Rais wa nchi yetu anachagua nani wa kwenda Ikulu ambayo ni Mali ya watanzania wote?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Sina Nia ya kumtusi Rais wa nchi ila Mimi kama Raia mwema wa Taifa Ili lazima nihoji pale ninapo his katiba yetu inavunjwa na watu ambao kimsingi mnakula KIAPO Cha kuilinda katiba.

Leo hii baadhi ya watu tunajiuliza Rais aliyetokea chama Cha mapinduzi ni Rais wa WANANCHI ambao ni Wanachama wa CCM tu?

Najiuliza Rais wa nchi yetu anachagua. Nani wa kwenda ikulu ambayo ni Mali ya watanzania wote?

Leo hii hii vijana wetu ambao tumewapeleka shule wenyewe ambao wamesoma Kwa Kodi za nchi yetu hawajaewa ma'ana ya mkataba wa bandari wanakuja ikulu Ili Wewe ulitewekwa ikulu na Watanzania uwaelemishe unawatumia watua ambao hawawezi hata elezea ukurasa mmoja wa mkataba WA bandar wawakamate na kiwasweka rumande?

Najiuliza Rais wenye haki ya kukanyaga ikulu ni akina nani? Ni wale wanaoimba mapambio ya mama unaupiga mwingi? Ni vijana wa umoja wa UVCCM wanaongoza kwa kuiba pesa za Halimashauri mama?

Hivi Rais upo ikulu kuchagua chakula Ili hali hapo Wewe sio mkulima?

Aliyevunja katiba Kwa kiwakamata hao vijana walio andamana ni nani ni wewe amiri jeshi mkuu au?

Rais wapinzani wako,wanaharakati ni watu wako, na ccm ni wako hacha kuchagua wakukufurahisha kufanya hivyo ni SAWA na kuchagua chakula Cha rojo lilihali bara Kuna ugali na Michele.
 
Ingawa napinga mikataba inayoifukarisha nchi! Ila hapa mkuu sjaelewa ulichoandika!

Inawezekana unayo nia njema kichwani ila ulichoandika, si kile kimebaki moyoni!

Huku ndo kunaitwa, ulimi kushindwa kutamka kile kimo moyoni
 
Kuandika kwa tafsida na sitiari ni kipaji na si kila mtu anacho.

Wengine tubaki kuandika kawaida tueleweke kuliko kufanya jaribio la kuandika vitu vya maana ila kuishia kuonekana kituko kisichokuwa na mantiki.

Kichwa cha habari na mudhui ni mbingu na ardhi.
 
Watu tuna mambo mengi ya kutafakari tutapata kweli muda wa kufumbua haya mafumbo yako?

Nenda moja kwa moja kwenye point mkuu acha kuzunguka zunguka
 
Back
Top Bottom