Rais wa Marekani alaumiwa kwa kuwaaibisha viongozi wa Afrika

Rais wa Marekani alaumiwa kwa kuwaaibisha viongozi wa Afrika

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
169
Reaction score
287
mmexport1752646721382.jpg
Marekani hivi karibuni iliandaa mkutano kati yake na nchi tano za Afrika ambazo ni Gabon, Guinea-Bissau, Mauritania, Senegal na Liberia. Lakini kwenye mkutano huo, Rais Donald Trump wa Marekani alifanya vitendo vingi visivyofaa kwa viongozi wa nchi hizo za Afrika, na jambo ambalo limewakasirisha Waafrika wengi, wakiona Marekani imeaibisha nchi za Afrika tena.

Katika mkutano huo, Trump alisifu kiwango cha Kiingereza cha Rais Joseph Boakai wa Liberia, ambapo alimuuliza amejifunza wapi Kiingereza vizuri na elimu yake, na kuuliza amesomea wapi, na alipoambiwa kuwa ni Liberia, rais Trump alimsifu kwamba anazungumza vizuri lugha ya kiingereza, tofauti na marais wengine waliokuwa kwenye mkutano huo.

Video ya tukuio hilo la kufedhehesha ilienea mara moja kwenye mitandao ya kijamii, na watumiaji wa mtandao kutoka nchi mbalimbali walimcheka rais Trump kwa kutojua kwamba lugha rasmi ya Liberia ni Kiingereza, na kumkosoa kwa kuwadharau viongozi wa Afrika.

Baadhi ya Waliberia walikasirika sana na matamshi ya rais Trump. Mwakili wa vijana wa Libeŕia Archie Tamer Harris alisema anahisi kutukanwa kwa sababu nchi yake ni nchi inayozungumza Kiingereza, na kusema kuwa alichokifanya rais Trmp si pongezi, bali ni ukweli halisi ambapo watu wa Magharibi bado wanawachukulia Waafrika kama watu wasio na elimu.

Mwanadiplomasia wa Liberia ambaye hakutaka jina lake litajwe pia alisema kauli kama hizo zinaonyesha dharau kwa rais anayetokea nchi inayozungumza Kiingereza barani Afrika.

Video nyingine iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii ilionesha kuwa viongozi wa Afrika walizungumza kwa zamu katika mkutano huo, na rais Trump alizidi kukosa subira, na ilipofika zamu ya Rais Mohamed Ould Ghazouani wa Mauritania, Trump alishindwa kujizuia. Kwanza alifanya ishara ya kuhimiza maendeleo, akitikisa kichwa, na kumkazia macho Rais Ghazouani, na mwisho alisema kwamba hataki kutumia muda mwingi kwenye suala hilo na kumtaka kuharakisha kwani kuna mambo mengine yanayofuata.

Vitendo hivyo vya rais Trump pia vimekosolewa kwenye mitandao ya kijamii. Mwanamtandao wa Marekani alilalamika kwa huzuni akisema, Trumo ni rais asiye na uwezo, huku mwanamtandao mwingine akisema, siku si nyingi zijazo, viongozi wa kigeni hawatafanya ziara nchini Marekani ili kukwepa kudharauliwa.

Kabla ya matukio hayo, rais Trump alikosolewa mara kadhaa kutokana na matamshi au vitendo vyake kuhusu nchi za Afrika.

Mwezi Mei mwaka huu, alimlaumu Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kwamba wakulima wa kizungu nchini Afrika Kusini walikuwa “waathirika wa mauaji ya kimbari,” lawama ambayo haina msingi hata kidogo.

Mwaka 2018, wakati Trump alipokuwa katika muhula wake wa kwanza wa rais wa Marekani, aliwaita wahamiaji Waafrika wametoka “nchi duni.”
 
Trump yupo Sahihi. Waafrika Hatujielewi Tunataka Nini?
Kabisa kabisa ata mie ningekuwa mzungu ningewadharau tuu waafrika. Wee mijitu imepewa akili na mungu lakini hawazitumii hizonakili. Kazi kuwaza ngono tuu kama mzabzab hapa alafu eti wananicheka🤣🤣🤣🤣

Ila waafrica tuna mambo ya kifala ujue...eti tunamsifu mtu na masters anauza kande🤣🤣🤣🤣. Alafu tunas3ma tunataka kuwa donor kantriiii while we embrace survival mode mentality. What a load of bullocks!!!
 
Rais wa Marekani Donald Trump ukimuangalia kwa macho matatu na kumsikiliza kwa masikio ya ndani utagundua ana kitu cha tofauti na cha kipekee sana kuliko watangulizi wake hasa kwenye sera za nchi ya dunia ya tatu zilizo Africa.

Waafrika kwa kutokujua na kutambua watamchukia Donald Trump kwa haiba yake na kutomungunya maneno katika kuusema UKWELI.

Kitendo cha kuwaita waafrika Shit hole countries ni UKWELI MCHUNGU ambao viongozi wengi wa Afrika hawependi wala kutamani kuambiwa ukweli.

Trump anajaribu kuwaonyesha na kuwaambia waafrika kuwa nyie mnauwezo na mmejaliwa kila kitu hamuhitaji misaada isiyo ya lazima kutoka Marekani.

Afrika kwa kuwa sera zake zimekuwa zikilemaa na kutegemea misaada ya Marekani inamuona Trump kama Rais mkatili wakati ndio Rais ambaye anataka na kutamani kuona viongozi wa Afrika wakijitegemea na kuleta maendeleo katika nchi zao

Alipoingia madarakani ameanzisha DOGE( Department of Government Efficiency) Marekani sababu anatambua uchafu mwingi ambao umekuwa ukifanywa na serikali yake.

Kwa hiyo tutake au tusitake lazima tukubali maumivu ya uchungu wa kukataliwa na kusemwa vibaya ili tuweze kubadili mitazamo yetu ya kuwa tegemezi na kuanza kujitegemea.

Binafsi namuona na kumchukulia Donald Trump kama shujaa ambaye ataisaidia Africa ijifunze in a hard way.

Tukitegemea na kuendelea kusubiri kuletewa au kufadhiliwa mambo muhimu kama madawa kutoka ufadhili wa Marekani ni ULEMAVU WA FIKRA.

Ukiangalia bajeti za serikali za Afrika hazijikiti katika kuboresha na kutoa kipaumbele kwa masilahi na manufaa ya wananchi wao badala yake inatumika kwenye kuboresha maisha na masilahi ya vikundi vya watu wachache ambao ni wanasiasa na washirika wao.

DONALD TRUMP AMEVUNJA CHUNGU CHA UFADHILI WAAFRIKA TUACHE KULIA LIA TUJIPANGE UPYA.
 
Kabisa
 
Back
Top Bottom