Siku nyingine mkipata nafasi za kwenda nje pitieni kwenye vijiwe vya watoto wa mujini mjifunze mbinu nyingine za kuishi nje za nchi.
...kati ya hao wanafunzi kuna ambao wanasoma mwaka wa tatu sasa, miaka mitatu Ujerumani bila ya kuwa na connection ya japo kijikazi cha kuosha vyombo kwenye migahawa ya Kebab si rahisi kumtokea mtoto aliyetokea "kijiweni" hata kukiwa na Wapolish,Wabulgaria,n.k wa kumwaga (Waturuki wapo wengi Ujerumani tokea zamani sana)!
Pia kuna tatizo kwa Watanzania wengi (si wote) ku-intergrate katika nchi wanazoishi.
Vinginevyo natumai kuwa matakwa yenu (waathirika)yaliyo katika mikataba yatatimizwa haraka!
Kua jambo muhimu sana umelisema kwenye thread yako...
Jibu lake ni Kwamba,Katika Wanafunzi ambao wanasoma NCHI za NJE DUNIANi(tofauti na nchi zao),hususani wanaotoka nchi zinazoendelea,WATANZANIA ni Wanafunzi wanaaonekana ni CLASS A citizens kutokana na kwamba wengi wao huwa wanatimiziwa MAHITAJI YAO kadiri iwezekanavyo kutoka kwa serikali zao...
Kama umewahi kusoma Vyuo vya nje,kwa kweli utaweza kuona jinsi Wanafunzi wa kutoka Nchi nyinginezo hususani za Afrika jinsi wanavyopata taabu katika kukidhi mahitaji yao,kwani serikali za Nchi zao either hazina uwezo kabisa wa kuwagharimia chochote,ama hazitimizi kabisa mikataba ya kuwalipia chochote kile,hivyo Waafunzi hao walishajizoesha kwamba serikali zao haziwasikilizi chochote,na mara zote wanajitahidi kufanya kile wawezacho kujikimu.
Hii inaweza kudhihirisha kwamba katika nchi zinazoendelea,Tanzania ni Nchi mojawapo inayojitahidi sana sana katika kutimiza majukumu yake,licha ya kwamba si kwa muda sana,lakini bado serikali ni Tegemeo kubwa sana kwa Wananchi wake.
Ukitaka kujua pia kwamba Tanzania ni Nchi nzuri,linganisha idadi ya Wanafunzi wanaorudi nyumbani mara tu baada ya kumaliza masomo yao katika nchi yeyote huko Ughaibuni.....Watanzania wanaongoza,,,,kwa sababu Nchini kwao kuna "promising future".......Waafrika wengi sana huwa wakimaliza masomo Nchi za nje hubaki huko
Ninakumbuka mwaka mmoja nusu uliopita mliandika pia hapa jamiiforums kuhusu malalamiko yenu kama haya
Ni haki yenu,,,,lakini ninadhani kwamba mnawahi mno kutoa malalamiko,,,,,hivi hamjalipwa hela ya May na June ama ni hela ya June tu?
Kuna Watu wanasoma nje pia,huwa hawalipwi hata kwa miezi 6,lakini huwa wanakuwa wavumilivu kidogo.
Kwa muda huu ninawatakia uvumilivu bora...endeleeni kutumia mishahara yenu(ambayo ninaamini mipango madhubuti ya serikali yenu inawawezesha muendelee kupokea mishahara huku mkiwa masomoni).
Nawatakia kila la kheir.....
Pia mjitahidi kuosha masufuria na kupandisha zege huko maghorofani jamani...Ohoooo