Rais wangu Kikwete kwa haya nitakukumbuka !!

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
Kila mmoja katika kuubeba ubinadamu anao uwezo na udhaifu wake.Na sitaki kuamini kuwa kuna binadamu ni mbaya wakati wote wa nafasi yake katika dunia bali yapo mazuri pia.Kwa haya mawili Kikwete nitakukumbuka
::
1
UHURU WA FIKRA
Nakuona kuwa Rais pekee mwenye kifua cha kuvumilia kukosolewa.Umeruhusu maoni,mitazamo,na michango tofauti.Uhuru huu umevuka mipaka lakini unauthamini.Sidhani ingekuwa rahisi kwa wengine nikikulinganisha na watangulizi wako.Ni kweli pia elimu na maarifa yamepanuka sana hivyo jamii inaamini ni vigumu kudhibitiwa Lakini kwa mamlaka uliyonayo ungeweza kutumia ubabe kuzima uhuru.Spika Anna Makinda nadhani anapaswa ajifunze kwa hili ili wabunge wetu awape uhuru wa kujadili hoja.
::
2
KUANIKA UOZO
Nikitazama vizuri hakuna awamu ya Urais iliyoweka hadharani uovu wake na ule wa nyuma kama awamu yako.Umekuwa wazi kuruhusu chunguzi japo matokeo ya chunguzi yanabaki kitendawili Lakini hata kuanikwa tu yakafahamika ni kazi nzuri.Mf. Kuanikwa kwa Uozo wa Richmond,Uozo wa EPA,uozo wa halmashauri nyingi Tanzania kupitia office ya C.A.G (uliyoipa nguvu ya kisheria) n.k Yote ya baraka zako.Ungeweza kuagiza yakafukiwa ila tabia yako ya kuruhusu UNDER CARPET to be ON CARPET inanipa nguvu ya kukusifu.
Rais wangu nitakukumbuka kwa hayo.
=
 
Bila kusahau huwa anashauriwa vibaya na watendaji wake
 
Umesahau mkuu mauaji ya mwangosi na mateso ya ulimboka na ugoni wa mwigulu nao ulikuwa wazi japo haujashughulikiwa pia
 
Kweli kabisa hata wezi wa pembe za ndovu kwa kutumia meli zao tume wafahamu kwenye awamu yake!

*Rushwa ya kutumia vitumbua tumeifahamu kwenye awamu yake!

*watoto kufaulu bila kujua kusoma na kuandika tumelifahamu kwenye awamu yake.

*mtihani wa hesabu kuwa na majibu ya kuchagua kama a,b,c tulipata kwenye awamu yake!

*muungano wa visiwa vya zimbabwe na pemba tumeupata kwenye awamu yake!

Kweli hata mimi sito msahau!

*
 
Kupendelea waislam zaidi katika kila jambo, anataka hadi sheria ziitambue dini yake. Anatulazimisha wakristo na madhebu mengine kuabudu dini ya kiislam. Huyu rais fake
 
dunia tunayoishi leo inawalazimu viongozi na serikali zao kuonekana hivyo!

UsiGeneralize mambo mkuu. Kuna nchi zinazoendeshwa kiimla hadi leo hii.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Sita msahau kwakupaisha deni la Taifa kwa kufanya kila mtanzania anadaiwa si chini ya laki nne mpaka mimba inadaiwa Ccm hoyeeeeeeeeeeeee
 
UsiGeneralize mambo mkuu. Kuna nchi zinazoendeshwa kiimla hadi leo hii.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

hebu nitajie nchi tano tu zenye serikali za kiimla na ambazo haziface hii challange ya mabadiliko.
 
Kama umekariri kwamba uongozi wa kiimla ni hadi iwe kama Uganda ya Idd Amin huwezi kunielewa.

Kwanza inaonyesha wewe ni bendera fuata upepo kwasababu kama ungekuwa unaamini kweli Tanzania inahitaji uhuru wa pili kutoka kwa mkoloni mweusi CCM (kwa imani yenu nyie wanaCHADEMA) basi ungeelewa moja kwa moja kwamba hadi leo hii bado kuna nchi zinazoendeshwa kiimla.

Changamsha akili mkuu, Google sasa hivi utaziona. Kupenda kwako kutafuniwa kila kitu ndiyo kumekufanya ukariri na kufuata mkumbo wa vitu usivyovielewa maana yake.

Sayansi na teknolojia mkuu inamfanya awe hivyo apende asipende,zamani ilikuwa ni ngumu kupata taarifa ndo maana ilikuwa rahisi kuficha mambo.mara ngapi mambo yanafichwa ila watu wakiyashupalia wanalegeza,kama ni uhuru kwanini asilifungulie gazeti la mwanahalisi?halafu kuruhusu uchunguzi ufanyike bila kutoa majibu au kufanyia kazi mapendekezo ya tume mbalimbali mi naona ni upumbavu zaidi kwa sababu measures taken ndo jambo la msingi
 
kyumana
Nakubaliana na hoja yako lakini tukitazama mamlaka ya Rais anayopewa na katiba,angeweza kufungia sio magazeti tu bali hata radio stations,mitandao ya kijamii kama Jamiiforums n.k ambazo zinajihusisha na siasa.PERSONAL CHARACTER aliyonayo Kikwete ndio walau inatufanya mimi na wewe tubadilishane fikra.
Nampongeza
 
Last edited by a moderator:

acha porojo jibu swali!
 
Umesahau mkuu mauaji ya mwangosi na mateso ya ulimboka na ugoni wa mwigulu nao ulikuwa wazi japo haujashughulikiwa pia

Bila ya kusahau na yule padre wa CD.M mwizi wa wake za watu
 
Sayansi na teknolojia mkuu inamfanya awe hivyo apende asipende,zamani ilikuwa ni ngumu kupata taarifa ndo maana ilikuwa rahisi kuficha mambo.mara ngapi mambo yanafichwa ila watu wakiyashupalia wanalegeza,kama ni uhuru kwanini asilifungulie gazeti la mwanahalisi?halafu kuruhusu uchunguzi ufanyike bila kutoa majibu au kufanyia kazi mapendekezo ya tume mbalimbali mi naona ni upumbavu zaidi kwa sababu measures taken ndo jambo la msingi

Huo utofauti wa technology kipindi cha Ben na sasa ni mkubwa kiasi gani hata ishindikane kipindi hicho.Hata kama hupendi ila ukweli utabaki kua ukweli
 
kyumana
Nakubaliana na hoja yako lakini tukitazama mamlaka ya Rais anayopewa na katiba,angeweza kufungia sio magazeti tu bali hata radio stations,mitandao ya kijamii kama Jamiiforums n.k ambazo zinajihusisha na siasa.PERSONAL CHARACTER aliyonayo Kikwete ndio walau inatufanya mimi na wewe tubadilishane fikra.
Nampongeza
Ni kweli na nimekusoma lakini inabidi kiwepo kigezo cha kufunga na ukifunga zote kwa wakati mmoja watu wanaquestion.Ila ukilinganisha na marais waliopita ye kajitahidi hata kama pengine hajapenda iwe hivyo.
 
hebu nitajie nchi tano tu zenye serikali za kiimla na ambazo haziface hii challange ya mabadiliko.

kwa kauli yako ya "idadi ya tano tu" unaonekana hujiamini.Kwanini usiseme taja moja tu?
 
Bila ya kusahau na yule padre wa CD.M mwizi wa wake za watu
hata mzee wa fast jet si alimpokonya juma nature mke(sinta) na kumpeleka Nairobi na kupata unyumba au umesahau mkuu
 
Back
Top Bottom