Kwa sasa Museveni amekuwa rais wa Uganda kwa muda mrefu kuliko Nyerere alivyokuwa rais wa Tanzania.Kaguta haachi vituko, mpaka vitukuu vitamkuta akiwa rais. Uganda inabidi iitwe the Kingdom under the leadership of King Yoweri Kaguta Museveni.
Wanasema kile kiti kina joto lenye utamu wa ajabu, kukiacha ni shida. Hata hawa marais wetu baada ya miaka mitano wanapigana kufa na kupona warudi tena.Kwa sasa Museveni amekuwa rais wa Uganda kwa muda mrefu kuliko Nyerere alivyokuwa rais wa Tanzania.
Museveni ana miaka 30 ya urais sasa.January 2017 anafikisha miaka 31.
Nyerere ukichanganya tangu uhuru wa Tanganyika 1961 mpaka anastaafu urais wa Tanzania 1985 ni miaka 24.
Mzee wangu alienda kumsalimia Mwinyi baada ya Mwinyi kustaafu (mshua alikuwa appointee wa Mwinyi). Kufika nyumbani mshua anamtakia hali, Mwinyi akawa anamlalamikia anasema ukitoka kwenye urais tu unaingia kwenye maisha tofauti sana na ulivyozoea. Watu wanakusahau unakuwa unakosa zile shamrashamra za power. Ile inawatia jakamoyo sana.Wanasema kile kiti kina joto lenye utamu wa ajabu, kukiacha ni shida. Hata hawa marais wetu baada ya miaka mitano wanapigana kufa na kupona warudi tena.
No commenta mkuu you said it all.Mzee wangu alienda kumsalimia Mwinyi baada ya Mwinyi kustaafu (mshua alikuwa appointee wa Mwinyi). Kufika nyumbani mshua anamtakia hali, Mwinyi akawa anamlalamikia anasema ukitoka kwenye urais tu unaingia kwenye maisha tofauti sana na ulivyozoea. Watu wanakusahau unakuwa unakosa zile shamrashamra za power. Ile inawatia jakamoyo sana.
Pia hawa wengine washaua na kutesa watu sana hivyo wanaona wakitoka madarakani watatupwa lupango.
We hebu fikiria Museveni astaafu urais halafu Kiiza Besigye awe rais. Patakalika hapo?
Kuna story moja ya Mugabe, baada ya Mugabe kushindwa urais, alikuwa tayari kuachia madaraka yaende upinzani. Wale ma top generals wake na watu wa security wakakataa, wakamwambia mzee wewe tulia tu kama matokeo ya uchaguzi sisi tutabadilisha tu.
Sababu ni kwamba wale watu wa security wameua sana na upinzani ungeshika madaraka wote wangefungwa. Kwa hiyo salama yao ilikuwa Mugabe aendelee kuwa rais.