Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi afanya uteuzi mwingine. Amteua Suleiman Ahmed Salum kuwa Katibu wa Rais

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Bwana Suleiman Ahmed Salum kuwa Katibu wa Rais.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kabla ya uteuzi huo Bwana Suleiman Ahmed Salum alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya Pamoja ya Fedha.

Uteuzi huo ameufanya Dk. Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Rais Dk. Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 6(1) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya mwaka 1997, amemteua Bwana Nahaat Mohammed Mahfoudh kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 04 Novemba, 2020.
67A5EC44-E4CE-476D-B018-89EBA982174D.jpeg
 
Attachments

  • 2160F9D7-0DCE-402A-B720-965874C8DEE3.jpeg
    2160F9D7-0DCE-402A-B720-965874C8DEE3.jpeg
    17 KB · Views: 1
Tarehe 4 November 2020 hadi tarehe 14 December 2020.
Hamna kuonyana awamu hizi.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua Bwana Suleiman Ahmed Salum kuwa Katibu wa Rais.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kabla ya uteuzi huo Bwana Suleiman Ahmed Salum alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Tume ya Pamoja ya Fedha.

Uteuzi huo ameufanya Dk. Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 53 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Rais Dk. Hussein Mwinyi kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 6(1) cha Sheria ya Shirika la Bandari Namba 1 ya mwaka 1997, amemteua Bwana Nahaat Mohammed Mahfoudh kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 04 Novemba, 2020.View attachment 1619498
Kapigwa SPANA.....hahahaaa
 
Back
Top Bottom