hiyo. Wakati ni sasa.