G. Activist
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 482
- 125
Rais Kikwete, miezi 2 iliyopita dagaa kilo moja ilikuwa tsh 3000, leo hii dagaa tsh6200.
Nina watoto 3 wanaosoma, siwezi kuwalisha. Nyama siwezi kununua, na hata dagaa siwei kununua kwa mshahara wa laki 250,000.
Nadhani umeshindwa kuongoza nchi kilichobaki ni sisi kuingia mitaani kukuondoa kama hautaki kuondoka mwenyewe. Siwezi kuendelea kuvumilia, kwa maana kama dagaa chakula cha masikini siwezi kukinunua ni nini sasa nitakachoweza kununua kuwalisha wanangu?
Niwalishe wanangu nini? Nilikupigia kura nikiamini kwamba ungeleta mabadiliko uliyoyaahidi...... baba ondoka, kwa maana umekiua chama chetu cha CCM, vinginevyo tunakwenda Chadema wamama wote
Pole sana ndugu, kumbe ulimpigia kura baada ya yote uliyoyaona kwa miaka yake mitano!!! Kweli watz tumefunikwa!!! Pole kaka, vumilia tu hivo hivo mpaka wakati wako uishe, sisi hatuwezi kukujoin wewe uliemfanikisha kufika alipo sasa.
Na aliekuwa akimpa ulinzi usio onekana ndo keshafariki hivyo mtaendelea kuona ya ajabu na hatari kuliko yaliyotokea na yanayotokea sasa.