Rais Wa Nchi ya Kusadikika...Azinduka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Wa Nchi ya Kusadikika...Azinduka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Mar 2, 2011.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Katika kutalii kwangu, nimepata kuitembelea nchi moja iitwayo kusadikika. Katika hiyo nchi, wananchi wanamlaani rais wao. Wanamuombea laana ya milele rais huyu wa ajabu anayetawala nchi kama yuko kwenye mdundiko wa kizaramo.

  Nadhani rais huyu anawaza midundko, miduara,kichen pati,sendoff, na safari za kujiuza marekani kuliko hali ngumu ya maisha ya Wanakusadikika. Sasa amezinduka baada ya kuona kinachoendelea Tunisia, Misri na Libya. ila pamoja nakuzinduka wananchi wake wenye hasira naye wanasema kwamba hataweza kufanya lolote kwani kichwani hana jipya zaidi ya midundiko na kutabasamu anapoona nzi wakipita mbele yake

  Rais huyu wa nchi ya kusadikika, ni mdini, mchonganishi na mtu mwenye kinyongo na raia wake. Amekuwa akiwajali marafiki zake na mafisadi kuliko raia wa kawaida. Rais huyu aliyetunukiwa shaada nyingi za falsafa amekuwa kama kikatuni fulani kwenye nchi yake. Urais ameugeuza kama mali ya familia yake. Rais analiacha taifa kwenye majonzi makubwa yeye anaelekea kutalii na kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya watu wengine huku nchi yake ikiwaka moto. Raia wamechoka na rais anayeendekeza starehe kuliko maslahi ya taifa. Rais ameiuza nchi. Kucheza ngoma na mduara kwenye ikulu ya kusadikika ina maana kubwa kuliko kutafuta suluhisho ya wanasadikika

  Kwa bahati mbaya kuyakumbatia mafisadi ndo chanzo cha kuangamia kwake... Laiti rais wa kusadikika angalijua mapema !
   
 2. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Rais Mcheza Kiduku Ikulu
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Kwa bahati mbaya kuyakumbatia mafisadi ndo chanzo cha kuangamia kwake... Laiti rais wa kusadikika angalijua mapema !
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Bahati nzuri tunalijua jina lake ni K J yaani KUBWA JINGA!!! :rain::rain::rain::rain:
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Rais ambae analalamika kila wakati na pia eti hajui kwa nini nchi yake ni masikini!
   
Loading...