Rais wangu Kikwete kwa haya nitakukumbuka !!

Museven ni mtu mbaya sana na anaitia doa Afrika Mashariki. Maswali ya kujiuliza, huko Uganda hakuna social networks? Hakuna magazeti? Hakuna watu wanaopingana na udhalimu wake? Wanaishia wapi?

Kikwete anastahili pongezi kwa hili la kuruhusu watu kujieleza.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Upuuzi ni kudhani kuwa uhuru tulionao ni kwa huruma/rehema za Kikwete. Ukweli ni kuwa Tanzania ya sasa hivi haitawaliki kiimla. Tunapenda kujilinganisha na Uganda, kwanini tusijilinganishe na Kenya? Mngekuwa na ndugu waliopigwa risasi na polisi msingeandika mlichoandika.
 
mi nitamkumbuka kwa kuwafunga amatus liyumba na babu seya kwa kisasi cha ngono na vilevile ntamkumbuka ktk awamu yake ndio rekodi ya ginesi ilipovunjwa kwa twiga kupanda ndege na vilevile waziri kusema bilion yani milioni elfu moja ni vijisenti wakati
serikari inashndwa kununua hata vitanda au nyembb kwa ajili ya wajawazito
 
Upuuzi ni kudhani kuwa uhuru tulionao ni kwa huruma/rehema za Kikwete. Ukweli ni kuwa Tanzania ya sasa hivi haitawaliki kiimla. Tunapenda kujilinganisha na Uganda, kwanini tusijilinganishe na Kenya? Mngekuwa na ndugu waliopigwa risasi na polisi msingeandika mlichoandika.

Kama unaishi Afrika Mashariki hiki ulichokiandika hapa ni negative effect ya kuPost saa tisa ya usiku.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Upuuzi ni kudhani kuwa uhuru tulionao ni kwa huruma/rehema za Kikwete. Ukweli ni kuwa Tanzania ya sasa hivi haitawaliki kiimla. Tunapenda kujilinganisha na Uganda, kwanini tusijilinganishe na Kenya? Mngekuwa na ndugu waliopigwa risasi na polisi msingeandika mlichoandika.

Nani kasema Rais akiamua udikteta kuna wa kumzuia? Nani kasema Kenya haina amani kwa sababu Kibaki hana huruma na watu wake?
Hatuoni kuwa tatizo la msingi lililopoteza amani Kenya ni ubaguzi wa kikabila?
Hatuoni jinsi Kenya inavyotumiwa na jumuiya ya Kimataifa kama kichaka kuendeleza vita Somalia?
Hatuoni unafiki wa nchi bepari zinavyochezea akili za waafrika na kuchochea vita Sudan? Libya? Mali? DRC,n.k ni kwa tamaa ya rasilimali na kutafuta soko la silaha?
BADO NAAMINI KIKWETE amejitahidi sana kuvumilia tofauti hizi angeamua angefanya.
 
kyumana
Nakubaliana na hoja yako lakini tukitazama mamlaka ya Rais anayopewa na katiba,angeweza kufungia sio magazeti tu bali hata radio stations,mitandao ya kijamii kama Jamiiforums n.k ambazo zinajihusisha na siasa.PERSONAL CHARACTER aliyonayo Kikwete ndio walau inatufanya mimi na wewe tubadilishane fikra.
Nampongeza

Mimi nashangaa unampongeza mtu kwa kukupatia haki yako kisa eti wengine hawapati haki kama wewe! Huu ni uzuzu. Kuna mwanafalsafa alisema nanukuu 'when oppression persist for long time it reaches a point when the oppressed starts to think like the oppressor'. Kwa sababu hiyo haya maneno yako kwamba rais angeweza kufungia hata radio, mitandao ya kijamii nk yanatakiwa yatamkwe na rais na sio wewe. Akili yako imeathiriwa na ukandamizwaji wa muda mrefu.
 
Last edited by a moderator:

Adolf Hitler ni dictator ambaye historia ya dunia haiwezi kumsahau.Alichaguliwa kidemokrasia lakini pamoja na umahiri wa hotuba za matumaini alizowapa wajerumani Bado alipoingia madarakani aligeuka wajerumani na kuwaachia makovu.
Nadhani tunaona Kikwete anasitahili kuwa kama alivyo lakini hili si sahihi wakati wote.MF awamu ya Nyerere sio kwamba haikuwa na watu wanaofikiri mf wa Kambona,,ila tu uhuru ulibanwa kitakatifu..
NG'OMBE HAJUI FAIDA YA MKIA MPAKA UKATWE,,siku tukipata Rais asiyevumilia kukosolewa ndio tutamkumbuka Kikwete
 
jamaa yangu we akili ya uelewa imebaki kwenye kisigino huku ukienda juu kama mti uliacha miziz chini niyap aliyoyafanya kukulazimisha uabudu dini yake huo ndio udini watanzania kila siku wanalisemea we mjadala wa jambo jingine umeingiza suala la dini unamaono kweli au kitumbuu changanya na kachumbar
 
