Rais wangu Kikwete, siwezi kununua hata dagaa sasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wangu Kikwete, siwezi kununua hata dagaa sasa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Dec 6, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Rais Kikwete, miezi 2 iliyopita dagaa kilo moja ilikuwa tsh 3000, leo hii dagaa tsh6200.

  Nina watoto 3 wanaosoma, siwezi kuwalisha. Nyama siwezi kununua, na hata dagaa siwei kununua kwa mshahara wa laki 250,000.

  Nadhani umeshindwa kuongoza nchi kilichobaki ni sisi kuingia mitaani kukuondoa kama hautaki kuondoka mwenyewe. Siwezi kuendelea kuvumilia, kwa maana kama dagaa chakula cha masikini siwezi kukinunua ni nini sasa nitakachoweza kununua kuwalisha wanangu?

  Niwalishe wanangu nini? Nilikupigia kura nikiamini kwamba ungeleta mabadiliko uliyoyaahidi...... baba ondoka, kwa maana umekiua chama chetu cha CCM, vinginevyo tunakwenda Chadema wamama wote
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,589
  Likes Received: 1,956
  Trophy Points: 280
  Pole sana, utaambiwa "kasi mpya na hari mpya na nguvu mpya"!
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Umeongea vizuri ila nilipofika kwenye RED ndio umenichosha kabisa, sasa unamlalamikia Kikwete kwa lipi wakati wewe unapigiwa mdundiko na ukiwepo tshirt na kanga ulikuwa unajisikia raha? na bado mtauza mpaka miili yenu mwaka huu.

  JK oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, kanyaga twende baba mpaka wapate akili hawa Wadanganyika.
   
 4. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mrembo, hakuna haja ya kulia nyie ndo mliompigia huyo JK kura.
   
 5. U

  UNIQUE Senior Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukisema siasa haikuhusu adhabu yake ni kutawaliwa na wajinga kama sasa hivi. Wanaomfahamu walisema hawezi ikaonekani ni wivu. Haya ngoja muone! Huyu jk siyo kwamba ana roho mbaya bali uwezo wake kichwani ni mdogo sana. Si aende kupata tuition kwa kagame!
   
 6. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Dah, pole sana. Lakini najiuliza ikiwa utapataje hayo mavi ya kuwalisha wanao ikiwa ww mwenyewe huli?
   
 7. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Ongeza speed mkwerè mpaka wadanganyika wapate akili... Wasirudie tena!
   
 8. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Heri yako wewe unaelipwa huo mshahara. Wengine tunapata kima cha chini kabisa yani TSh.150,000 kwa mwezi. Any way pole sana vipi zile Tshirt za kijani ulizopewa wakati wa kampeni bado zipo??

   
 9. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  GDP inazidi kuongezeka. Inflation iliyoto ni temporarly tu. Wengine kwetu dagaa ni superior goods wakati wewe unanziona inferior! Kama ukishindwa kula dagaa...unaweza kushift kwenda kwenye mikate.
   
 10. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Go kikwete...mpaka wapate akili!
   
 11. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  JICHO D, you have the great point.
  JUWATA na OTTU walipokuwa wanajenga hoja ya kuongezewa mshahara na kutoa mchanganuo wa gharama ya mahitaji ya msingi, dagaa ilikuwa katika orodha na bei yake ilikuwa chini ya utumbo wa ng'ombe. Leo kilo ya dagaa inaacha zaidi ya maradufu ile ya sukari.

  Lipo tatizo kubwa katika Serikali ya Kikwete nalo kutowajibika na kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei. Nchi inaenda naturally.
   
 12. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Dah!ni miaka isiyo na njaa vyakula vipo ila havishikiki.
   
 13. Digna37

  Digna37 JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: May 17, 2010
  Messages: 835
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Subirini njaa itakapoingia. Sasa kila kitu kipo na hali ndio hiyo.
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Tena nimesikia Tanzania inataka kuipa msaada wa Computer Japan, na imedhihirika Obama anaionea gere Tanzania kutokana na uchumi wetu kupaa kwa kasi ya ajabu.
   
 15. MANI

  MANI Platinum Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,870
  Trophy Points: 280
  Mwe yaani raha tupu!
   
 16. h

  hamenya Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 7, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nadhani hao ni wale dagaa wa Ziwa Victoria na may be dagaa wa Baharini... Kimbembe ni kwa sisi tuliozoea dagaa wa KIGOMA-ziwa tanganyika hapo ndio balaa maana kwasasa bei ni 22,000 kwa Kilo. Maisha bora kwa kila mtaanzania.

  :A S embarassed:
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Heri yako wewe unapata 250,000/=, sisi wabunge tunalipwa elfu 70 tu (kwa siku), tumelilia 200,000/= hatujapewa!
   
 18. M

  MUGUNDA Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Kikwete kaza buti watu wapasuke wajue kilichowatuma kukupigia kura, ingawa kura nyingine uliiba kweli inawezekana na yangu uliiba make sikukupa kura mie.
   
 19. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Bado tunangoja kompyuta kwa kila shule na bajaji ambulance bana,oh no hayo mambo hayapo kwenye ilani ya chama,kumbe ilikua ni changa la macho, wajinga ndio waliwao
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Dagaa huwezi kununua lakini fedha ya kuingia mtandaoni unayo, au unaiba mtandao wa ofisini?
   
Loading...