Rais wa wanyonge, wanyonge wapi?

Rais wa wanyonge, wanyonge wapi?

Molembe

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
9,932
Reaction score
11,849
Tangu ameingia madarakani rais Magufuli amekuwa akijinasibu kuwa yeye ni rais wa wanyonge, kauli hii imekuwa ikinishangaza sana, hivi rais Magufuli ni rais wa wanyonge wapi? Tangu ameingia madarakani hao wanyonge wamenufaika vipi na uongozi wake.

Rais aliingia madarakani wanyonge wakinunua sukari 1800/= leo hii 3000/=, unga 800/= leo hii 1200/=~1,500/= hao wanyonge anaowasaidia ni wa nchi gani?

Kipindi cha nyuma kulikuwa na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa wakulima lakini tangu aingie madarakani ruzuku hiyo haipo, watoto wa wanyonge waliokuwa waingie vyuo vikuu hawana mikopo wapo nyumbani wamekaa, kuna wanyonge wamemaliza vyuo vikuu lakini mpaka sasa hawana ajira na hawajui hatma zao, rais ameua elimu kwenye shule za kata ambazo watoto wa wanyonge wanasoma.
Kwa ufupi ni kwamba ameongeza umaskini kwa jamii, lakini cha ajabu kila akisimama anajinasibu yeye ni rais wa wanyonge, wanyonge wapi hao.
 
Halafu watu wengine bhana sijui mkoje,
Ina maana mkuu wanyonge huwajui wewe au unachezea akili zetu,
Mnyonge Gambo humjui au?
Mnyonge bashite humjui pia? Hebu acha hizo
Yule mnyonge Dotto James humjui pia?
Ina maana hujawahi kabisa kujua wale ndo wanyonge aliowasema rais?
Hizo habari zenu za pembejeo nyie kalimieni meno pumbafu zenu
Sisi kipaumbele chetu sio ninyi ni chato kwanza
Tunataka chato iwe kama dubai watu watoke los angels na Miam kuja kushangaa chato ilivyojengeka
 
Hao waliokosa mkopo waendelee kukaa tu nyumbani hivyohivyo wasijiongeze kwa lolote
Kuna watu lukuki wana vyeti wamerudi mtaani wanatoka kwa fursa nyingine kumbe wao wamekaa tu
 
Kwa kweli pamoja mimi ni mshabiki wake namba moja, naona swala la urais kwa wanyonge halipo, umeeleza yote hapo juu muhimu, hasa kutokusaidia mzunguko wa pesa kuwa mzuri, benki kunyanyasa wafanyabiashara wadogo na kutokutoa mikopo, tena wakadiriki na kusema wanawakopesha serikali tu na taasisi zake!
Asiporekebisha hili, tutamuona ni muongo na mbabaishaji, na huu mtindo wake wa kugawa mamilioni in (cash), na kuwagawia wanakwaya itabidi aache, kwani anafanya hivyo kuturingishia kwamba sisi hatuna ile yeye ndiyo anazo au?!
Either hasikilizi washauri au hana washauri, kwa kweli tumechoka kabisa na hili swala...
 
Raisi wa wanyonge ni Mungu tu.
Huyu mwingine ni raisi wa Wanaonyongwa.

Hakuna utetezi wowote,
Wanyonge wanateseka na kuhangaika na mtetezi anashangilia tu.

Oooh Tanzania nakupenda, siendi Zimbabwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri mataira wa kutoka ofisi ndogo za chama pale Lumumba watoke kanisani wakiwa matumbo wazi waje wakujibu
 
Back
Top Bottom