Undercover_Bot
JF-Expert Member
- May 8, 2018
- 416
- 414
Hatuwezi shirikiana nao hao ndugu zako kwenye maswala ya usalama bado sanaaa...naona unawapigia debe sana ndugu zako hao watukamate akili kwenye idara zetu sahau hicho kituKama kuna Kitu kikubwa ambacho nakupongeza na sitoacha Kukupongeza Rais Dkt. Magufuli ni cha Kuona umuhimu wa kuwa na ukaribu kabisa na Rais wa Rwanda ' Genius ' na ' Mwanamume ' Paul Kagame na nina uhakika kuwa hutokuja Kujutia Ukaribu na Urafiki wako nae hasa katika suala zima la Maendeleo ya nchii yako hii ya Tanzania.
Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli yatasemwa mengi sana juu ya Urafiki na Ukaribu wako na Rais Kagame ila Mimi kama GENTAMYCINE leo nakuhakikishia kama kuna Rafiki mwema, makini na mzuri wa Kimaendeleo na ambaye nakuomba na nakushauri uendelee ' Kumkumbatia ' na hata ikibidi ' Kumnyenyekea ' basi ni Rais wa Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame.
Tena nakushauri Rais Dkt. Magufuli usiishie tu kuwa nae katika mambo ya Kimaendeleo hasa ya Kiuchumi bali nakuomba pia muombe akusaidie hasa katika Taasisi zako ' Nyeti ' kama za Polisi, Usalama na Jeshini kwani siyo Siri kwa sasa nchi ya Rwanda katika hayo maeneo ' Nyeti ' tajwa hapo ipo vizuri yawezekana hata kuliko Tanzania hivyo ukiwa nae karibu Rais Kagame atakusaidia ili kuboresha zaidi.
Ni kweli Rwanda ni nchi ndogo sana ambayo ' Kijiografia ' ina usawa wa Mji mzima wa Kahama ( kwa wale msiojua / Mangumbaru ) lakini ina Watu / Raia ambao yawezekana wakawa na uwezo mkubwa wa Kufikiri ( IQ ) kuliko hata nchi moja hivi Afrika Mashariki ( jina nimeisahau ) yenye Watu kama Milioni 55+ lakini wenye ' IQ ' kubwa hawazidi hata 3500 huku waliobaki wakiwa na ama Ungumbaru au Upopoma mwingi.
Rais yoyote yule makini duniani ni lazima tu atampenda Rais Kagame kwani Kiongozi Shujaa, Mthubutu, Makini, Haogopi, Anajiamini, ana Maono makubwa ya Kimaendeleo, Hatishwi na Wapuuzi wachache au wengi, Mzalendo wa ukweli na Mpambanaji hasa. Sishangai sana ndiyo maana unaweza kuona pamoja na Kelele za ' Mangumbaru ' na ' Mapopoma ' wengi dhidi yake lakini bado Rais Kagame ameendelea kuwa Kipenzi si tu kwa Wananchi wenye ' Akili ' kubwa wa Rwanda bali hata kwa Viongozi wa Mataifa makubwa na Tajiri duniani kama Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, Uchina na Ujerumani bila kuisahau na Afrika Kusini.
Rais Dkt. Magufuli piga Kazi na usimwache huyo ' Genius ' na ' Mwanamume ' Rais Kagame akae mbali nawe. Mtumie, Msikilize, Muige kwa mambo yake mengi ambayo pia ni mazuri sana na nina uhakika kuna Siku utakuja Kunikumbuka GENTAMYCINE kuwa nilikushauri Jambo zuri / jema. Tena kwa hii Tanzania yako ya sasa unayoiongoza nadhani unahitaji zaidi Msaada na Mwongozo mkubwa wa Rais Kagame ili kuiweka Tanzania sawa na kuwafanya Watanzania wawajibike, wajue kutumia akili zao vizuri na waache Kulialia na Kuendekeza tu Siasa kila mara wakati Maendeleo yanatuacha na wenye upeo wanatukimbia.
Ni hayo tu Rais Dkt. Magufuli na nakuomba uyazingatie yote haya niliyokueleza hapa.
Mungu ibariki Rwanda
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mungu ibariki Afrika
Mungu wabariki sana Marais Paul Kagame na Dkt. John Magufuli
Mungu mbariki mno GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE
Mungu walaani vikali na wapige Kofi zito wale wote wanaoichukia Rwanda, Rais wake, wanaomchukia pia GENTAMYCINE na Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli
Mungu ubariki kupita maelezo huu Mtandao wangu / wetu pendwa kabisa wa JamiiForums
Nawasilisha.
Sent using Jamii Forums mobile app