Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy azuiliwa na polisi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
_100490169_sarkozyindexafp.jpg

France.jpg

Aliyekuwa Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anazuiliwa na polisi akihojiwa kuhusu tuhuma kwamba alipokea pesa za kufadhili kampeni zake kutoka kwa kiongozi wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.

Polisi wanachunguza tuhuma hizo kuhusiana na ufadhili wa fedha alizotumia kwenye kampeni za uchaguzi wa urais mwaka 2007.

Polisi waliwahi kumhoji awali.

Msaidizi wake wa zamani Alexandre Djouhri pia alikamatwa jijini London karibuni.

Bw Sarkozy alishindwa katika juhudi zake za kutaka kurejea madarakani mwaka 2012.

Chanzo: BBC
 
3000.jpg

Nicolus Sarkozy, rais mstaafu wa Ufaransa, anashikiliwa na jeshi la polisi la Ufaransa kwa tuhuma za ufisadi wa chaguzi zake zilizotumia hela ya Muammar Gaddhafi wa Libya.

Huu ni muendelezo wa marais wastaafu wanaotuhumiwa kwa makosa mbali mbali baada ya kutoka madarakani, akiwemo Jacob Zuma wa South Afrika.

Haya yanawezekana tu katika nchi ambazo katiba zao hazilindi madhambi ya Rais kwa kinga ya mashitaka. Tanzania sio mfano wa nchi hizo, hivyo Rais yeyote wa Tanzania anakaa kwa amani ya kufanya lolote analotaka.
 
Kumbe Unazungumzia Dunia Ya 3...!!!!

Huku Kwetu Bado Kidogo Tutafika Ndugu Yangu Tuwe Wapole Na Wavumilivu
 
Well, South Afrika ni dunia ya tatu lakini wamefika. Isipokuwa ndio hivyo tena, dunia ya tatu hakuna kinacho make sense, Zuma anashitakiwa kwa makosa aliyofanya kabla hajawa Rais, which means mlimuweka mtu madarakani akiwa tayari criminal!

Afrika ni kituko cha dunia
 
Hizi nchi za dunia ya kwanza hazikufika hapo leo,kwa hiyo kuwa mpole mkuu polepole ndio mwendo!!!!
 
South Africa ni iko kwenye Dunia ya pili.
 
Well, South Afrika ni dunia ya tatu lakini wamefika. Isipokuwa ndio hivyo tena, dunia ya tatu hakuna kinacho make sense, Zuma anashitakiwa kwa makosa aliyofanya kabla hajawa Rais, which means mlimuweka mtu madarakani akiwa tayari criminal!

Afrika ni kituko cha dunia
Nikili Kwa Kusema

Sehem Zingine Kuna Mapungufu Ila

Africa Tumezid
 
Hizi nchi za dunia ya kwanza hazikufika hapo leo,kwa hiyo kuwa mpole mkuu polepole ndio mwendo!!!!

nchi za dunia ya kwanza hazikufika hapo leo, ndio, lakini pia wao walikuwa hawana template, yani kitu cha kuiga na kujifunzia, ndio maana walichukua muda mrefu.

Hapakuwa na live TV wala smartphone zinazopata habari za dunia nzima ndani ya dakika.

Sisi tunayo blue print, yani tunawaangalia wenzetu walipokosea na wanapopatia lakini hatujifunzi. Unataka kunambia waandishi wa Katiba zetu hawajui madhara ya kumpa mtu madaraka bila uwajibikaji?

Kwa nini watu wa chini ya Rais wanapelekwa mahakamani, Rais yeye ni malaika?
 
African countries,except SA
 
Back
Top Bottom