Rais wa Guinea, Alpha Conde apinduliwa na Jeshi

hito

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
501
913
Nimeona sehemu wanasema rais wa Guinea amepinduliwa na wanajeshi waasi na anapelekwa kwenye mahakama ya kijeshi
View attachment 1925186

===
GUINEA: WANAJESHI WAMPINDUA RAIS

Wanajeshi wamefunga mipaka ya Guinea na kufunga anga baada ya kufanya mapinduzi na kutangaza kutoitambua Katiba iliyorekebisha na Rais Alpha Conde uwezo wa kuwa Rais kwa mara ya tatu

Mamady Doumbouya amesema Umasikini na rushwa iliyokithiri imefanya wapindue nchi. Hivi karibuni kulikuwa na ongezeko la tozo na mafuta yalipanda kwa 20%

Wanajeshi wametangaza kuwa nchi hiyo itakuwa chini ya serikali ya mpito baadhi ya video zikimuonesha Rais Alpha Conde akiwa chini ya maafisa wa Jeshi
 
Nimeona sehemu wanasema rais wa Guinea amepinduliwa na wanajeshi waasi na anapelekwa kwenye mahakama ya kijeshi
View attachment 1925186

76F7F27E-53A1-4973-86D6-D16A29B0B32A.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sijui bwana hito unaharaka gani kutuletea habali isiyoeleweka......rudi kajipange kwanza utuletee habali iliyonyooka...
 
Jaribio la mapinduzi linaendelea nchini Guinea, mpaka muda huu vikosi maalum vilivyoasi tayari viko ndani ya Ikulu ya Rais na vimeondoka na raisi wa nchi hiyo kuelekea naye pasipo fahamika.

20210905_181034.jpg

Hizi ni picha ambazo baada ya vikosi hivyo kuongia ikulu walipiga naye picha na kupiga naye picha na Rais anaonekana kukamatwa, askari wakimpiga picha.

Picha ya juu ni Rais wa Guinea Alpha Condé aliyekamatwa na jeshi alionekana kwenye mitandao ya kijamii.


20210905_181043.jpg


Picha ya video ikimuonyesha rais huyo akiwa kakaa na vikosi hivyo vya waasi vikipiga naye picha kabla ya kuondoka naye.

Wananchi katika mji mkuu wa nchi hiyo Conakry wameonekana wakishangilia mapinduzi hayo wakati wanajeshi walipokuwa wakipita barabarani.




Kamanda anayeongoza mapinduzi hayo ya kijeshi nchini humo inasemekana ni Luteni Mamady Doumbouya ambaye alikuwa mtu karibu kwa upande wa rais wa nchi hiyo.

20210905_185011.jpg

☝🏾Luteni Mamady Doumbouya
 
Back
Top Bottom