Rais wa zamani wa DRC atua Goma

Rais wa zamani wa DRC atua Goma

VERITE-NUE

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
1,481
Reaction score
1,450
Joseph Kabila aliyekuwa Rais wa DRC amezungumza kwa video na akamuita Rais wa sasa wa DRC Dictator. Kabila amezungumza baada ya Bunge la DRC kumuondolea kinga ya kutokushitakiwa. Mamlaka za DRC zinataka kumshitaki kabila kwa makosa ya Uhaini na uhalifu wa kivita akihusishwa na M23.

Serikali ya sasa ina wafuasi wengi wa Kabila, na huku zaidi ya wanajeshi wakuu 20 wapo nyuma ya nondo, kufuatia kinachoitwa usaliti uliopelekea Kivu zote kuangukia mikononi mwa AFC/M23(waasi).
 
Goma Kwa Sasa Iko chini ya M23.
Tshekedi anamshutumu Kabila kujihusisha na M23.
Kabila anakanusha hahusiki na M23.
Kabila ameondolewa Kinga.
Kabila anamshutumu Tshekedi kwamba ni Dikteta.
Kabila amekimbia kukamatwa na Mamlaka za DRC.
Kabila amekimbilia Goma kwenye Ngome ya M23..
 
Kwa kifupi ni kwamba serikali ya Tshisekedi baada pia ya kugundulika mawaziri ni wala rushwa na wezi hatari, ni ngumu kuhimili. Nguvu yake na rais wa Burundi, haiwezi kuliokoa taifa.
 
Na hapo ndo pa kufikilia zaidi ya mara mbili, kuwa tuhuma za SADC kurudisha wanajeshi na silaha zao huko mashariki mwa DRC zina mashiko.
 
Joseph Kabila aliyekuwa Rais wa DRC amezungumza kwa video na akamuita Rais wa sasa wa DRC Dictator. Kabila amezungumza baada ya Bunge la DRC kumuondolea kinga ya kutokushitakiwa. Mamlaka za DRC zinataka kumshitaki kabila kwa makosa ya Uhaini na uhalifu wa kivita akihusishwa na M23.

Serikali ya sasa ina wafuasi wengi wa Kabila, na huku zaidi ya wanajeshi wakuu 20 wapo nyuma ya nondo, kufuatia kinachoitwa usaliti uliopelekea Kivu zote kuangukia mikononi mwa AFC/M23(waasi).

Waasi wa M23 wasema rais wa zamani Joseph Kabila amewasili mjini Goma
Kabila

Chanzo cha picha,Joseph Kabila PR
Waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DRC wanasema rais wa zamani Joseph Kabila amewasili katika mji mkuu Goma, akitokea uhamishoni.
Serikali mjini Kinshasa imemshutumu Bw Kabila kwa kuhusishwa na kundi linaloungwa mkono na Rwanda, M23. Wiki iliyopita, Seneti iliondoa kinga yake dhidi ya kushtakiwa ili aweze kushtakiwa kwa uhaini, Mhariri wetu wa kanda ya Afrika, Will Ross, anaripoti.
Joseph Kabila yuko katika mazingira magumu kwa sasa kwa kuwa hana tena kinga ya kushtakiwa.
Wiki iliyopita Bw Kabila alisema kipaumbele chake kikuu ni kuondoa kile alichokiita udikteta. Kwa hiyo inawezekana kwamba mtu ambaye kwa muda mrefu anaonekana kuwa karibu na Rwanda anajiunga na waasi wa Kigali wanaoungwa mkono na M23 kama sehemu ya harakati za kujaribu kumpindua rais Felix Tshisekedi.
Kuna hatari ambayo inaweza kusababisha mvutano mpana wa mzozo katika nchi jirani kwa pande zinazopingana.
Unaweza kusoma;
Mzozo wa DRC: Kwanini jeshi la Congo haliwezi kulilinda eneo la Mashariki?
Je, kurudi DR Congo kwa Joseph Kabila kuna maana gani wakati huu wa vita?

=========================

Kumekucha huko Drc, ... Kabila ana ndoto za kurudi madarakani?

Tresor Mandala JokaKuu Yoda zitto junior
 
Habari ya lini hii? Najua alikua huko muda kdg
 
SADC wamerudisha silaha na askari DRC!?
Inavosemekana. Maana badhi zilitoka South Africa na kuhifadhiwa Burundi, na njia kutoka Rusumo hadi Bujumbura, ipo wazi. SADC haijaamini kilichoikuta, huenda bado ina nia na sababu ya kupigana. Ila jamaa walikusanya kitendea kazi aise! Vitu cinavyosombwa mpaka leo hii, ile mission ndo ingeitwa Almagedon.
 