Udini wenu utawamaliza. Lakini mtaipata fresh sasa hivi!
 
jamaa yangu we akili ya uelewa imebaki kwenye kisigino huku ukienda juu kama mti uliacha miziz chini niyap aliyoyafanya kukulazimisha uabudu dini yake huo ndio udini watanzania kila siku wanalisemea we mjadala wa jambo jingine umeingiza suala la dini unamaono kweli au kitumbuu changanya na kachumbar

IKORI
Ni wapi nimetaja kumkumbuka Kikwete kwa udini wake?
That's a wise word out of this topic
 
Last edited by a moderator:
Kila mmoja katika kuubeba ubinadamu anao uwezo na udhaifu wake.Na sitaki kuamini kuwa kuna binadamu ni mbaya wakati wote wa nafasi yake katika dunia bali yapo mazuri pia.Kwa haya mawili Kikwete nitakukumbuka
::
1
UHURU WA FIKRA
Nakuona kuwa Rais pekee mwenye kifua cha kuvumilia kukosolewa.Umeruhusu maoni,mitazamo,na michango tofauti.Uhuru huu umevuka mipaka lakini unauthamini.Sidhani ingekuwa rahisi kwa wengine nikikulinganisha na watangulizi wako.Ni kweli pia elimu na maarifa yamepanuka sana hivyo jamii inaamini ni vigumu kudhibitiwa Lakini kwa mamlaka uliyonayo ungeweza kutumia ubabe kuzima uhuru.Spika Anna Makinda nadhani anapaswa ajifunze kwa hili ili wabunge wetu awape uhuru wa kujadili hoja.
::
2
KUANIKA UOZO
Nikitazama vizuri hakuna awamu ya Urais iliyoweka hadharani uovu wake na ule wa nyuma kama awamu yako.Umekuwa wazi kuruhusu chunguzi japo matokeo ya chunguzi yanabaki kitendawili Lakini hata kuanikwa tu yakafahamika ni kazi nzuri.Mf. Kuanikwa kwa Uozo wa Richmond,Uozo wa EPA,uozo wa halmashauri nyingi Tanzania kupitia office ya C.A.G (uliyoipa nguvu ya kisheria) n.k Yote ya baraka zako.Ungeweza kuagiza yakafukiwa ila tabia yako ya kuruhusu UNDER CARPET to be ON CARPET inanipa nguvu ya kukusifu.
Rais wangu nitakukumbuka kwa hayo.
=

Ongeza Miundombinu,Afya na Elimu.
 
Adolf Hitler ni dictator ambaye historia ya dunia haiwezi kumsahau.Alichaguliwa kidemokrasia lakini pamoja na umahiri wa hotuba za matumaini alizowapa wajerumani Bado alipoingia madarakani aligeuka wajerumani na kuwaachia makovu.
Nadhani tunaona Kikwete anasitahili kuwa kama alivyo lakini hili si sahihi wakati wote.MF awamu ya Nyerere sio kwamba haikuwa na watu wanaofikiri mf wa Kambona,,ila tu uhuru ulibanwa kitakatifu..
NG'OMBE HAJUI FAIDA YA MKIA MPAKA UKATWE,,siku tukipata Rais asiyevumilia kukosolewa ndio tutamkumbuka Kikwete

Hamna mantiki hapo zaidi ya 'ukarimu' wa kitanzania wa kuomba bia kaunta ilhali unailipia!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nani kasema Rais akiamua udikteta kuna wa kumzuia? Nani kasema Kenya haina amani kwa sababu Kibaki hana huruma na watu wake?
Hatuoni kuwa tatizo la msingi lililopoteza amani Kenya ni ubaguzi wa kikabila?
Hatuoni jinsi Kenya inavyotumiwa na jumuiya ya Kimataifa kama kichaka kuendeleza vita Somalia?
Hatuoni unafiki wa nchi bepari zinavyochezea akili za waafrika na kuchochea vita Sudan? Libya? Mali? DRC,n.k ni kwa tamaa ya rasilimali na kutafuta soko la silaha?
BADO NAAMINI KIKWETE amejitahidi sana kuvumilia tofauti hizi angeamua angefanya.

Unadharau ufahamu wako. Niko nilivyo kwa kuwa Mungu ametaka iwe, sio Kikwete. Kama nyie mnaneemeka kwa sababu yake, good for you.

Back
Top Bottom