Kabila aliacha watu ndani ya serikali ya DRC, ndiyo iliyowa-cost sadc
 
Goma Kwa Sasa Iko chini ya M23.
Tshekedi anamshutumu Kabila kujihusisha na M23.
Kabila anakanusha hahusiki na M23.
Kabila ameondolewa Kinga.
Kabila anamshutumu Tshekedi kwamba ni Dikteta.
Kabila amekimbia kukamatwa na Mamlaka za DRC.
Kabila amekimbilia Goma kwenye Ngome ya M23..
Unaposema kabila amekimbia kukamatwa, amekimbilia Goma unamaanisha nini!? Kabila siku zot3 baada ya utawala wake hakuwa anaishi Congo DR so unaposema kakimbia kukamatwa na kukimbilia Goma unakuwa unapotosha. Kabila kaenda Goma kwa ziara/ misheni maalum na atarudi alipokuwa.
 
Inavosemekana. Maana badhi zilitoka South Africa na kuhifadhiwa Burundi, na njia kutoka Rusumo hadi Bujumbura, ipo wazi. SADC haijaamini kilichoikuta, huenda bado ina nia na sababu ya kupigana. Ila jamaa walikusanya kitendea kazi aise! Vitu cinavyosombwa mpaka leo hii, ile mission ndo ingeitwa Almagedon.
Kabila alihusika kuuwa mzee desire kabila rais wa congo. Baba wa Jambo. Kosa alilofanya tshekedi ni kumuacha hai. Ilitakiwa alipoingia madarakani wangemuuwa. Haya unayoyaona usingeyaona Wala kuyasikia
 
Unaposema kabila amekimbia kukamatwa, amekimbilia Goma unamaanisha nini!? Kabila siku zot3 baada ya utawala wake hakuwa anaishi Congo DR so unaposema kakimbia kukamatwa na kukimbilia Goma unakuwa unapotosha. Kabila kaenda Goma kwa ziara/ misheni maalum na atarudi alipokuwa.
Amekuwa akiishi wapi? Je ni kweli anataka kuwa raisi mpya wa kivu Republic?
 
Unaposema kabila amekimbia kukamatwa, amekimbilia Goma unamaanisha nini!? Kabila siku zot3 baada ya utawala wake hakuwa anaishi Congo DR so unaposema kakimbia kukamatwa na kukimbilia Goma unakuwa unapotosha. Kabila kaenda Goma kwa ziara/ misheni maalum na atarudi alipokuwa.

Kuondolewa Kinga ya kushtakiwa kumemuweka kwenye hatari ya kukamatwa, na ameona Goma ndiyo mahali salama Kwake dhidi ya wanaotaka kumkamata..

Huenda huko unakosema alikuwa amehofu kuwa wanaweza kumnasa kirahisi.

Hayo ya misheni unayosema, angeweza kwenda Kinshasa kuifanyia huko, ila ameona ni bora Goma ambako ni strong hold ya M23 Kwa Sasa.. Swali ni je, Kabila anahusiana na M23 Kwa maslahi ya nani?
 
Kuondolewa Kinga ya kushtakiwa kumemuweka kwenye hatari ya kukamatwa, na ameona Goma ndiyo mahali salama Kwake dhidi ya wanaotaka kumkamata..

Huenda huko unakosema alikuwa amehofu kuwa wanaweza kumnasa kirahisi.

Hayo ya misheni umeyasema wewe, angeweza kwenda Kinshasa kuifanyia huko, ila ameona ni bora Goma ambako ni strong hold ya M23 Kwa Sasa.. Swali ni je, Kabila anahusiana na M23 Kwa maslahi ya nani?
Si kwa maslahi gani. Nchi ni yake, ameiongoza kama rais, yule ni mwanajeshi. Unadhani Tshisekedi anamzidi nguvu na maarifa? Kujiunga na M23 kwanza ni pigo lingine kwa serikali. Kumbuka, enzi zake, ana washilika wangapi, kibiashara! Siasa ni faida hainaga urafiki. Atakaewekewa mezani mikataba inayoeleweka, support atapata ya kutosha.
 
Goma Kwa Sasa Iko chini ya M23.
Tshekedi anamshutumu Kabila kujihusisha na M23.
Kabila anakanusha hahusiki na M23.
Kabila ameondolewa Kinga.
Kabila anamshutumu Tshekedi kwamba ni Dikteta.
Kabila amekimbia kukamatwa na Mamlaka za DRC.
Kabila amekimbilia Goma kwenye Ngome ya M23..
Mchezo mgumu sana huu kuucheza, ni kama wa Mbwa kufukuza mia wake.
 
Si kwa maslahi gani. Nchi ni yake, ameiongoza kama rais, yule ni mwanajeshi. Unadhani Tshisekedi anamzidi nguvu na maarifa? Kujiunga na M23 kwanza ni pigo lingine kwa serikali. Kumbuka, enzi zake, ana washilika wangapi, kibiashara! Siasa ni faida hainaga urafiki. Atakaewekewa mezani mikataba inayoeleweka, support atapata ya kutosha.

Je ni sahihi kutumia Siasa Kwa Maslahi Binafsi na kuacha nyuma maslahi ya Nchi na Wananchi wote kiujumla?

Je anachokifanya Kabila kuungana na Waasi (ambao kimsingi waliokuwa maadui zake kipindi akiwa Rais) Kuna Manufaa Kwa Congo na Ukanda wa Africa Mashariki na Kati kiujumla?
 
Back
Top Bottom